kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 18,154
- 17,491
Wakati wa kusajiri wachezaji umefika, ni sasa. Kama yupo mfadhili, kiongozi, mwanachama, shabiki, mchambuzi, mwamuzi, mchungaji, sheikh au mganga wa jadi anataka kuisadia timu yake kupata matokeo msimu ujao afanye hivyo sasa wakati dirisha la usajili liko wazi.
Changia fedha, mawazo, maoni, maombi, au kupiga ramli ili timu isajiri wachezaji bora kabisa badala ya kusubiri siku na wakati wa mechi kiwanjani, utakuwa umechelewa sana. Kuna watu wana tabia ya kuahidi kutoa fedha kwa wachezaji kama wataifunga timu fulani au kutwaa kombe, ni heri fedha hiyo waitoe sasa iingie kwenye usajiri. Kuna wachambuzi ambao wanasaidia kuzipa matumaini ya kijinga timu na wachezaji wao baada ya kusajiliwa, ni heri maoni na uchambuzi wao wautoe sasa ili timu zao zisajiri wachezaji bora.
Kuna wachungaji na masheikhe ambao wanaziombea timu zao kushinda mechi, ni heri maombi yao wayafanye sasa ili wachezaji wazuri wakubali kuja kucheza kwenye timu zao hata kwa dau dogo tu na walioko wasiondoke.
Waganga waroge sasa ili wachezaji mahiri wajikute wamekubali kuja kwenye timu zao kimazingahombwe hata bila fedha yoyote, na wale walioko wasiuone mlango wa kutokea hata kama wanatakiwa na timu za ulaya.
Wanachama lipieni sasa kadi zenu za uanachama ili timu zenu zipate fedha nyingi za kusajili na kubakiza wachezaji wazuri
mashabiki msiwe oyaoya tu kusubiri matokeo uwanjani na kwenye luninga, kuweni wanachama mchangie timu yenu ipate wachezaji wazuri na kuwabakiza waliopo.
Baada ya hapa kaeni kimya msubiri matokeo.