Wanaotetea Sakata la mkataba wa bandari hawana tofauti na waliokanusha kifo cha Rais enzi zile ilikuwa hivi hivi

Wanaotetea Sakata la mkataba wa bandari hawana tofauti na waliokanusha kifo cha Rais enzi zile ilikuwa hivi hivi

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
11,793
Reaction score
22,552
Wanaotetea Sakata la mkataba wa bandari hawana tofauti na waliokanusha kifo cha rais enzi zile ilikuwa hivi hivi!

Wengine walikwenda mbali zaidi wakidai wameongea nae kwa simu asubuhi kawaambia wachape kazi yuko mzima!

Watu walizidi kuhoji rais wetu yuko wapi walijibiwa yupo chato anawageni kutoka inje!

Ni ishara mbaya sana kuwa na viongozi waongo! Zamani kiongozi kudanganya hadharani ilikuwa ni aibu na fedheha,
Sasa hivi inataka kuonekana ni kawaida kuwa muongo muongo!

Madhara ya uongo huondoa imani kwa wananchi, kuna Leo na kesho serikali mathalani italeta jambo la kitaifa mfano; chanjo, itakuwa ni vigumu sana kuaminika kwamba ni chanjo salama!

Viongozi wakiwa waongo tunaunda jamii ya waongo inamaana hata watumishi wataiga uongo na huenda hata itapenya hadi kwenye familia na ndoa zitazidi kuvunjika kwa uongo uongo unaogeuzwa tabia!

Kesho Rais akitangaza kwamba mkataba wa bandari haujakaa sawa! Watu walewale watarudi kusema ni kweli hauko sawa!

Ifike mahala tuanzishe kampeni ya kukataa kuongozwa na wahuni wahuni!
Eti tumefikia hatua Hoja za mkataba wa bandari ufafanuzi unatolewa na DP world! Kwamba tusiwe na wasiwasi!

Cha ajabu kuliko vyote!
Wanasheria nguli wanachambua vipengere vya mkataba lakini wanaotakiwa kutoa majibu wanaeleza kwa hisia!

Kwanini hisia waliyo nayo isiwe hasi na chanya?
Wale wale waliokanusha kifo cha Rais mpendwa ndiyo wale wale wanaokanusha kwamba mkataba siyo mbovu
 
Kula chuma hii

 
Wote wanamaslai binafsi,usiumie kichwa kuhusu wao et wamewapeleka cjui zembwera cjui nani yule kifupi nyundo nyerere
 
Kuna baadhi waliposema Magu ni mgonjwa, au amekufa walikamatwa, ambapo ilikuwa ni kweli.
Lakini waliodanganya kwamba ni mzima, na anachapa kazi sana ndiyo walionekana ni wazalendo!
 
Dmkali mtu wangu tuacheni tupumzike jamani. Kama una uwezo wa kula mara moja kwa siku na ngono unapata kwa nini usumbuke kupoteza energy and time?
 
Kuna baadhi waliposema Magu ni mgonjwa, au amekufa walikamatwa, ambapo ilikuwa ni kweli.
Lakini waliodanganya kwamba ni mzima, na anachapa kazi sana ndiyo walionekana ni wazalendo!
Tunaongozwa na waongo wengi kuliko wakweli
 
Machoni kama wanasema ukweli lakini historia yao mambo mengi sana walitudanganya kwa style hii hii ya kuwaamin
 
Back
Top Bottom