Wanasayansi wa kiafrika ndio wanaoikuza Amerika na Ulaya, kwanini wasiikuze Afrika yao?

Wanasayansi wa kiafrika ndio wanaoikuza Amerika na Ulaya, kwanini wasiikuze Afrika yao?

Nimekuelewa wataalamu kwenye uzi wako wapo from hizo nchi.

Lakini ninahitaji kujua exact number ya wataalamu mashuhuri kutoka kusini mwa jangwa la sahara.
ni wengi mno hao nimetaja wale waliotikisa dunia tu yaani kuna ambao bado wanasoma huko kwa wenzetu na hawana mategemeo ya kurudi na wengine ndio wanafanya kazi za kawaida kwenye mataifa yaliyoendelea ila bado hawajagundua vitu

hivi unafikiri kwanini sasa matangazo ya scholarship kwa waafrika yamekuja mengi?
 
ndo hvyo mkuu kikubwa tusiache kupambana kwakuwa hii hali tunayopitia hata wao walipitia pia enzi zao,tusione aibu kukazania elimu kilimo na viwanda vdg vdg huko kwngne tufnye taratibu
ndio hivyo ila inabidi ili tujitoe kwenye haya matatizo nchi nyingi za africa ziungane ili kuwa na nguvu kama walivyofanya USA kwahiyo kama tz inaonekana jimbo tu bila hivyo bado tutakuwa tunazingirwa na makamasi
 
Hahahahaa hahahahaa
Bora sijatajwa
Lakini kuna Uzi niliwahi ongea kitu kuwa Y? Wasomi wengi wa Africa hawatumikii Nchi zao!.

Kubwa zaidi mfumo mbovu Na sera mbovu za elimu pamoja Na kujuana sanaaa!.

Mf: Mimi nilisoma aerospace engineering
Unadhani kwa huko bongo ningefanyaje nini???????

Pia unakuta mtu una hustle kutoboa halafu uje kuganga Na mshahara wa TGS C?!!!!
.
Waafrika wanaojitambua wapo njeee!
Ukibaki Africa ni kupoteza Muda tu!.
Mleta maada wapo wa TANZANIA wengi NASA lakini wamebadili kila kitu Na hawataki hata kusikia jina TANZANIA!.
 
ndio hivyo ila inabidi ili tujitoe kwenye haya matatizo nchi nyingi za africa ziungane ili kuwa na nguvu kama walivyofanya USA kwahiyo kama tz inaonekana jimbo tu bila hivyo bado tutakuwa tunazingirwa na makamasi
ah ndo hvyo mkuu kama hatujitahidi tutaendelea kuwa watumwa tu sema tunabadilisha tu bwana sasa hivi bwana yetu mchina
 
Wangeuawa zamani tu,tena kama huyo mwenye celtel angeshapigwa risasi.
Hata mack aliyegundua facebook asingefika popote na fb yake wala whatsapp,angepigwa risasi na yeye.
Nata mimi nikiwa scientist sifanyi ujinga huo wa kukaa humu tena hususani Tanzania.
Huyo mrusho satellite angeambiwa aishushe haraka sana la sivyo atapigwa kipigo cha mbwa koko.
 
Hahahahaa hahahahaa
Bora sijatajwa
Lakini kuna Uzi niliwahi ongea kitu kuwa Y? Wasomi wengi wa Africa hawatumikii Nchi zao!.

Kubwa zaidi mfumo mbovu Na sera mbovu za elimu pamoja Na kujuana sanaaa!.

Mf: Mimi nilisoma aerospace engineering
Unadhani kwa huko bongo ningefanyaje nini???????

Pia unakuta mtu una hustle kutoboa halafu uje kuganga Na mshahara wa TGS C?!!!!
.
Waafrika wanaojitambua wapo njeee!
Ukibaki Africa ni kupoteza Muda tu!.
Mleta maada wapo wa TANZANIA wengi NASA lakini wamebadili kila kitu Na hawataki hata kusikia jina TANZANIA!.
Mkuu kweli haki ya mungu wallah huu mwezi mtukufu wagunduzi wa instagram,facebook na whatsapp wangekua wanatokea Tanzania wangeshaambiwa wafunge mitandao means hata dunia isingenufaika navyo wala wasingekuwa hata billionares kama zuckerberg.
 
