Kuelekea kikao cha Mkutano Mkuu wa CCm kuna propaganda zinaendelea zikisema Mzee Mpango anaumwa wakati huohuo zikidai KM CCM amejiuzulu
Hawa watu wa tweeter wapuuzwe, tufike wakati tubaki na verified information tu. Tunapokuwa na viongozi wa kisiasa wanaoandika na kupost kila kinachovumishwa kwenye mitandao kunawaondolea kuaminika kwenye jamii.
Kiongozi wa kisiasa jaribu kuchuja habari unayoweka kwenye mitandao ya kijamii. Nimtakie Mzee wetu Mpango maisha mema na afya tele zaidi kulitumikia Taifa. Nimtakie Mdogo wetu Chongolo uvumilivu kipindi hiki ambacho ameletewa watu wanaotaka aonekane kama hana hadhi ya kuwadhibiti kusema.
Natambua mtandao mbaya umerejesha kazini ila wakimtegemea Mungu watavuka salama. Waovu siku zote kwa Mungu ni chukizo. Waovu wakipewa madaraka madhara lazima yawepo hasa kwa watu wema na waadilifu......mimi personally nawaombea wale wote wenye uadilifu waweze kusimama dhidi ya kundi la waovu linalopigana usiku na mchana kurejesha ukatili kwenye siasa za nchi na ustawi wa watu wake.