Wanasheria Waelimisheni Viongozi Wetu Kitu Kinachoitwa "Vicarious Liability", Hata Kama Wewe Hujaua, Kama Muuaji ni Mtu Wako, Then Unawajibika Wewe

Wanasheria Waelimisheni Viongozi Wetu Kitu Kinachoitwa "Vicarious Liability", Hata Kama Wewe Hujaua, Kama Muuaji ni Mtu Wako, Then Unawajibika Wewe

Mkuu Steve, Steven Joel Ntamusano,
Kwanza naomba nikuhakikishie Rais Samia ni mkweli kabisa, kama ni kuua, ameua sisimizi tuu, ila anajua watu wake wanafanyaga nini, akiwa VP alimtembelea Lissu hospitalini Nairobi na kulihakikishia taifa, wale sio watu wao, watu wetu ukikosa mbili unaandika maelezo!.

Kanuni ya vicarious liability anatamka mamlaka ndio inabeba the final responsibility kwa matendo ya maofisa wake, hivyo kama ni watu wake, anapaswa kusafisha. Ile 1976 Nyerere aliwasafisha!.

Mazingira ya baadhi ya matukio haya suggest sio "wasiojulikana" bali ni 'wasiojulikana', hivyo kwa vile kwa mujibu wa Katiba yetu, the right to life iko kwenye katiba yetu, ila kuna mazingira fulani inaondolewa na mamlaka pekee ya kusaini death warrant ni mamlaka moja tuu, President of URT, ikitokea wamefanya walichokifanya bila kumhusisha au kumdanganya hao watu ni dissidents, they deserve to be eliminated, vicarious liability inasema the one responsible ni mamlaka na sio watekelezaji.

Ndio maana tumewahi kushauri TISS Ikanushe tuhuma za uvamizi, utekaji, utesaji na mauaji!. Wasijadiliwe na Bunge kwa uwazi bali wachunguzwe, wakithibitika wafumuliwe!

Hivyo kama kuna watu wake wanatenda vitendo hivyo behind the closed doors, awashughulikie vinginevyo watamponza bure yeye na karma ikaja kumshukia.

Sisi wenye jicho la tatu, tunaumia sana jinsi watu wake wanavyomset na issues za uhaini just to justify vitendo vyao viovu!. Uhaini My God!. Kuna Uwezekano Anadanganywa na Kadanganyika? I Don't Believe This!. Sitatizwi na Uongo Wao, Natatizwa na The Motives Behind Such Lies! hili la uhaini nimeliendeshea darasa humu na magazetini Ijue Katiba ya JMT kwa Jicho la Mtunga Katiba: Watanzania Tusishabikie Uhaini. Hukuna Uhaini wa Kauli na Maneno, Uhaini ni Mipango na Matendo

Mtu Watanzania waliomkabidhi dhamana ya maisha yao ni mtu mmoja, watumishi wote wa umma, wanafanya kazi kwa niaba ya mtu mmoja tuu, the big boss, wakiharibu kazi wanatakiwa kuwajibishwa, wasipowajibishwa then the vicarious liability shifts to the boss!.

Waswahili wana kamsemo chao cha mchelea mwana kulia, hulia yeye!.

P
Hiyo Vicarious Liability mpaka iwepo ni lazima uwepo ushahidi wa kutosha kwamba wauaji wametumwa na mamlaka ya Rais.

Waliuliwa wengi kule MKIRU na wengine miili ikawa inaokotwa Coco Beach sikuwahi kuisikia hiyo liability ikiwa kazini kwa maana ya Hayati JPM kubebeshwa mzigo wa hayo mauaji.

Vyombo vya upelelezi vipo siku zote na ni jukumu lao, kuanza kumhusisha moja kwa moja Rais na murder cases za raia wake kisa masuala ya kisiasa ni uoga na wasiwasi wetu ambao siku hizi unaendelea kuwa mkubwa zaidi.
 
Hiyo Vicarious Liability mpaka iwepo ni lazima uwepo ushahidi wa kutosha kwamba wauaji wametumwa na mamlaka ya Rais.
Mkuu Steve, Steven Joel Ntamusano, vicarious liability, haihusu kiongozi kuhusika direct au kumtuma, kiongozi anahisika vicariously kama baba anavyo wajibika kwa makosa ya mwanae hata kama hajamtuma,
Waliuliwa wengi kule MKIRU na wengine miili ikawa inaokotwa Coco Beach sikuwahi kuisikia hiyo liability ikiwa kazini kwa maana ya Hayati JPM kubebeshwa mzigo wa hayo mauaji.
Ni bahati Bongo hatuna mawakili aggressive kutetea haki za watu watu masikini wa kutupwa ambao wanauawa kwa makosa na serikali. kuna vifo vingi serikali zimehusika, lakini watu hao hawana uwezo wa kuajiri mawakili na wengi wa mawakili wetu ni after money, hakuna mawakili wa kutosha wa pro borno kufungua mashitaka hayo kwa kujitolea matokeo yake ni kuiachia tuu karma, iliwashughulikia viongozi wetu.
Tatizo la karma, inapokushughulikia haikuambii kosa lako!.