Mkuu kweli haki ya mungu wallah huu mwezi mtukufu wagunduzi wa instagram,facebook na whatsapp wangekua wanatokea Tanzania wangeshaambiwa wafunge mitandao means hata dunia isingenufaika navyo wala wasingekuwa hata billionares kama zuckerberg.
Upo sahihi kiongozi!.
Africa ni laana Na kupotezeana ndoto+bahati Na nyota!.

Kwanza wamekalia uchawi mwingi!.Na imani haba

Kuja siku nilienda kijijini Na Mzungu daaah
Aseeee walisema nitawaleta mikosi
Tena wakafika mbali zaidi Na kusema ety
Nimekuwa Freemason!..

Kisa niliosomaga nao primary wapo kijijini wamechoka me naonekana Bado kijana Na napesa
Nilichoka hoi
 
TANZANIA
1. Felix A. Chami
Felix A. Chami is an archaeologist from Tanzania. He is a professor at Dar es Salaam University. Dr. Chami discovered, on the island of Mafia and Juani, artefacts that revealed East Africa as being integral to the Indian Ocean trade huyu yupo africa na anafanya kazi africa alichogundua imebidi nikiweke kwenye lugha ya fumbo ili mjiulize kwanini kabaki africa

Sasa mbona huyu kabaki Afrika na bado hakuna maendeleo?
 
HII NI LIST YA WANASAYANSI KUTOKA AFRICA NA KAZI WANAZOZIFANYA KWENYE MATAIFA MAKUBWA

EGYPT
1. Euclid of Alexandria
huyu ni founder wa geometry ni mzaliwa wa egypt
amefanya kazi katika European Space Agency's (ESA) na ameunda euclid space craft
220px-Euklid-von-Alexandria_1.jpg


2. Sameera Moussa
huyu ni ni mwanafizikia aliyebobea kwenye maswala ya nyukilia na ni mzawa wa egypty ana doctorate ya atomic radiation na alifia huko California, united state
220px-SameeraMoussa.jpg


3.Ahmed Hassan Zewail
Huyu ni wa Egypt ni mwanzilishi wa femtochemistry anafanya kazi amerca
185px-Ahmed_Zewail_HD2009_Othmer_Gold_Medal_portrait.JPG


Eritrean
1. Haile Debas
huyu ni mfanya sugery, mwanafizikia na ni academic adminstrator katika chuo kikuu cha California ni mzawa wa africa

Carthage
1. Abbas Ibn Firnas
huyu ni mwanafizikia mchemia na engineer alifanya kazi huko spain ila ni mzawa wa carthage africa

Morocco
1. Rachid Yazami
huyi ni morocan alifanya research kuhusu lithium battery na graphite anode anafanya kazi katika French National Centre for Scientific Research (CNRS) ni wa kwaza kugundua intercalation ya lithium kwenye graphite katika electrochemical cell
220px-Rachid_Yazami_2011.JPG

Ethiopean

1. Sossina M. Haile

huyu ni profesa na mchemia pia ni mwanafizika na ni mhandisi anafanya kazi california instute of technology huyu aligundua solid acid fuel cells

2. Kitaw Ejigu
Ethiopian engineer and Chief of Spacecraft and Satellite Systems engineer at NASA.
KENYAN
1. Calestous Juma
Huyu ni professor pia ni mfanya kazi katika havard university ni mzawa wa kenya

MALI
1. Cheick Modibo Diarra
Huyu ni aerospace engineer amechangia kukamilika kwa mission nyingi za NASA mfano kupatikana kwa njia ya kwenda kwenye sayari ya mars , galileo space craft na kuchunguza sayari ya mars
NIGERIAN
1. John Uzo Ogbu
huyu ni professor alikuwa anachunguza maswala ya intelligence kuendana na rangi ya ngozi (race) inasemekana alikuwa na IQ kubwa ni mzawa wa nigeria lakini alikuwa anafundisha na kuishi California

2. Bisi Ezerioha

huyu ni professor, engeneer huyu ndie mgunduzi na mtengenezaji wa honda pia ameshiriki katika utengenezaji wa Hyundai Motor America mhshimiwa huyu pia anatengeneza injini za magari pia
220px-Bisi_before_a_race-_2013-09-24_11-08.jpg


SOUTH AFRICA

1. Aaron Klug
Huyu ni mchemia na biophycist alijishindia tuzo kwa kugundua crystallographic electron microscopy pia amegundua structure ya tobacco mosaic virus huyu ni director wa maabara ya molecular biology huko cambridge

