Wanaosema Rais Magufuli hajui Kiingereza leo amewasuta

Wanaosema Rais Magufuli hajui Kiingereza leo amewasuta

eti alikaa Uingereza! 😂😂😂😂😂😂labda Uingereza ya chato 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
“Nilipoingia madarakani nikaanza kutoa hotuba kwa Kiswahili, niliambiwa sijui Kiingereza wala sikujali, UDSM nimekaa miaka mitatu nikisoma masomo yangu ya Sayansi, Chemistry na Mathematics zote zinaandikwa kwa Kiingereza,lakini Mtu akasema sijui Kiingereza”-JPM kwenye Siku ya Sheria Dodoma leo


“Nimefanya PHD bado wanasema sijui Kiingereza, na nikakaa mwaka mzima Uingereza, sijui nilikuwa nazungumza Kisukuma kule!, wakasema sijui Kiingereza, niliamua kuzungumza Kiswahili na kuki-promote kwasababu ni lugha iliyoachwa na Baba wa Taifa”-JPM
View attachment 1691833
 
Hao mnaojua kiingereza mna nini cha ziada ? Kazi kushinda JF tu njaa tupu.
 
Raisi Magufuli ni sawa na maraisi Putin, Xi Jinping, Angela Markel, Emanuel Macron na wengine ambao hutumia lugha mama.

Hicho kiingereza ni lugha kama lugha zingine za kawaida sana.

Kufahamu kuzungumza kiingereza hakumaanishi wewe umesoma sana na kuelimika.
Hao wote wamesoma mpaka vyuo vikuu kwa lugha za kwao ila Jiwe wanamzodoa kwasababu kasoma vyuo vinavyofundisha english alafu kashindwa kuwa fluent kwenye matamshi na mpangilio.
Ingekua na sisi tunafundisha kiswahili mpaka level ya PhD sidhani kama kuna mtu angemzodoa.
 
Tuambie Nani ambaye Hana broken..ambaye anaongea Kama mzungu mwenyewe..Nani..???!

..Jpm hata Kiswahili anazungumza cha kuungaunga.

..Kiongozi na Raisi wa nchi ambayo Kiswahili na lugha yake ya taifa hapaswi kuzungumza Kiswahili kibovu kama cha Jpm.

cc Kiranga, Nguruvi3
 
Raisi Magufuli ni sawa na maraisi Putin, Xi Jinping, Angela Markel, Emanuel Macron na wengine ambao hutumia lugha mama.

Hicho kiingereza ni lugha kama lugha zingine za kawaida sana.

Kufahamu kuzungumza kiingereza hakumaanishi wewe umesoma sana na kuelimika.

..Je, Putin anazungumza Kirusi ambacho ni broken?

..Manaake huyu bwana mkubwa wa hapa kwetu Kiswahili chake ni kibovu.
 
"My teaching experiences in different parts of the world convinced me that something is wrong with English education. Everywhere I went, it was the same situation. The students were bored, frustrated, stressed, and nervous. Most students, even after years of studying English, failed to speak the language fluently. You are not alone, because it’s a global problem.

One of my students, Seiko from Japan, described this combination of failure and stress as “English trauma.” Seiko said that she hated English. She felt that learning English was boring and stressful and speaking English was even worse. In fact, the thought of speaking to a native speaker immediately made Seiko feel extremely nervous and shy. Seiko felt she had developed a psychological problem with English and had named it “English trauma.” A “trauma” is a deep wound or injury. “How sad,” I thought to myself, “that so many people now think of English as a kind of injury or mental disease.”

Throughout my teaching career I’ve met many students who had similar feelings about English. I discovered that Seiko was not alone. Rather, “English trauma” is a globa epidemic. Though most people feel they must learn to speak English, very few seem to enjoy it. Most who learn the language struggle with the same feelings of nervousness and frustration that Seiko had.

As I encountered this problem more and more, I began to look for the root causes. I realized that before I found a solution, I needed to understand the problem. Just as a doctor must first diagnose a disease before treating it. Think about it. What is the cause of all this misery and failure? Why do so many people fail to speak English effortlessly despite years of study? What is wrong with English education?"

Effortless English by A.J Hoge
 
Ngoja siku aje Joe Biden hapo ndo tutajua yaliyomo yamo au hayamo..[emoji23]
Nakumbuka alivyokuwa Uganda alipigwa swali na muandishi wa BBC English Service,ilibidi mzee Museveni aingilie kati kumtafasilia. Maana jiwe alitoka kapa kabsa akabaki anatoa macho tu! [emoji86][emoji86][emoji86][emoji12][emoji12]
 
mambo yanakwenda ...saaa hivi tunaheshimiana .... Wee kaa ngoja....

Kiingreza...ndo utatoboa...
 
Uko sahihi mkuu, unaona sasa mpaka nakosea. Na yeye (jiwe) akubali tu hii lugha ya kuja tu kutoijua vizuri sio tatizo.
... halafu mtaanza ku-question mengine! Mara Mfumo wetu wa elimu; mara thesis iko wapi. Bora kukomaa hivyo hivyo mtajua wenyewe.
 
Back
Top Bottom