Steven Joel Ntamusano
JF-Expert Member
- Jun 17, 2023
- 5,203
- 3,913
Hiyo Vicarious Liability mpaka iwepo ni lazima uwepo ushahidi wa kutosha kwamba wauaji wametumwa na mamlaka ya Rais.Mkuu Steve, Steven Joel Ntamusano,
Kwanza naomba nikuhakikishie Rais Samia ni mkweli kabisa, kama ni kuua, ameua sisimizi tuu, ila anajua watu wake wanafanyaga nini, akiwa VP alimtembelea Lissu hospitalini Nairobi na kulihakikishia taifa, wale sio watu wao, watu wetu ukikosa mbili unaandika maelezo!.
Kanuni ya vicarious liability anatamka mamlaka ndio inabeba the final responsibility kwa matendo ya maofisa wake, hivyo kama ni watu wake, anapaswa kusafisha. Ile 1976 Nyerere aliwasafisha!.
Mazingira ya baadhi ya matukio haya suggest sio "wasiojulikana" bali ni 'wasiojulikana', hivyo kwa vile kwa mujibu wa Katiba yetu, the right to life iko kwenye katiba yetu, ila kuna mazingira fulani inaondolewa na mamlaka pekee ya kusaini death warrant ni mamlaka moja tuu, President of URT, ikitokea wamefanya walichokifanya bila kumhusisha au kumdanganya hao watu ni dissidents, they deserve to be eliminated, vicarious liability inasema the one responsible ni mamlaka na sio watekelezaji.
Ndio maana tumewahi kushauri TISS Ikanushe tuhuma za uvamizi, utekaji, utesaji na mauaji!. Wasijadiliwe na Bunge kwa uwazi bali wachunguzwe, wakithibitika wafumuliwe!
Hivyo kama kuna watu wake wanatenda vitendo hivyo behind the closed doors, awashughulikie vinginevyo watamponza bure yeye na karma ikaja kumshukia.
Sisi wenye jicho la tatu, tunaumia sana jinsi watu wake wanavyomset na issues za uhaini just to justify vitendo vyao viovu!. Uhaini My God!. Kuna Uwezekano Anadanganywa na Kadanganyika? I Don't Believe This!. Sitatizwi na Uongo Wao, Natatizwa na The Motives Behind Such Lies! hili la uhaini nimeliendeshea darasa humu na magazetini Ijue Katiba ya JMT kwa Jicho la Mtunga Katiba: Watanzania Tusishabikie Uhaini. Hukuna Uhaini wa Kauli na Maneno, Uhaini ni Mipango na Matendo
Mtu Watanzania waliomkabidhi dhamana ya maisha yao ni mtu mmoja, watumishi wote wa umma, wanafanya kazi kwa niaba ya mtu mmoja tuu, the big boss, wakiharibu kazi wanatakiwa kuwajibishwa, wasipowajibishwa then the vicarious liability shifts to the boss!.
Waswahili wana kamsemo chao cha mchelea mwana kulia, hulia yeye!.
P
Waliuliwa wengi kule MKIRU na wengine miili ikawa inaokotwa Coco Beach sikuwahi kuisikia hiyo liability ikiwa kazini kwa maana ya Hayati JPM kubebeshwa mzigo wa hayo mauaji.
Vyombo vya upelelezi vipo siku zote na ni jukumu lao, kuanza kumhusisha moja kwa moja Rais na murder cases za raia wake kisa masuala ya kisiasa ni uoga na wasiwasi wetu ambao siku hizi unaendelea kuwa mkubwa zaidi.