2. Sydney Brenner
huyu amebobea kwenye genetic alipata tuzo noble prize kwenye phsiology or medicine anafanya kazi kwenye maabara ya molecular biology huko cambridge england pia ni mwanzilishi na mmiliki wa California instute of molecular bilology kwa kipindi cha maisha yake

3. Christiaan Barnard
huyu ni mpasuaji bingwa wa moyo pia alifanikiwa kuhamisha moyo kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa mara ya kwanza duniani hajareportiwa sehemu aliyokuwa anafanyakazi nnje ya africa lakini alionekana kuondoka sana africa na alikufa mwaka 2001

SUDANI
1. Mohammed Ibrahim
Huyu engineer na ni billionaire pia aliwahi kuishi british na kufanya kazi huko katika vitengo vya telecomunication aliajiriwa na british telecom huyu ni mwanzilishi wa mtandao wa celtel
220px-Mo_Ibrahim.jpg


2. Ali M. El-Agraa
huyu ni mwanauchumi bingwa amefanya kazi british, usa, na japan nchi ambazo sasa zinaonekana kukua kiuchumi mno

200px-Editing_Ali_M._El-Agraa.JPG


3. Mohamed Osman Baloola
huyu ni biomedical engineer pia ni mtafiti na mwendesha research kuhusu diabetes anafanya kazi uarabuni katika Ajman University of Science and Technology

220px-Mohamed_Osman_baloola.jpg

TANZANIA
1. Felix A. Chami
Felix A. Chami is an archaeologist from Tanzania. He is a professor at Dar es Salaam University. Dr. Chami discovered, on the island of Mafia and Juani, artefacts that revealed East Africa as being integral to the Indian Ocean trade huyu yupo africa na anafanya kazi africa alichogundua imebidi nikiweke kwenye lugha ya fumbo ili mjiulize kwanini kabaki africa
220px-Professor_Felix_Chami.jpg

UGANDA
1. Kwatsi Alibaruho
Huyu ni director wa kurusha vifaa vya anga anafanya kazi National Aeronautics and Space Administration (NASA) alishadirect human spaceflight mwaka 2005 pia anahusika kumanage na kucarry space shuttle flight
220px-Kwatsi_Alibaruho_-_flight_director.jpg

AFRICA TUNA LIST YA WANASAYANSI WENGI AMBA O NI WAZAWA WA AFRICA LAKINI SASA WANAYATUMIKIA MATAIFA MAKUBWA BADALA YA TAIFA LAO PIA WENGINE WANAONEKANA KUTAFUTA URAIA KWENYE MATAIFA HAYO

1. Je hii ni akili na wanasababu mdhubuti kufanya hivyo? je kuna watu wa mataifa makubwa kama amerca wanakuja kulitumikia tafa dogo africa?

2. Je tukisema waafrica wanatamaa ya pesa na si wazalendo wa nchi zao tunakosea? unafikiri hawa wanasayansi wangefanya kazi kwenye mabara yao africa tungekuwa bado maskini?

3. Je unafikiri hawa wanasayansi wangefanya kazi africa kungekuwa na mgogoro mkubwa na mataifa makubwa na huenda wangefanikiwa kuwaua?

4. je wanasayansi wa africa wanalazimishwa kufanya kazi kwenye mataifa makubwa na kutishiwa kuuliwa hivyo wanaogopa kufa



ILA NIMEGUNDUA WANASAYANSI WENGI WA KIAFRICA WANAOJULIKANA DUNIA NA NI WAZAWA WA SOUTH AFRICA BADO WANAFANYA KAZI SOUTH AFRICA JAPO SIJAWAWEKA KWENYE LIST HAPO

UMEGUNDUA NINI? africa tunajiona tuna wanasayansi wengi lakini wanaofahamika ulimwenguni pote ni wachache mfano kwa tanzania anafahamika mmoja kwani tunamaporofesa wangapi kwenye vyuo vyetu je wametendewa haki kutotajwa kwenye hii list?


nawasilisha
Jibu ni rahisi, hakuna haja ya kusema wana tamaa ya pesa ama c.yo wazalendo. Ni kwa sbb hakuna nchi za kiafrika zilizojikita seriously kwenye uendelezaji wa sayansi na teknolojia ama hata R&D.
 
Africa inateswa na siasa mbovu. Kutothamini ujuzi wa mtu siasa mbele. Ndio maana mpk sasa makonda asie na kitu kichwani ni mkuu wa mkoa na anatukana mainjiania na wenye akili, ukae Afrika ufanye nini?

