Wanaosema kujenga ni kuzika pesa

Unaizungumzia nyumba iliyojengwa hewani au kwenye hiyo ardhi unayoisema inaongezeka thamani?
 
Mambo mengine ni akili ya biashara tu. Kununua viwanja inategemea na eneo, kama unataka fedha ya haraka usinunue porini sana, Dodoma watu wamepiga fedha sana hadi hata sasa. Ilikuwa kununua maeneo kwa bei rahisi, baadae mtu anapima viwanja na kuuza. Biashara hii ni nzuri kwa yale maeneo mji unapoelekea au maeneo ya kimkakati. Hata biashara ukiiendea vibaya unapigwa vizuri tu.
 
Real estate ni biashara kubwa sana tu na imetajirisha watu wengi.

Wana timing zao, mda wa kununua, location za kununua, na namna ya kucheza na mabenki etc.
 
Sehemu yeyote ile.
Hivi kipi cha ajabu hapo?
Ardhi inapanda thamani, nyumba inashuka thamani.
Tumia uwiano mzuri ili ujenge nyumba kwa kutumia ardhi badala ya kutumia ardhi kujenga nyumba.
"Tumia uwiano mzuri ili ujenge nyumba kwa kutumia ardhi badala ya kutumia ardhi kujenga nyumba." Naomba ufafanuzi hapa mkuu.
 
Kama nakuelewa hivi.
 
Acha uwoga wa maisha wewe, panga, achana na maujenzi.
 
Laki 1 ya mwaka 70 sio laki 1 ya mwaka 2022. Angalia ktu inaitwa "money value" au "purchasing power" ya hela
Harafu mueleze kilichoipa thamani sio nyumba,ni location ya kiwanja . Mwambie achekeche kichwa, anunue viwanja mjini...

Usijenge nyumba kwa mateso, tafuta pesa unaweza kujenga kwa miezi miwili tu. La msingi jitwalie viwanja ,kata hati.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…