Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 1,679
- 2,123
Mfumo mpya wa kinga ya mwili umegunduliwa. Upo katika sehemu ya mwili inayojulikana kwa kusaga protini. Mfumo huo una muundo wa siri unaoweza kutapika kemikali zinazoua bakteria.
Watafiti kutoka Israel wanasema ugunduzi huu utabadilisha uelewa wetu wa jinsi mwili unavyolindwa dhidi ya maambukizi. Utafiti huu unatoa nafasi mpya ya kutafuta dawa mpya za antibiotiki ili kukabiliana na tatizo linaloongezeka la wadudu ambao ni sugu kwa dawa zetu za sasa.
Mfumo huu upo katika proteasome – eneo dogo ambalo lipo katika kila seli ya mwili. Kazi yake kuu ni kukata protini kongwe na kuzifanya vipande vidogo ili ziweze kuchakatwa na kutengenezwa kuwa protini mpya.
Source: BBC News
Ugunduzi huu unazidi kuthibitisha unabii wa Danieli kuwa siku za mwisho maarifa yataongezeka.
"Lakini wewe, Danieli, yafunge maneno haya, ukatie muhuri kitabu hata wakati wa mwisho; wengi wataenda mbio huko na huko, na maarifa yataongezeka." (Danieli 12:4)
Israeli imebarikiwa katika maeneo mengi ya kiuchumi, kiteknolojia na kiafya kama Mungu alivyoahidi:
"Nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka; Nami nitawabariki wakubarikio, na yeye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa."( Mwanzo 12:2-3).