Lakini alipouliwa Imran Kombe, aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TISS, familia yake ilifungua shauri la vicarious liability na familia walilipwa fidia ya zaidi ya shilingi milioni 300!.
Vyombo vya upelelezi vipo siku zote na ni jukumu lao, kuanza kumhusisha moja kwa moja Rais na murder cases za raia wake kisa masuala ya kisiasa ni uoga na wasiwasi wetu ambao siku hizi unaendelea kuwa mkubwa zaidi.
Hakuna mtu yoyote amemuhusisha rais na mauaji, ninachofanya hapa ni kufundisha somo la kuwajibika, watendaji wote wa serikali, kila wanàfanya ni kwa niaba ya rais wa JMT, hivyo muwajibikaji wa mwisho anayewajibika na uhai wa raia wake, ni rais wetu, ikitokea waserekili wamefanya madudu ya ajabu
ajabu, rais, anapaswa kuwawajibisha, na wasipowajibishwa, ni rais ndio anakuja kuwajibishwa na karma kwa makosa ya watendaji wake!. Kwa vile si wengi wanaijua karma, ndio maana tunawashauri wateule wake wawajibike kumuepushia adhabu ya karma kwa bosi wao Wito Kwa Viongozi Wetu: Unapokosea, hata kwa kujikwaa tu ulimi, tujenge utamaduni wa kuwajibika ili kumuepushia Rais wetu kubeba mzigo wa karma
Na Utamaduni Viongozi Kuwajibika umeishia wapi?, Mbona Mwinyi, mauaji Mwanza aliwajibika?. Tusiruhusu madoa haya ya damu kuichafua nchi yetu -Wajibikeni!
P
 
Watanzania Tungekua na akili nafikiri wote tungeungana kudai katiba mpya katiba itayoweka wazi kuwajibisha viongozi wote kuanzia Rais katiba itayopunguza nguvu ya Rais katiba itayoipa nguvu mihimili mingine ila kwa ya sasa bado sana tulifukuza wakoloni tukaacha katiba yao na tukaendelea kuitumia ni hatari sana katiba ndo ukoloni wenyewe
 
Wanabodi

Hata yale matukio ya utekaji, utesaji na mauaji enzi za kipindi kilee... watu humu tulishauri TISS Ikanushe tuhuma za uvamizi, utekaji, utesaji na mauaji!. Wasijadiliwe na Bunge kwa uwazi bali wachunguzwe, wakithibitika wafumuliwe! hao majamaa wali mute kimya, wakijua hawawezi kufanywa lolote, lakini mwisho wa siku aliyewajibishwa ni top boss wao!.

Hivyo ni muhimu sana kwa viongozi wetu kuijua hii vicarious liability kwa vifo vyovyote vya kizembe vinavyotokea chini ya mamlaka yao, na matukio yote ya utekaji, utesaji na watu kuuliwa au kupotezwa, hata kama wahusika hawatatafutwa, serikali inajifanya kusema itafanya uchunguzi, kumbe ni uongo tuu kwasababu kila kitu wanakijua kwasababu hao watu wanaotenda vitendo hivyo ni watu wao!, hivyo hawatapatikana, hawatashitakiwa popote, na hawata wajibishwa kwa vitendo vyao viovu, lakini hukumu karma ambayo ndio hukumu ya haki hapa duniani, inakuwa ii juu yao!, anayewajibishwa mwisho, sio wale watendaji, wale walikuwa ni watekelezaji tuu, lakini anayewajibika, vicariously ni yule mwenye dhamana. The Power of Karma- Ndio hukumu pekee ya haki kamili hapa Duniani. Unahukumiwa kwa matendo yako! .
huu ni ugaidi unaofanywa na serikali kwa watu wake
Haya majitu majinga sana!, yanafanya mambo ya hovyo
na vitu vya ajabu ajabu!, hayajui kuwa mwisho wa siku watamponza bosi wao mkuu!。
P
 
Watanzania Tungekua na akili nafikiri wote tungeungana kudai katiba mpya katiba itayoweka wazi kuwajibisha viongozi wote kuanzia Rais katiba itayopunguza nguvu ya Rais katiba itayoipa nguvu mihimili mingine ila kwa ya sasa bado sana tulifukuza wakoloni tukaacha katiba yao na tukaendelea kuitumia ni hatari sana katiba ndo ukoloni wenyewe
true
P
 
Paschal, umeongea kitu cha maana sana. Hata hivyo, kama tunataka kuwasanua wasije siku moja wakaadhibiwa kwa makosa ya subordinate wao, tunatakiwa kuwafundisha kitu kinaitwa "COMMAND au SUPERIOR RESPONSIBILITY", hii ndio principle iliyopo kwenye international law, na ndiyo viongozi wengi wanaweza kushitakiwa. Kwa Tanzania, kosa la subordinate ni "ENFORCED DISAPPEARANCE", watu kupotea ovyo, huko kutekwatekwa huko, na mara unaona walikamatwa na polisi na hawakuwa na sababu za msingi. hayo mambo ya kina mdude, sativa, hao waliokamatwa na polisi wazi wasi na hawajulikani walipo na serikali haitaki kuacknowledge walipo, ni kosa. kuna siku dunia ikikaa vibaya kuna mtu anaweza kuletewa samansi/arrest warrant wampeleke the hague hapa. washaurini viongozi wenu.
 
Back
Top Bottom