Wanaosema Rais Magufuli hajui Kiingereza leo amewasuta

Mungu aturehemu sisi tunaojadili kuongea lugha ya taifa lengine kwa ufasaha karne ya 21.....Moja ya mafanikio ya waTz nikumpeleka mtoto "English-medium school"
 
Kwa kiingereza chake anajitahidi, kawaida wengi wanaosoma masomo ya science viingereza vyao huwa wanavijua wenyewe.
Ni wabongo wote tu mkuu. Kiingereza hakiwapendi. Ndiyo maana wakenya walijaa ktk shule za English medium, mpk hapo vikwazo dhidi yao viliooanza ndo wakapungua
 

 
Siku moja Rais wetu atoe hotuba kwa kiingeleza mwanzo mwisho !
 
Hiyo ni lugha tu Kama lugha nyingine, hata ungeijua namna gani kama kichwani Hanna kitu, Wala hiyo lugha haikusadii lolote.
sizitaki mbichi hizo! Can you make your sentence above (hiyo ni lugha....... in English)! Usitazamie please
 
Kwahiyo ni sawa na kusema Magufuli alikuwa anaona kichina china tu wakati akiwa chuoni kwamba lugha ya kufundishia hakuwa anaielewa?
 
Mr much know kwani ukisema haujui Kiinglish kuna shida gan?
Jiwe haujui English Watanganyika tunajua kama haujui
Ameweka hoja zake kwamba amesoma hapo UDSM miaka mitatu na lugha iliyokuwa ikitumika ni kiingereza sasa utasemaje hajui hiyo lugha?na pia ameishi London mwaka mmoja na lugha inayotumika kule kwa mawasiliano ni kiingereza sasa utasemaje hajui kiingereza?
 
Hujui kwani hukumbuki swali alilokusaidia museveni kukupa tafsiri na ukajibu utumbo
 
Ila hao kutokusoma kwa kutumia english sio sababu ya wao kutokujua english,kwa sababu soma la english lilikuwepo wakati wanasoma na lengo la hilo somo ni kufunzwa lugha ya kiingereza sasa iweje wasijue kama walifundishwa english?
 
Kiswahili kimeachwa na baba wa Taifa ?

Ndiyo maana hata kingereza hajui.
 

Hili la kujitoa kimasomaso ni tamu kwa mijamaa ya chama fulani.😂😂😂😂😂
 
Ngoja siku aje Joe Biden hapo ndo tutajua yaliyomo yamo au hayamo..[emoji23]
Mkuu kwani Joe Biden anakijua au na yeye anakitumia kama lugha mama na ya syllabus,tufanye na yeye aongee English + kiswahili sanifu uwone atakavyojing'ata apo meza kuu
 
Naona leo ndo kapata ujasiri wa kumjibu saa8...

Basi atuambie alipo..
 
Ni mwendelezo wa kusema uongo aliozoea. Magu anajua kiingereza?
 

Kusema ukweli bila ya mapendeleo yoyote, mzee baba kiingereza anakipenda. Kushindwa kukimudu tu ndiko kunako mfikisha hapa:

"Sizitaki mbichi hizi."

Ingekuwa dhana ya promotion ya Kiswahili kweli angekuwa anachomeka chomeka kiingereza fyongo fyongo kila anapopata nafasi hiyo?

Kina Ping, Merkel, Putin na wengine wa namna hiyo ambao mijamaa ya chama fulani ingependa kwa ghiliba eti tumfananishe nao, katu hawachomeki vijimaneno au sentensi uchwara za kiingereza kwenye kauli zao zozote.

Mataga na yachutame tu hii mbombo nkafu!
 
Ila hao kutokusoma kwa kutumia english sio sababu ya wao kutokujua english,kwa sababu soma la english lilikuwepo wakati wanasoma na lengo la hilo somo ni kufunzwa lugha ya kiingereza sasa iweje wasijue kama walifundishwa english?
Hujanielewa..... Wao ni kama tu kiswahili nchini Uganda, kinafundishwa kama somo tu ambalo ni optional sio compulsory lakini TZ kiswahili ni lugha ya kufundishia masomo yote primary school (ambapo hushape uelewa wa mwanafunzi)

Kwahiyo probability ya mganda kujua kiswahili ni ndogo ila kwa Mtanzania ni kubwa. Hivyo same case to Putin ni ngumu sana kuwa competent kwenye english ilihali aliisoma kma somo tu na sio lugha ya kufundishia.

So bado JPM is in for it......hawezi jitetea kwa mgongo wa Putin wakati ni context tofauti. Wenzetu mpaka kemikali na software sipo developed kww lugha yao sie mpaka manual huko maabara ni za kiingereza kitupu so usipofahamu lazima tukuzodoe tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…