Wanaosema kujenga ni kuzika pesa

Nakuelewa saana mzee
 
Trump anajenga kwenye prime location pia hatumii cash kujenga, ni mkopo wakati watz wanadunduliza savings zao kwa ajili ya kujenga kwa miaka.
Msamehe tu, huyo jamaa inabidi utenge muda haswa wa kumuelewesha.
 
Huyo aliyejenga nyumba kariakoo mwaka 1970 saizi umemuona yupo katika hali gani? nyumba tunajenga kama security ya maisha tu kwamba ikitokea siku huna ajira basi usishindwe kulipa kodi ukae kwako. Kama sio mfanyabiashara ukijenga nyumba umefukia pesa shimoni. Unajenga nyumba ya milion 70 mpangaji analipa kodi sh laki 2. mpaka ije irudi pesa uliyoifukia hapo ni miaka 20 ijayo baada ya hiyo miaka 20 nyumba yako inaonekana kama kibanda cha mganga wa kienyeji. Wafanyabiasha wanajenga nyumba wanaenda benk wanakopea mzigo wa maana wanauzungushia ndani ya muda mfupi wanapata faida kibao kodi za wapangaji ndo marejesho ya mkopo
 
Rudi na haya mawazo ukiwa na 55 years old
Mtu aliye serious na biashara inayofanya uweze kulipa 2M per month kama kodi ya nyumba atakula kukosa sehemu ya kuishi at 55 yrs??? Labda akosee mahala.

Tatizo linaanza pale ambapo mtu ndo kwanza ana 5M benki, tayari akili yake unawaza kuzitumia hizo hela kujenga badala ya kuziendeleza😅. Matokeo yake ni kujenga nyumba ambayo mpaka unakuja kuimaliza tayari ilishapitwa na fashion.
 

Labda tunapishana lugha.

Nisome vzr sehemu zote nilizopita utanielewa.

Mara zote nimetumia neno UWEKEZAJI au BIASHARA YA UWEKEZAJI!

Nadhani neno UWEKEZAJI linaeleweka maana yake!
 
Hivi Yesu alijenga nyumba au alinunua nyumba?
Au alikuwa mpangaji?
 
Unakuta mtu ni kijana wa 25-35 yrs ana 7M eti anaweza kujenga, huo sip upuuzi wa kukariri maisha??

Kwanini usipange nyumba hâta ya 200K per month (kulingana na hiyo hela), kisha inayobaki ukiingiza katika mpango kazi??

Unakuta hiyo 7M anaitupia kwenye ujenzi yote inaishia kwenye msingi kisha anaanza kuitafuta 7M nyingine kwa miaka hâta SITA maana kazini analipwa 300K au 400k (kabla haujakata hela za matumizi binafsi)
 
Hilo kundi la bata ndio huwa na tabia ya kuwapotosha wenzao na kuwakatisha tamaa kujenga ni kuzika pesa ilihali amepanga nyumba mjini vijiroom 2 anajibana hapo na watoto 3 na beki tatu juu na analipa kodi na inamuumiza kichwa.
 
Hakuna kitu kama pesa kuongezeka thamani iwe benki au kununua ardhi, ni upuuzi tu….unawezaje kulinganisha thamani ya kitu kwa nyakati tofauti?

Waiter, one for the lord.[emoji1634]
 

Kiufupi nilifikia uamuzi wa kujenga kutokana na kero za kupanga ,wanaopanga wananielewa nachomaanisha hapa,i wish nikitoka kazini nikapumzishe akili nyumbani kwangu.
Alaf sio kila anaejenga hana viwanja vingine tunavyo sana na hatulipwi hio hela ya mbuzi uliyotaja hapo
 
Daaah!!! Nimepitia comments zote, pasipo na mashaka wale wa nunua viwanja zaidi kuliko kujenga majumba wamekuwa na hoja zenye uzito, itoshe tu kusema WAMESHINDA.

Muhimu zaidi, lazima uwe na nyumba yako hata ya kawaida ya kuishi, then ndo wekeza kwenye viwanja, siyo umepanga na unakazana kununua viwanja.

Kuishi kwako Kuna raha yake, mara hapa umeweka kabustani, pale umeweka Banda la kuku, UPO KWENYE MJI WAKO UMETULIA HAKUNA WA KUKUFOKEA.
 

Wanaosema kujenga sio kuzika pesa ukifika Chato, musoma mjini, iringa, Tanga, Hai mjini, kondoa mjini, utapata jibu.​

 
Unaweza kuitunza aridhi ya mikocheni ikiwa tupu bila kuendelezwa kwa miaka 5?
Hakuna anayekatazwa asijenge mkuu! Kujenga sawa jenga lakini, suala linabaki pale pale Ardhi na Nyumba kinachoongezeka thamani ni Ardhi na sio nyumba elewa hilo ... !

Mtu anapo nunua kiwanja chenye nyumba ya udongo pale kariakoo kwa billion kadhaa anacho nunuwa pale sio ongezeko la thamani ya hio nyumba bali ni kiwanja !

Nyumba na Gari hivi vyote kwa aslimia kubwa ni liability tu na sio asset..
 
Hao wanaopata shida, wanaipata sio kwakua wamepanga bali ni sehemu walizopanga.

Nyumbani kwangu ni Dsm ila nipo Geita for 8 years now, huku napo nijenge?
 
Muda huu Donald Trump anajenga the tallest bulding in the world
Yes hiyo suo nyumba ya kuishi mkuu ..jaribu kuelewa .. nyumba yako ya kuishi haikuingizii pesaaa,

Kitu utakachojenga na kukuingizia pesa tena iwe kwenye location nzuri majengo kama ni hotel, lodge, guest house , restaurants , na kidogo ni apartment zinazoweza kuwa sehemu yenye uhitaji mkubwa (hawa ndio wanaopata faida),

ila wewe unayepangisha nyumba za kuishi chanika , mbagala hukoni umeweka tu pesa zako... unarudisha ghrama za ujenzi kidog kidogo na itakuchukuwa muda mrefu kuanza kupata faida !
 
Watabisha sio kwasababu hawaelewi au wana point za maana, ila watabisha kwasababu hawataki kushindwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…