Wanaosema Rais Magufuli hajui Kiingereza leo amewasuta

Wanaosema Rais Magufuli hajui Kiingereza leo amewasuta

Basi hayo maelezo yake angeyaongea kwa kiingereza fluently ili tuamini, aseme tu ukweli hajui kiingereza mbona sie wengine tuna ma PhD lakini lugha inatutatiza.

Na wewe Mbona huandiki maelezo haya kwa English ?

Mbona nyie mnatukuza sana English, English ni lugha kama lugha nyingine
 
Magufuli ajuwe Kingereza safi au asijuwe siyo hoja. Kila mtu anatakiwa kujuwa lugha yake, Mjerumani anatakiwa kujuwa Kijermani. Mwingereza kwake Kingereza lazima. Mtanzania lazima ajuwe Kiswahili na anaweza kuiongezea lugha yake ya asili, kwa mfano Magufuli tunategemea ajuwe Kisukuma. First language ni ile lugha anategemewa kuifahamu.

Nafikiri wenzangu mmewahi kuwasikia Wamarekani, Waingereza, n.k. wakijaribu kuongea Kiswahili lakini huwa kibovu. Wageni wa kimataiofa wakitoka nchi zisizoongea Kingereza wakienda nchi zinazoongea Kingereza huongea Kingereza lakini hicho Kingereza sioyo Kizuri kama cha wazawa. Kwa hiyo kuongea lugha ya kigeni bila kukosea ni kitu kizuri lakini pia ukifanya makosa machache siyo aibu, maana siyo lugha yako. Mbona watu toka mataifa mengine (hasa wazungu) wakiboronga kingereza hatuwasemi?

Kama alivyosema Magufuli mwenyewe, kamaliza sekondari akitumia Kingereza. Amepeta stashahada (degree) ya kwanza akitumia Kingereza. Amepata master akitumia Kingereza. Amepata Ph.D. aklitumia Kingereza. Mbona huko kote hakushindwa kwa sababu ya kutojuwa Kingereza. Hivi ni kweli hao mnaomkosoa mnajuwa Kingereza? Kama mnajuwa Kingereza mbvona mnaandika para moja huku kukiwa na makosa? je, mkiambiwa mhutubie siyo kashikashi. Mwisho ya yote, lugha siyo akili. Luggha kazi yake ni kutuwezesha kuelewana. Kama unaweza kumuelewa mtu alikuwa na maana gani hasa anapotumia lugha isdito yake, inatosha.
Utatetea sana lakini ukweli utabaki pale pale,,,
Akubali tu hawezi
 
Raisi Magufuli ni sawa na maraisi Putin, Xi Jinping, Angela Markel, Emanuel Macron na wengine ambao hutumia lugha mama.

Hicho kiingereza ni lugha kama lugha zingine za kawaida sana.

Kufahamu kuzungumza kiingereza hakumaanishi wewe umesoma sana na kuelimika.
Wapinzani watapinga.
 
Hapa Jamii inakosea hata kama hamumpendi rais wa nchi, kwani kujua kingereza au kutokujua ni dhambi au kosa la jinai?? Tufanye ninyi mnajua Rais wetu yeye hajui, furahini sasa..
Kwani kusema mtu fulani hajui au hawezi kitu fulani ndio maana yake kumchukia/kutompenda?...

Naona kama watu kama ninyi mnapotosha sasa
 
Aibu haiji kwa kutokujua kiingereza vizuri, watanzania wanahitaji maji, barabara, mahospitali na huduma zingine za kijamii ambazo hazihitaji ujue kiingereza kuzitekeleza

Nini faida ya kujua kiingereza kwa ufasaha?

Kuna maraisi wa Uganda na Kenya wanakijua kiingereza vizuri sana, unaweza kunambia hizo nchi zinatofauti gani na tz hadi sasa?
mtu haishi kwa mkate peke yake
 
Siku hizi mpaka rais anasutana?
Mbona sioni mahali aliposutwa mtu.Tanzania hasa Dar hakuna Corona.Mnahangaika nini.Mimi nilijifukiza nikiwa std 2 sasa ni mtu mzima kuna cha kunifundisha hapo.HAKUNA CORONA TANZANIA.WOOOOTE TULALE MBELR
 
Hapa Jamii inakosea hata kama hamumpendi rais wa nchi, kwani kujua kingereza au kutokujua ni dhambi au kosa la jinai?? Tufanye ninyi mnajua Rais wetu yeye hajui, furahini sasa..
Acha nyeupe ibaki nyeupe na nyeusi kama ilivyo.Usichanganye.1+1=2
 
google.. do your h/w

Tatizo watanzania wengi Hamna Maturity na Mental Strength ndio maana mnajadili mambo ya Broken English. Exposure ni muhimu sana NINASISITIZA. WTZ wengi mnakosa hii kitu EXPOSURE ndio shida.

JPM ni President of our time. Watanzania jifunze kuwa na AKILI. Focus kwenye mambo ya Msingi.
 
Back
Top Bottom