Wanasayansi wa kiafrika ndio wanaoikuza Amerika na Ulaya, kwanini wasiikuze Afrika yao?

Wanasayansi wa kiafrika ndio wanaoikuza Amerika na Ulaya, kwanini wasiikuze Afrika yao?

nchi kama marekani ilitumia takribani miaka 80's mpaka nayo inajitambua na kujiona imeendelea na hawakutaka kupiga propaganda nyingi kwenye sekta ya maendeleo ya viwanda na kama wao wangehesabia cherehani ni kiwanda wangekuwa wapi leo hizi cherehani tunazoziona ni kiwanda hapa nchini utakuta ni kitu kilichotumiwa miaka hata 50 iliyopita eti sisi leo tunashtuka na kukumbuka nacho ni kiwanda aibu sanaa tena mnoo
Mkuu cherehani zimeanza huko Uingereza mwaka 1790, leo hii hapa bongo ndo kiwanda. wenzetu wako kwenye nanotechnology bado sisi tunalima kwa jembe la mkono huku tukisugua magoti kumuomba mleta mvua atusaidie.
 
Tunaweza kusema hawana tamaa ya pesa na utakuta asilimia kubwa ya hao hapo hawajasoma nchini kwao,sasa kama mtu amesoma mambo ya anga na kurusha space objects huko juu na ni mzaliwa wa Uganda je lini uganda itaweza kugharamia utengenezwaji hata wa satellite yake yenyewe au kuweza kufanya utafiti wa anga na kuleta takwimu nchini kwao kikubwa ni kwamba waafrica tunapewa nafasi ya kwenda kusoma nchi zilizoendelea vitu ambavyo ni vikubwa na vinatakiwa maandalizi mazuri yakifedha na miundombinu lakini nchi zetu hazitaki kuwekeza kwenye hayo mambo ambayo sisi tunayasoma sasa utakuta mtu kama huyo au hao hawawezi kurudi nchi zao kinachotokea anachukuliwa na nchi zilizojipanga na asilimia kubwa huwa wanajitahidi pindi wanapopata hizo nafasi.

Kwahio tujipange tuu ili wasomi pindi wanapomaliza wawe na uhakika na mtu unakuta anashauku kweli ya kuisaidia nchi yake sema ndo hivyo hatuna hiyo miradi wala fedha za kuwekeza
Well said mkuu,
Kwa kuongezea tu ni kwamba, mtu kama alikuwa interested kusomea kitu flan maana yake anategemea katika maisha yake afanye kazi zinazoendana na taaluma yake, hapo ndio utauona utam wa elim. Sasa chukulia mfanò huyu kiongozi wetu wa visiwani (naskia taaluma yake ni mambo ya nyuklia) assume angekuwa sio kiongozi mkubwa wa nchi ambaye anapata pesa na maisha mazuri, maana yake ingekuwa ni rahisi sana kwake kushawishiwa kwenda nje ya nchi ambako may be wangemuhitaji.
Kuna vijana wenzangu wamesomea petroleum na wamehitim vzr kwa pesa za mikopo ya watanzania lkn cha kushangaza hakuna kazi mtaan. Swali ni; hivi wakienda nje ya nchi na kupewa kila wanachohitaji na wakapiga kazi vzr, ni nani wa kumlaum?
 
ila kwa mfano aliyetengenezaga lile gari kwa kipindi kile hata angepewa support bado asingeweza kuliingizia taifa kipato kikubwa kwakuwa hata yangetengenezwa hayo magari yasingeweza kuuzwa nje ya tanzania pili yasingeweza kupambana sokoni na magari yanayingizwa nchini kutokana na ubora wake. je uanafikiri kungekuwa na uwezo wowote wa kuzuia magari kutoka mataifa makubwa yazuiliwe kuuzwa tanzania ili magari yatakayotengenezwa hapa yapate soko?

kikubwa mtu ili apewe support na kuliletea faida taifa anapaswa kuvumbua kitu ambacho hakijawahi kugunduliwa duniani hapo ndipo technologia ya huyo mtu itakuwa na manufaa na kuuzika kwa bei kubwa.
Kumuendeleza nikumpa uwezo. Awe expert maana yake waweza mpeleka kusoma badae kuongeza ujuzi. Ukiwa nao 10 ukashawishi makampuni yenye majina kuja kuwekeza assembling industries nchini expert wanakuwa wazawa. Kuanzia hapo wanaweza kubuni vitu.