Naonaga vijana wanatengeneza wanavumbua vitu kwenye magereji na mitaani huko nani anawapa sapoti? Zipo wapi karakana za taifa kukuza vipaji?

Mtu akitengeneza kitu badala apewe karakana na uwanja wa majaribio utasikia hairuhusiwi iko kitu maana hakijathibitishwa. Nyumbu nyumbu tu Africa haitaendelea. Kuna tatizo.

Sasa kwa akili za kiongozi wa malaika unategemea ipo siku Afrika itatoka
 
Nchi nyingi za kiafrika wanasiasa ndio tatizo letu. Wanasiasa ni zigo kubwa sana tunalolipia gharama zao za juu za maisha kuliko kundi lolote. Hivi kweli kwa mfano tu Profesa maji marefu analipwa zaidi kuliko daktari bingwa pale muhimbili!!! inaingia akilini mheshimiwa msukuma na mwenzie Sugu wanalipwa zaidi kuliko engineer fulani?
 
Sasa huko Bongo tunazibiwa na kuongozwa na Bashite.

Kwa nini tusisepe tu?
 
Jibu mbona Dogo sana ,angalia mshahara wa mbunge na wa Mwalimu,hapo ndio utapata jibu.

Nchi za afrika husani Tanzania haiungi mkono profession Bali inaunga mkono politics.
 
Africa hatuna kipaumbele cha kukuza taaluma au kua support wana-Sayansi kwenye gunduzi au tafiti zao...

Africa tunakazania zaidi, vibali au uhalali wa kufanya hicho ulichovumbua au unachotakakuvumbua, mengine utajijua mwenyewe...

Africa tunakazania zaidi, unataka kuvumbua au kufanya tafiti fulani wewe kama nani? Na je umepitia Msingi, secondary na chuo? Je vyeti vyote unavyo... mengine utajijua mwenyewe... na je hicho unachotaka kuvumbua au kukifanyia tafiti kuna chochote kitu watapata?

Ndiyo maana wana-Sayansi wengi kutoka Africa wanakimbilia Ulaya...


Cc: mahondaw
 
hakika umetoa point kubwa hata mimi nakubaliana na wewe ni kitu cha kushangaza sana kama profesa kabisa anakitolea kufanya kazi lakini anazalilishwa kwenye nchi maskini wakati mwanzo alikuwa anaheshimika kwenye mataifa yaliyoendelea hakika tanzania inabidi kubadlilika
NAcho sikitika zaidi prof amekufa KIFO ambacho nahisi alikufa huku anajilaumu why alirudi home, is very sad.
 
kwani wangebaki kwenye nchi zao wakayafanya hayo waliyoenda kufanya kwenye mataifa makubwa si ipo siku kazi za mikono yao zingewalipa au tuseme wana tamaa ya pesa?
Africa hakuna masilahi halafu kitu kingine kuna sheria za ovyo sana Africa na hakuna support.
Mfano mzuri. Ni yule jamaa aliyetengeneza helcopter. Unamsikia kwa sasa?
Hata ningekuwa mimi siwezi kubaki Africa hata wangenipa nini. Mshahara wa mzoa taka USA unamzidi meneja wa bank. Hapana aiseeee
 
Africa hatuna kipaumbele cha kukuza taaluma au kua support wana-Sayansi kwenye gunduzi au tafiti zao...

Africa tunakazania zaidi, vibali au uhalali wa kufanya hicho ulichovumbua au unachotakakuvumbua, mengine utajijua mwenyewe...

Africa tunakazania zaidi, unataka kuvumbua au kufanya tafiti fulani wewe kama nani? Na je umepitia Msingi, secondary na chuo? Je vyeti vyote unavyo... mengine utajijua mwenyewe... na je hicho unachotaka kuvumbua au kukifanyia tafiti kuna chochote kitu watapata?

Ndiyo maana wana-Sayansi wengi kutoka Africa wanakimbilia Ulaya...


Cc: mahondaw
Africa inayolipa ni siasa tu. Mambo ya taaluma unajitafutia umasikini. Siku hizi tunaangalia masilahi
 
Nani aliyekuambia wanasayansi wa kiafrika ndo walioikuza ulaya na marekani?

Hao waafrika wamekwenda huko washakuta ulaya na marekani zimeendelea
 
Back
Top Bottom