PostGE2025 Wanasheria watinga ICC na kufungua kesi dhidi ya Rais Samia na wakuu wa Vyombo vya Usalama Tanzania

PostGE2025 Wanasheria watinga ICC na kufungua kesi dhidi ya Rais Samia na wakuu wa Vyombo vya Usalama Tanzania

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Mkuu, Point wanayoisimamia Serikali kwasasa ni kusema kuwa waliouwa watu si Watanzania ni Wanajeshi kutoka nje na wameua mpaka polisi wetu.

Na hawatashindwa kuleta list ya Polisi waliouawa hata kwa kutengeneza na kuwapa namba

Hili mnalipinduaje?
Hiyo hoja yao ni ya kitoto sana.
Mpaka raia wa nchi jirani waingie na siraha nchini mwetu na wafanye mauaji,vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vilikua wapi na vinafanya nini?
Mpaka sasa raia wangapi wa kigeni waliokamatwa kwa kufanya hayo mauaji?
 
Walahi kwahili Kikwete kampiga tobo Samia. Alafu anavyomfariji kinafiki huku akijua kizimkazi yupo maji ya shingo. Mama aumia iweje yeye tangu uhuru ndio amwage damu kiasi hiki.

Walahi anajutraa. Wahuni wanamsukumizia kwenye shimo la choo, Kikwete aseme yeye hana cheo chochote huko serikalini.

Hahusiki na mambo yayo. Nye nye.
Hachomoki
 
Humu ndani watu wanaidharau ICC, lakini hawajui kwa Nini Putin na ubabe wake hawezi kukanyaga , Ulaya na nchi nyingi tuu...
Putin anakwenda kwenye nchi ambazo sio mwanachama wa ICC kama China, US, India, Noth Korea labda na Belarus.. sehemu nyingine hakanyagi...mkutano wa BRICKS Africa Kusini kashindwa Kwenda...
Angalia Netanyahu...alienda US akakwepa anga la Ulaya makusudi..anajua akitua hata kwa bahati mbaya ni mwisho wake

Sisi Tanzania Rais akipewa arrest warrant..hawezi Kwenda hata Kenya...itakuwa balaa kubwa kwake...akistaafu bado watamtafuta...
Haya ni matokeo ya uongozi mbovu usio sikiliza watu na kuona Kila siku Watanzania ni mazezeta...
 
Kwa ufupi wakikutwa na hatia siku akinyanyua mguu wake kwenda nje ya mipaka ya Tanzania atakamatwa. Pona pona yake ni kubakia nchini...

Hivyo basi ule u Vasco da Gama hautokuwepo tena kwake....
Kwahiyi asipotoka ndo basi tena?
 
Kazi kubwa vipi wakati picha za satellite zipo nyingi, na baadhi ya video na picha zinaonyesha sura za wauaji?

Sawa. Tuseme basi kwa hizo satellite videos and pictures tutakua tumeweza thibitisha uvunjifu wa haki za binadamu, ikiwemo haki ya kuishi kwa Watanzania wenzetu wengi. Lakini je tuna ushahidi upi wa kumuunganisha raisi na wakuu wake wa majeshi ktk hizo abuses? Kamanda mkuu wetu wa jeshi na wakuu wengine wanaweza sema wao hawakuwatuma askari wa chini kuua raia. Je askari wetu wanaweza testify ICC kwamba waliagizwa na Mkunda au Samia?
 
Lakini je tuna ushahidi upi wa kumuunganisha raisi na wakuu wake wa majeshi ktk hizo abuses? Kamanda mkuu wetu wa jeshi na wakuu wengine wanaweza sema wao hawakuwatuma askari wa chini kuua raia. Je askari wetu wanaweza testify ICC kwamba waliagizwa na Mkunda au Samia?
Dah,
Kwa hii kauli yako ni wazi hujui majeshi yanavyofanya kazi. Hilo halihitaji ushahidi, lipo wazi mno
 
Dah,
Kwa hii kauli yako ni wazi hujui majeshi yanavyofanya kazi. Hilo halihitaji ushahidi, lipo wazi mno
Nakuelewa vizuri sana tu. Ila najaribu kukuonyesha kwamba kwa tawala za kwenye jamii zetu za hili bara jeusi usishangae kuambiwa nyeusi ni nyeupe na hakuna atakaye pinga.
 
Upo sahihi zikitumika hizo mahakama za kupewa maelekezo kutoka juu, ila siyo iCC
ICC watategemea witnesses from Tz, ambao kwa muktadha wa hoja yako tuseme watakua ni askari waliotumwa kutuliza fujo OCT 29. . Hao witnesses wanaweza kupotezwa au kuamriwa cha kusema na hakuna kitu ICC wanaweza fanya. Hicho ndicho ninachomaanisha. Ndicho kilichowashinda kule Kenya. Unaweza onyesha kabisaa watu wanaua. Ila uthibitishe sasa nani kamtuma nani kuua.
 
Back
Top Bottom