Wanaoshinda kwenye computer/laptop na wanapata pesa huwa wanafanya kazi gani huko?

Wanaoshinda kwenye computer/laptop na wanapata pesa huwa wanafanya kazi gani huko?

Au wana daytrade crypto. Inawezekana ila ngumu sana, markets za crypto zipo volatile mno

Hii inawezekana ila kwa manati
Mimi nahisi hii unayoisema, ananunua coin labda kwa 2000 anaweza nunua hata za million 10, then anaziuza Kwa 2020, Kila coin Moja anaitafutia faida ya 20, Sasa anakua anashinda kwenye computer kuangalia soko linaendaje, kanambia soko ni uhakika maana watu was forex woote wananunua coin sijui.
 
Ingia google utapata mafundisho yote kuhsu jinsi ya kuingiza pesa kwenye mitandao.
Sisi tunachoma bando kutazama ngono TU wakati kuna program kibao za kupata pesa online mfano.
Kufundisha lugha,kuwasaidia watu kupata visa,vyuo,kazi,nk.
We poteza TU mda kutembeza bahasha ukiota kuokota ajira
 
Mtandaoni Kuna pesa nyingi sana ila ukisikia mtu anaishi kupitia mtandaoni mheshimu sana sio kazi ndogo sio sawa na kuchukua Michele mbeya na kuleta dar huku kunahitaji watu wenye elimu tu bila elimu mtandaoni utaishia kuchart
 
Vipi Ina Hela lakini? Nadhani ndio hii inaitwaje?
Screenshot_20240402-174623.png

Iko poa, sema niliingiza tamaaa 😋😋, mimi ndo nilikuwa natumia hii...
 
Mimi narudia kusema:-

IT Knowledge haihitaji vigezo vya kufaulu Maths na Physics, inahitaji PASSION na iwe ni Hobby au Interest ya Mtu basi ataperform kila kitu

Yaani ni kitu ambacho ukikipenda utakiweza tu

Kuna watu wamesoma Computer Science hapo UDSM ila Computer ikisumbua tu hata kuwaka (Booting problems) hawajui cha kufanya mpaka awatafute hao madogo wa mtaani
 
Mimi narudia kusema:-

IT Knowledge haihitaji vigezo vya kufaulu Maths na Physics, inahitaji PASSION na iwe ni Hobby au Interest ya Mtu basi ataperform kila kitu

Yaani ni kitu ambacho ukikipenda utakiweza tu

Kuna watu wamesoma Computer Science hapo UDSM ila Computer ikisumbua tu hata kuwaka (Booting problems) hawajui cha kufanya mpaka awatafute hao madogo wa mtaani
Vijana wengi wa IT wanaomaliza chuo ukimpa kazi ya kutengeneza App anakimbia
 
Kuna mtu nilimwambia biashara niliyoipata na inaniingizia hela nzuri sana kwa siku
Ila nilipofungua mdomo tu likawa kosa kubwa sana
Ingawa aliifanya lakini aliangukia pua
Najuta kusema tena ninafanya nini cha halali kinachoniingizia mlo wa siku
Pambana na hali yako mkuu ukifuatilia ya watu utasahau ya kwako na siku zinaenda
 
Hawahitaji kuwa na degree za ICT, hayo mambo hayahusiani na ict, ni kujua kutumia pc tu kawaida.

Tukiingia kwenye blogs, tukiangalia video youtube, tukitumia apps, huwa tunaona matangazo ya makampuni kama mitandao ya simu, makampuni ya vinywaji, n.k. hawa huwa wanapeleka matangazo yao google mfano tangazo likifika kwa kila watu elf 1 wanalipia kiasi kadhaa, Wao google wanaingia makualiano kuwalipa sehemu ya hio pesa wenye channel za youtube, blogs, apps, n.k. waonyeshe hayo matangazo.

blogger, wanaoweka videos youtube, wenye apps wanalipwa na google kwa kuwaruhusu hao google waonyeshe matangazo kwenye blog, video za youtube, apps ili wanaotembelea wayaone matangazo, mfano mwezi mzima watu milioni 1 wakiyaona matangazo wanalipwa takribani milioni 1 (inaweza kuzidi au kupungua kulingana na natangazo yanayoonekana na nchi wanazotokea watazamaji wa matangazo )

huyo crypto currency ananunua mfano bircoins nyingi kwa bei rahisi anauza kwa mafungu madogo madogo kwa bei ya juu
 
Back
Top Bottom