kuna wale professsional wamesomea...wapo kwa ajili ya kuua tu serikalini, sasa imetokea miaka kadhaa marais wanajifanya hawataki kusaini wapate ruhusa ya kuwanyonga waliohukumiwa kifo....hawawanyongaji hawapati mahali kwa kutekeleza kazi zao......wanakuja nje huku wanadhani wameruhusiwa na rais kuteka raia.....raia akizingua kidogo au wamemhisi tofauti tu wanapita naye ilimradi tu watimize takwa lao la kutesa na kuua, na unashangaa watu rundo kupotea na kukutwa wameuliwa lakini mwenye nchi ana amani anafurahia....kule kutia saini tu anajinasibu yeye hapendi. Upande wa pili watu wa visasi na chuki binafsi na wivu nao wapo busy kuteka, kutesa na na kuua...wakibainika wakahukumiwa kunyongwa ..mkuu wa nchi anagoma kuweka saini kuruhusu watu wanyongwe.....alafu anajitapa hadharani kwamba mimi siwezi tia sahihi yangu mtu anyongwe...hapo unatarajia uuaji nchini utaisha ?, kwa njia ipi sasa?. Binadamu tuna safari ndefu sana..yaani huku unawindwa na nyoka, kule simba, huku mamba, kule mbwa, huku wachawi, kule binadamu wauaji, wezi, tandu, mara ukwepe ng'nge, ukwepe ajali, mara uumwe U.T.I....unajikuta unamtumainia Bwana na kubaki hai inakuwa ni Kristo kufa inabaki Faida tu...shida zinakuwa nyingi aisee😎