Wanaotajwa kumrithi Chongolo Ukatibu Mkuu CCM

Wanaotajwa kumrithi Chongolo Ukatibu Mkuu CCM

Wamo Mabalozi, Wastaafu, Mawaziri,Wakuu wa Mikoa na Vijana Chipukizi.

Kufuatia Katibu Mkuu Daniel Chongolo kuachia ngazi, wimbi la kupata Mrithi limezidi ongezeka Mtaani huko Dar es Salaam.

Makada wanaotajwa kwa ukaribu kurithi mikoba hiyo ni pamoja na aliyewahi kuwa wa Tanzania Nchini Misri
Balozi Emmanuel Nchimb, Mwenyekiti wa zamani wa Jumuiya ya Wazazi Alhaji Abdalah Bulembo, Mbunge wa Isimani William Lukuvi na Mwenezi Taifa Paul Makonda aidha Mawaziri wanaotajwa kwa kuvaa Mikoba hiyo ni Waziri wa Habari Nape Nnauye, Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile na Waziri wa Utumishi na Utawala Bora George Simbachawene. Pia wamo wakuu wa Mikoa wa Geita Juma Homela-Mbeya, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Amos Makala na Mkuu wa Mkoa wa Mara Said Mtanda.

Taarifa zinaonyesha kwamba Katibu Mkuu mpya anatarajiwa awe ni mbombezi kwenye Mipango na Mwenye haiba lakini mwenye umri wa ujana ili kuleta mvuto wa kundi kubwa la vijana wa Nchi hii ambao wanatajwa kufikia 75% ya watanzania.

Kadhalika Mtendaji mpya pia inatarajiwa awe Mtiifu asiye na mashaka kwa Mwenyekiti wa CCM Dkt Samia Suluhu Hasaan ambaye kama ilivyo desturi ya CCM anatazamiwa kuwa Mgombea pekee kwenye uchaguzi ujao wa 2025 ndani ya CCM.

Kwenye barua ya Kujiuzulu Katibu Mkuu Chongolo amehitimisha kwa kutoa tahadhari ya kumsihi Rais Samia awe makini dhidi ya watu wenye hila dhidi yake Rais, Chama na Taifa na akahitimisha kuendelea kuwa mtiifu kwa Chama siku zote, kauli hii imeibua minong'ono na imezidi toa mwanga pengine ndani ya Chama hicho wako Makada ambao wangekuwa hawana nia njema na Rais na Chama chao kwa mwaka 2025.
Wassira ? Hebu acheni masihara, toka enzi ya Nyerere yumo!

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Wamo Mabalozi, Wastaafu, Mawaziri, Wakuu wa Mikoa na Vijana Chipukizi.

Kufuatia Katibu Mkuu Daniel Chongolo kuachia ngazi, wimbi la kupata Mrithi limezidi kuongezeka Mtaani huko Dar es Salaam.

Makada wanaotajwa kwa ukaribu kurithi mikoba hiyo ni pamoja na aliyewahi kuwa Balozi wa Tanzania Nchini Misri, Balozi Emmanuel Nchimbi; Mwenyekiti wa zamani wa Jumuiya ya Wazazi, Alhaji Abdalah Bulembo; Mbunge wa Isimani, William Lukuvi na Mwenezi Taifa, Paul Makonda

Aidha, Mawaziri wanaotajwa kwa kuvaa Mikoba hiyo ni Waziri wa Habari, Nape Nnauye; Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile na Waziri wa Utumishi na Utawala Bora, George Simbachawene.

Pia, yumo Mkuu wa Mkoa wa Geita, Juma Homela-Mbeya; Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Amos Makala na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Said Mtanda.

Taarifa zinaonesha kwamba Katibu Mkuu mpya anatarajiwa awe ni mbombezi kwenye Mipango na Mwenye haiba lakini mwenye umri wa Ujana ili kuleta mvuto wa kundi kubwa la Vijana wa Nchi hii ambao wanatajwa kufikia 75% ya Watanzania.

Kadhalika Katibu huyo anatarajiwa awe Mtiifu asiye na mashaka kwa Mwenyekiti wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hasaan ambaye kama ilivyo desturi ya CCM anatazamiwa kuwa Mgombea pekee kwenye uchaguzi ujao wa 2025 ndani ya CCM.

Kwenye barua ya Kujiuzulu Katibu Mkuu, Chongolo amehitimisha kwa kutoa tahadhari ya kumsihi Rais Samia awe makini dhidi ya watu wenye hila dhidi yake Rais, Chama na Taifa na akahitimisha kuendelea kuwa mtiifu kwa Chama siku zote. Kauli hii imeibua minong'ono na imezidi kutoa mwanga pengine ndani ya Chama hicho wako Makada ambao wangekuwa hawana nia njema na Rais na Chama chao kwa mwaka 2025.

Soma Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo aandika barua ya kujiuzulu
Ningekuwa napendekeza majina ningewachukua Lukuvi, Simbachawene na Juma Homela. Mmoja kati ya hawa angefaa kuwa Katibu mkuu!
 
Back
Top Bottom