Wanasheria tusaidieni kufungua kesi mahakamani ili mikataba yote ya rasilimali zetu ambayo Rais Samia kasaini na wageni ipelekwe bungeni

Wanasheria tusaidieni kufungua kesi mahakamani ili mikataba yote ya rasilimali zetu ambayo Rais Samia kasaini na wageni ipelekwe bungeni

Mbaya zaidi rasilimali zinazoshambuliwa ni za Tanganyika, baada ya hapo mtu anaenda kutulia zake Kizmkazi, wqtanganyika watabaki wanahaha wenyewe na kulaumiana na viongozi watanganyika waliokuwa na nanafasi wakati wa ushambuliaji wa rasilimali hizo.
 
Wanasheria wetu wanaonisoma, naombembeni mlisaidie Taifa kufungua kesi mahakamani ili mikataba yote inayohusu rasilimali zetu ambazo utawala wa Rais Samia umesaini ipelekwe bungeni.

Tunajua kuwa ipo sheria inayohusu rasilimali na Soveregnty ya nchi, inayotaka mikataba yote inayohusu rasilimali za nchi yetu ipitishwe bungeni.

Sasa tunasikia rais kasaini mkataba wa Ushirikiano na waarabu wa UAE kuhusu misitu yetu. Mkataba haujapitishwa bungeni na sisi wananchi hatujui humo ndani kuna nini!.

Ipo haja mahakama iiagize serikali itii sheria.

Pengine ndiyo maana Samia badala ya kupeleka mikataba hiyo bungeni yeye anakimbilia kubadili sheria ili kuhalalisha uvunjaji wake wa sheria.

Hii maana yake ni kwamba anajua fika wakati anasaini mikataba hiyo, alikuwa anavunja sheria lakini akaamua tu kusaini kwa kuwa anajua atazibsdili sheria zinazombana kumfavor yeye.

Na si mkataba wa misitu tu, tunasilia kuwa kasaini mikataba mingine 37 ambayo hatujui ndani kuna nini.

Ipo haja mahakama imlazimishe mikataba inayopaswa kufikishwa bungeni ifike bungeni!.
Ila kabla ya kwenda bungeni pia watusaidie wananchi wapige kura ya maoni,juu ya imani yao kwa bunge letu pia,ili iwapo wataonyesha imani nalo,kusiwe na mashaka juu ya upitishwaji au ukataji wa maamuzi yake.Kura ya maoni isimamiwe na tume huru isiyo egemea serikali,bunge,wala mahakama.
 

Kwa ile IGA hata kama mimi ni DP. Yaani ningeiambia gov kuwa hata kuijadili ni haramu. Kifupi ningewakomesha milele after 1000 mngekuwa history.
 
Back
Top Bottom