Wanaosema Rais Magufuli hajui Kiingereza leo amewasuta

Wanaosema Rais Magufuli hajui Kiingereza leo amewasuta

Ni sawa na mimi nimshangae Joe Biden kwa kutokujua kifaransa au kiswahili

Ni utoto!
kweli mkuu wakati huo unamshangaa kwa kutojua lugha hizo anakuwa kasoma na kahitimu hadi elimu ya juu kwa lugha hizo na hazijui utaachaje shangaa
 
Rubbish, anajua kiingereza gani, cha kusema “in addition of that” mbele za watu bila aibu huku akijiita Dr.
 
..Je, Putin anazungumza Kirusi ambacho ni broken?

..Manaake huyu bwana mkubwa wa hapa kwetu Kiswahili chake ni kibovu.
Ametamka mara nyingi kwamba kiswahili chake ni cha kisukuma.
 
“Nilipoingia madarakani nikaanza kutoa hotuba kwa Kiswahili, niliambiwa sijui Kiingereza wala sikujali, UDSM nimekaa miaka mitatu nikisoma masomo yangu ya Sayansi, Chemistry na Mathematics zote zinaandikwa kwa Kiingereza,lakini Mtu akasema sijui Kiingereza”-JPM kwenye Siku ya Sheria Dodoma leo

“Nimefanya PHD bado wanasema sijui Kiingereza, na nikakaa mwaka mzima Uingereza, sijui nilikuwa nazungumza Kisukuma kule!, wakasema sijui Kiingereza, niliamua kuzungumza Kiswahili na kuki-promote kwasababu ni lugha iliyoachwa na Baba wa Taifa”-JPM
View attachment 1691833
Hayo maelezo ya kujitetea angeyasema basi kwa Kiingereza tuache kubishana
 
Mimi nakubali kuwa mjinga. Acha jinga la mwaka, naweza kuwa jinga la karne, lakini ukweli unabaki kuwa pale pale, fani na lugha ni vitu tofauti. Kuna watanzania wengi wana Ph.D. za uchumi, fizikia, madawa, uhandisi, n.k. Kikubwa kwao ni kujuwa walichosomea na siyo lugha. Kwanza kuna wengine hawakutumia Kingereza kwenye hizo Ph.D. Wengine walisom,a Urussi, Ujermani, Ufaransa Hispania, na walitumia lugha za huko kwenye Ph.D.
да .. вот ты где
 
..aliyemshauri Raisi kuzungumzia hayo ni nani?

..Jpm amekuwa madarakani huu ni mwaka wa 6, hivi anahitaji kujieleza na kujitetea kwamba anaimudu lugha ya Kiingereza?
2016 alichekwa hadharani katika tukio kama la leo kwa kuboronga Kiingereza, nafikiri lile tukio lilikuwa likimkera.
 
Nani kasema Ph.D. holder lazima awe mater of English. Kwani Ph.D. lazima ifanwe kwa Kingereza? Nchi nyingi Ph.D. zinafanywa kwa lugha zao, siyo Kingereza. Muhimu kwenye Ph.D. ni somo. Kama Ph.D. ni kemia lazima uwe matser wa kemia siyo kingereza. Ila tutakushangaa kama una Ph.D. ya Kingereza huku hujui kingereza cha kuandika.
Nchi zipi? Umefanya PhD? Commonwealth countries wanatumia lugha gani katika PhD level?
 
Back
Top Bottom