Mi nadhani pia nchi zetu za Kiafrika pia zinachangia sana kuwafifisha wataalamu wetu
Wee fikiria nchi kama DRC au Burundi au Sudan zimejaa migogoro ya kivita na kisiasa alafu unawaambia Wanasayansi wabaki pale wafanye nini cha maana?! Hata raia tu wakawaida wanakimbia nchi kuokoa maisha yao Sembuse Wanasayansi wabaki?!
Mataifa mengi ya Kiafrika yamejaa siasa za ufisadi, na Siasa za ukabila badala ya kujali maendeleo, wanasiasa wanalipwa zaidi hela nyingi kuliko hata Wanasayansi,, unakuta mbunge ni darasa la saba analipwa hela nyingi kuliko mhadhiri au profesa wa chuo kikuu alafu bado unawaambia Wanasayansi wetu wabaki Afrika?! Huoni Hata maprofessa wanakimbilia kwenye siasa kuliko kubaki kwenye taaluma zao?! Sio kwamba hawana uzalendo bali serikali zetu zimesababisha hayo yote badala ya kujali taaluma za Wanasayansi wetu wao wanajali sana siasa kuliko sayansi,, inauma sana
Pia hawaweki mkazo katika ugunduzi na ubunifu wa kisayansi,, hivi ni bajeti kiasi gani inawekwa kwenye ugunduzi Na Utafiti wa kisayansi?! Sasa hata mwanasayansi mfano wa spacecraft akibaki hapa nchini atafanya utafiti au ugunduzi wa kitu gani kama hakuna bajeti au fund ya utafiti wa kitu hicho?!
Bora waende tu kwenye mataifa hayo yanayo wajali Wanasayansi na kutenga fedha kwaajili ya utafiti ili kuendeleza ugunduzi wao kuliko kubakia Wakiwa marecturers hapa bongo mpaka kifo chao,,,