Wanasema simjali mama yangu ila kiukweli sioni athari yake kwangu

Kama mama yako aliondoka na bado mzee wako kamtimua mwanamke mwingine . Jua Maza ako hakuondoka kwa kupenda hivyo mjali. Mwanamke nikiumbe mvumilivu kwasababu Ni mnyonge . Ukiona angeondoka ujue Kuna sababu kubwa
 
Kwanza ni mama Yako by any means unatakiwa Kumjali Kwa utakachojaliwa. Kama huna mwambie Sina. Akini jitahidi uwe karibu naye Kwa kadiri itakavyowezekana. Pili umesema aliondoka na watoto wa kike hujui aliishi vp ukizingatia uchumi ni mgumu hivyo alifanya alichoweza kulingana na mazingira.
 
Wazazi wa hivi inabidi umtake akueleze sababu za yeye kukukimbia. Usipozielewa mteme mazima kwa sababu hakuna connection.
Nina mtazamo tofauti kidogo ju ya hu ushauri wako kwa dogo. Akitaka kujua why mama aliondoka na kumuacha baba yao, atapata ukweli wa upande mmoja tu, is only mama ndio atasema sababu za yeye kuondoka, huenda akaongeza na chumvi nyingi sana ili baba aonekane mbaya na hatasema ni nini yeye alimkosea baba yake BUT baba hatakuja kusema why mkewe aliondoka, hata kama mama yake alifanya jambo baya sana na la aibu; baba hatasema, siri hiyo itabaki kifuani mwake hadi anakufa so nashauri, dogo wala asitafute kujua why wazazi wake walitengana, itamsababishia kumchukia mzazi mmoja. Aishi nao hivo hivo bila kujua why wao walitengana
 
Huwezi ukawa unajua kila kitu punguza ujuaji.
 
Kwani ukimjali mama yako unapungukiwa nini? si mama yako huyo na ndiye aliyekuzaa. Wanawake ni viumbe wa hisia, mama anataka kuona bado anahitajika kwa watoto wake, muoneshe bado unamuhitaji acha kujiona Mwamba
 
huenda anamaisha magumu hata vocha ni kama amenunua gari chunguza kwanza zen ujitahidi kumsalimia
 
Hata wajinga huzaa watoto.

kigezo cha kuwa mzazi si kigezo cha kukwepa uwajibikaji na kutaka huruma na upendo ambao huku utengeneza tangu awali.

Ubaya ubaya.

Hakuna huruma wala msamaha kwa mzazi mjinga.
 
Sababu zilizopelekea wao kutengana na kuishia kugawana watoto kwa ajili ya kuwalea wewe haikuhusu..

Cha muhimu ni kuwa sasa mna mawasiliano so play your part as a son.

Baraka zako zinatoka Kwa wote baba na mama.
 
Pole sana mkuu i
 
Nilipokuwa mdogo Kila nilichoambiwa na mama kuhusu baba nilikuwa nikiamini. Nilivyokuwakuwa nikagundua baba alikuwa dume hasa asiyependa kuendeshwa na wanawake. Maamuzi yake daima yalilenga kuhakikisha familia inakula na inaishi poa japo familia ilikua kubwa. Kwa Hili mama nilisikia akikiri siku Moja kwamba Kwa maisha ya miaka 40+ aliyoishi na baba familia haikuwahi kulala na njaa.
Nilikua kugundua pia stori zote mbaya za dingi kutoka Kwa mama ni kwamba kumbe dingilai alikuwa anawakanda mamanzi vibaya coz miaka hiyo Mzee pesa ipo na Maza wivu ulimshika.
Leo maza na faza ni wazee but ule wivu Bado humsumbua Maza . Siku Moja nilisikia alisema mama flani na flani ni maadui zangu siwapendi hata kuwaona.
So kijana huwezijua mambo ni mengi kwanini Maza aliondoka na girls faza akaondoka na boys.
 
Wazazi wa hivi inabidi umtake akueleze sababu za yeye kukukimbia. Usipozielewa mteme mazima kwa sababu hakuna connection.
hapo mzazi hakuwakimbia WATOTO...ndoa ilivunjika... wazazi wakagawana WATOTO,..... mama hana kosa,...ni uelewa mdogo wa mtoto,.....vipi kama mama alipewa vitisho vizito na Baba yao?,.. ..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…