Ili kuja na kipya lazima uwe na theories za wengine kwanza na ujuzi wa wengine. Najiuliza tu sisi tuna robotics engeneers wangapi? Robotics electrician wangapi? Lazima uwe na hawa watu kwanza ili waingie laboratory kubuni. Na sio uokote tu mitaani wanaosoma ili wapate kazi. Unachukua wenye passion na feel ya kitu husika.

Tanzania tuna ITs walienda kusoma tu pale UCC ili wapate kazi ila mtu hana hata exposure kwa hiyo computer anaiona siku ya kwanza anapoingia chuo akiambiwa touch a mouse anashika mdomo.

Lakin kuna watu hawajaenda chuo anatumia uwezo binafsi anacheza na computer huyu ukimpa na formal knowledge bila shaka anakuwa mbaya vibaya.

So si lazima tupate tecnolojia ya kuuza tu mpya, china wenzao wanavumbua wao wanakopi na wanauza..ha ha ha
 
hilo ni tatizo kubwa
hivi kuna kipindi mulishafikiria au ulishajaribu kutafuta njia ya kulisaidia taifa lako hata kimawazo tu?
Mkuu mbona unanichimba sana?!
Nifikirie bongo kwa mambo haya yanayotendeka?!

Viongozi wa huko,wengi wanaamini katika vitu Na wala siyo maendeleo ya watu!

Nilishangaa kusikia Kiongozi akisema kuwa maendeleo ni kuwa na ndege wakat huo kuna uhaba wa walimu Na shule
 
sasa kama unatafuta pesa kwenye taifa lenye kipato kidogo badala ya kuliendeleza lli liwe na kipato kikubwa nawe upate pesa badala yake unakimbia sasa hapo utakuwa huna uzalendo hata kidogo na taifa lako

unafikiri mataifa yaliyoendelea sasa hakuna wanasayansi na wataalamu waliojitolea zamani na kulitumikia taifa bila kulipwa pesa kubwa mpaka taifa likapata mwanga
Tupo kwenye stage ya capitalism. Huo uzalendo upo kwenye communalism kwahiyo stage iliyopita. Unakuwa mzalendo halafu unakufa masikini wakati hivyo vitu unavyo ukienda ng'ambo unakuwa tajiri baada ya mwezi. Sasa hivi tunaangalia pesa nzuri iko wapi. Huo uzalendo baki nao tu kwasbb hauna faida kwenye njaa na ukiangalia kwenye suala la teknolojia nchi za kiafrika bado sana. Unakuwa na vitu vyingi halafu unaishi maisha km ya kondakta wa daladala. Yote ya nini. Mm siwezi aisee.
 
Well said mkuu,
Kwa kuongezea tu ni kwamba, mtu kama alikuwa interested kusomea kitu flan maana yake anategemea katika maisha yake afanye kazi zinazoendana na taaluma yake, hapo ndio utauona utam wa elim. Sasa chukulia mfanò huyu kiongozi wetu wa visiwani (naskia taaluma yake ni mambo ya nyuklia) assume angekuwa sio kiongozi mkubwa wa nchi ambaye anapata pesa na maisha mazuri, maana yake ingekuwa ni rahisi sana kwake kushawishiwa kwenda nje ya nchi ambako may be wangemuhitaji.
Kuna vijana wenzangu wamesomea petroleum na wamehitim vzr kwa pesa za mikopo ya watanzania lkn cha kushangaza hakuna kazi mtaan. Swali ni; hivi wakienda nje ya nchi na kupewa kila wanachohitaji na wakapiga kazi vzr, ni nani wa kumlaum?
shukrani mkuu
matabibu wapo tunapambanaa sotee
emoji23.png
emoji23.png
 
