Wabunge wa kupelekewa hiyo mikataba ndo akina Ndiyoooooo? Kifupi hakuna hoja itapita ndani ya bunge iliyoasisiwa na ccm isiungwe mkono. Wataunga mkono hoja.
Wale wanawaza hela tu
Ni kweli kabisa ulichokiongea.
Tukisema tuwaondoe kwa kuandamana watatupiga risasi, mabomu ya machozi na kutufungulia kesi za uhaini, watatufunga gerezani.
Tukisema twende mahakamani kufungua kesi,tutashindwa maana mahakama, mahakimu na Majaji ni wa kwao.
Tukisema tuwaondoe kwa sanduku la kura,hapa tutapoteza muda wataiba kura maana tume ya uchaguzi ni yao, watahonga na kuwatumia wasimamizi wa uchaguzi ili kura ziibwe na watangazwe wao.
Tukisema tuwaamini wapinzani, hawa hawatabiriki kuna wakati nao wanawekwa mifukoni na hawa hawa watawala, wananchi tunachezwa shere.
Tukisema tuwatumie viongozi wa dini, kuna baadhi wanamegewa mkate wa taifa na hawa hawa viongozi wa serikali wanageuka kuwa Mafarisayo na Masadukayo hata wasiweze kukemea uovu.
Tukisema tuloge hatuwezi maana wenzetu Wabunge wana hela zetu nyingi za kodi huwa wanatoa kafara za ng'ombe makumi makumi wakati sisi uwezo wetu ni kuku, bata na njiwa ,wameinajisi nchi yetu.
Wasomi wetu wako "busy "kukimbizana na fursa za chama na Serikali ili nao wafurahie mema ya nchi mpaka wanafikia kuingia mikataba ya kipumbavu inayoigharimu nchi, kwasababu wanaambiwa watapewa kidogo. Prof Mruma hakushindwa kujibu maswali isipokuwa mkataba ulikuwa wazi kwamba ulisainiwa kimakosa tangu awali,alibanwa akakosa mahali pa kutokea.
Mfano mkataba usainiwe hauna kikomo, hautavunjwa hata akiingia kiongozi mwingine.Sasa itokee umevunjwa (breach),huyu atakayekwenda nje kuutetea ataongea nini zaidi ya kujiumauma tu.
Nina wazo kwa Watanzania.
Hivi hatuwezi kuhamasishana sisi kwa sisi kumlilia Mungu kila mtu kwa wakati wake na tukajibiwa maombi kwa kuondoa huu udhalimu unaoendelea hapa nchini?
Tusiwategemee Viongozi wa dini eti kutusaidia kutuombea, tunaweza kuomba maana Mungu ni wetu sote ,anasikia maombi yetu, hatuhitaji bunduki wala panga kufanya mabadiliko.
Laana isiyo sababu haimpati mtu. Sisi sababu tunayo, tumewachekea sana wametuzoea sana.
Sisi tuna haki. Mithali 15:28
Wenye hekima wataelewa, ila wapumbavu na walevi wa madaraka watabaki kujibaraguza.
MUNGU IBARIKI TANZANIA.