Wanaosema Rais Magufuli hajui Kiingereza leo amewasuta

Wanaosema Rais Magufuli hajui Kiingereza leo amewasuta

Badili kichwa Cha habari kisomeke
"Wanaosema Magufuli hajui kiingereza leo wamekumbuka"
 
Inferiority complex....huyu jamaa bana asijitetee tu kwenye kiingereza maana hata kiswahili lugha yake ya taifa bado haimudu vizuri.
 
“Nilipoingia madarakani nikaanza kutoa hotuba kwa Kiswahili, niliambiwa sijui Kiingereza wala sikujali, UDSM nimekaa miaka mitatu nikisoma masomo yangu ya Sayansi, Chemistry na Mathematics zote zinaandikwa kwa Kiingereza,lakini Mtu akasema sijui Kiingereza”-JPM kwenye Siku ya Sheria Dodoma leo

“Nimefanya PHD bado wanasema sijui Kiingereza, na nikakaa mwaka mzima Uingereza, sijui nilikuwa nazungumza Kisukuma kule!, wakasema sijui Kiingereza, niliamua kuzungumza Kiswahili na kuki-promote kwasababu ni lugha iliyoachwa na Baba wa Taifa”-JPM
View attachment 1691833
 
3
Yes mkuu kukosea maana yake sijui na sio dhambi kwa sababu kila siku tunajifunza.

Vipi wewe hapo juu INAKISEA ndio nini ni kifaransa au utashupaza shingo kwamba hujakosea?
Unaweza kumrekebisha mtu wakati huohuo unafanya kosa (unakosea)
😂😂😂😂
 
Kwa kiingereza chake anajitahidi, kawaida wengi wanaosoma masomo ya science viingereza vyao huwa wanavijua wenyewe.
Kusoma science sio sababu ya kutojua kiingereza wala hakuja justification ya kutokujua kiingereza kisa umesoma science
 
Kumbe wote waliopitia vyuo vikuu wote wanajua kiingereza! Somo pekee linalothibitisha kuwa unakijua kiingereza ni la kiingereza.
 
Kadri anavyotumia nguvu nyingi kujibu hoja hii ya kutokujua inglishi ndio anavyozidi kuharibu bora akae kimya
 
Maisha haya mtu unatakiwa uwe na maarifa tu...

Lugha ni chombo cha mawasiliano na si lazima sana ujue kila lugha...
 
Kwa mazungumzo yale inaonekana wazi kabisa kuna kikundi cha watu hawataki au wanapinga kabisa matumizi ya lugha ya kiswahili, lkn huo ni unafiki mkubwa maaana huwezi kuwa mzalendo wa kweli halafu wakati huo huo unadharau lugha ya Taifa lako,
huwezi kujifanya una muenzi baba wa taifa halafu wakati huo huo unadharau lugha ya kiswahili amabayo imeasisiwa na Baba wa Taifa hili na ndiyo kitu pekee kilicho tuunganisha watanzania wote hadi leo hii tuko wamoja.
najivunia kuwa na Rais Jasiri shujaa asiye tetereka maenye kujivunia lugha yake.
Hongera sana JPM

Sent using Jamii Forums mobile app
 
“Nilipoingia madarakani nikaanza kutoa hotuba kwa Kiswahili, niliambiwa sijui Kiingereza wala sikujali, UDSM nimekaa miaka mitatu nikisoma masomo yangu ya Sayansi, Chemistry na Mathematics zote zinaandikwa kwa Kiingereza,lakini Mtu akasema sijui Kiingereza”-JPM kwenye Siku ya Sheria Dodoma leo

“Nimefanya PHD bado wanasema sijui Kiingereza, na nikakaa mwaka mzima Uingereza, sijui nilikuwa nazungumza Kisukuma kule!, wakasema sijui Kiingereza, niliamua kuzungumza Kiswahili na kuki-promote kwasababu ni lugha iliyoachwa na Baba wa Taifa”-JPM
View attachment 1691833
Tusi pekeche maneno....

Iko ivi

Kwenye lugha yeyote Kuna hizi components 4.

1. Speaking skills
2. Reading skills
3. Writing skills
4. Listening skills

Ukichunguza hizo components lazima utagundua Kuna udhaifu kwenye component kadhaa.......

N.b
Pia tukumbuke kua kuongea kingereza kizuri sio kwamba ndio mtu ana akili sanaa....
 
Back
Top Bottom