Mkuu cherehani zimeanza huko Uingereza mwaka 1790, leo hii hapa bongo ndo kiwanda. wenzetu wako kwenye nanotechnology bado sisi tunalima kwa jembe la mkono huku tukisugua magoti kumuomba mleta mvua atusaidie.
haahahaha aisee kumbe ni muda kweli haya sasa huku ndo viwanda mimi bado namtafakari alietoa hiyo kauli na yupo tuu kakaa nae anajiita mjenga taifa au kiongozi naona ni akili ndogo tuu samahani kwa kutumia hili neno ila inabidi tuu kwa mudaa litumike
 
Pia mazingira hayatatoa fursa kwa wao kuutumia ujuzi na uzoefu wao, sana sana wataishia kuwa frustrated. Hii Afrika waachiwe wanasiasa.
waachie hiyo afrika kwa nini sasa wanatakiwa wajue kinachotakiwa kifanyike
 
Kumuendeleza nikumpa uwezo. Awe expert maana yake waweza mpeleka kusoma badae kuongeza ujuzi. Ukiwa nao 10 ukashawishi makampuni yenye majina kuja kuwekeza assembling industries nchini expert wanakuwa wazawa. Kuanzia hapo wanaweza kubuni vitu.
sasa kama atakayegundua kitu akiwa hajasoma hata college/university au hana hata secondary education utamwendeleza vipi au hata akipata sponsor kwenda kusoma nje ataenda kupata elimu ya ngazi ipi either higher education au diploma etc?
huoni hilo ni tatizo
 
Tupo kwenye stage ya capitalism. Huo uzalendo upo kwenye communalism kwahiyo stage iliyopita. Unakuwa mzalendo halafu unakufa masikini wakati hivyo vitu unavyo ukienda ng'ambo unakuwa tajiri baada ya mwezi. Sasa hivi tunaangalia pesa nzuri iko wapi. Huo uzalendo baki nao tu kwasbb hauna faida kwenye njaa na ukiangalia kwenye suala la teknolojia nchi za kiafrika bado sana. Unakuwa na vitu vyingi halafu unaishi maisha km ya kondakta wa daladala. Yote ya nini. Mm siwezi aisee.
umeeleweka kiongozi ila hiyo capitalism tuliyopo haina sifa ya capitalism ile ya zama zile sababu huku ni vibanda na si viwanda kama capitalist wa zamani walivyofanya
 
waachie hiyo afrika kwa nini sasa wanatakiwa wajue kinachotakiwa kifanyike
Mkuu hawa wanasiasa wana exposure kubwa tu ya hii dunia, wamesoma na kusafiri sana nchi za wenzetu. Wanajua kinachotakiwa kufanyika ili tusonge mbele. Ila ubinafsi, tamaa, uchoyo, ulafi n.k vimewapofusha na kuamua kutokuona. Hata leo nchi hii tunao wasomi wazuri sana, ila kila kitu wanaamua wanasiasa tena wengine elimu ya kawaida sana, so wasomi makini wameamua kutulia na kufanya yao.
 
Je, TANTRADE wanalo gazeti la BUSINESS JOURNAL au COSTEC wana SCIENTIST JOURNAL? Ama wanavyo au hawana, wanatujuza vipi maendeleo ya wanasayansi wetu au wanabiashara / wanaviwanda wetu?
 
Je, TANTRADE wanalo gazeti la BUSINESS JOURNAL au COSTEC wana SCIENTIST JOURNAL? Ama wanavyo au hawana, wanatujuza vipi maendeleo ya wanasayansi wetu au wanabiashara / wanaviwanda wetu?
 
Tunae aliefanyia kazi kwenye maganda ya korosho hadi kazamia huko na ni mtanzania hajatoka nje ya Tanzania na hataki hata kutoka nje ya TZ mbona yeye humpi credit yake?
 
Back
Top Bottom