Ni wapi na ulipo ushahidi wa kuthibitisha madai ya wizi wa kura uliofanywa na
magufuli ?
Unapoandika uzi kwenye jukwaa hili hasa kuwahusu viongozi hao wa kitaifa ni vema unatuwekea ushahidi na sio dhana fikirika.
Halafu unapaswa kujiuliza swali moja.
Chadema walidai kukamata begi la Kura feki walizodai ilikuwa zitumbukizwe kwenye kasha la kura!
Lakini Chadema hao hao ndio waliochoma hilo begi badala ya kulitunza na kura hizo ili ziwe kidhibiti muhimu sana baada ya uchaguzi.
Wewe uliona wapi mtu kuchoma ushahidi muhimu ambao ungeisaidia Dunia kuujua ukweli?.
Magufuli alikuwa ndani ya mioyo ya wananchi kutokana na alivyokuwa akisimamia mambo na kuhakikisha yanatendeka ipasavyo na kwa wakati.
Kama binadamu alikuwa na mapungufu yake pia.
Lakini hayakuweza kufunika yale mengi mazuri aliyokuwa ameyaasisi.
Vema mumuache alikotangulia kwenye haki ya kweli na nyinyi mliobaki hai bado.
Mngejikita kupambana na yaliyo mbele yenu kuliko kila kukicha mnapambana na mtu aliyekwisha lala milele.
Hii pia ni uthibitisho kwamba Magufuli alikuwa anakubalika na bado anawanyima usingizi mlio hai,kwa kivuli chake tu.
View attachment 2240240