Wanasiasa acheni kuwachonganisha watoa huduma za afya na wananchi

Enthusiastic

Senior Member
Joined
Dec 21, 2023
Posts
109
Reaction score
256
Kwa sababu watanzania wengi ni wajinga, wamezoea kudanganywa, wanadanganyika, wanapenda kudanganywa na hawapendi kuambiwa ukweli.
Kumekuwa na changamoto ya sera ya afya inayotaka huduma za uzazi na za watoto chini ya miaka mitano kushindwa kutekelezwa ipasavyo. Mimi nataka kuchangia kama ifuatavyo;
1. Huduma za afya hazitolewi Kwa matamko ya wanasiasa , huduma zinahitaji fedha. Vituo vinanunua dawa na vifaa tiba kutoka MSD na washitiri. Kule MSD vya bure ni condoms na ARVs nazo hatujui hatma yake baada ya Trump kufanya yake
2. Hospitali za umma zinaendeshwa na vyanzo mbalimbali vya mapato baadhi ni kama ifuatavyo
a. NHIF - Hili ni shirika la umma nalo lina changamoto zake
b. User fee- haya ni malipo ya papo kwa papo
c. Mfuko wa chanjo (GAVI) - Hapa huwezi sikia Kuna mtoto amelipia hela kuchanjwa. Chanjo zingine kama ya kichaa cha mbwa utalipia kwa sababu haiko kwenye ufadhili
d. Basket Fund - Hizi ni fedha ambazo hutolewa na serikali ikishirikiana na benki ya Dunia na wadau wengine wa maendeleo ambazo kwa baadhi ya hospitali hazikidhi mahitaji
3. Napenda kumpongeza RC Chalamila kwa kusema ukweli na kama wanasiasa wanataka huduma za uzazi na watoto chini ya miaka mitano zitolewe bure basi waitake serikali iongeze ufadhili kwenye huduma hizo vinginevyo waache porojo Kwa sababu tu watanzania wengi ni wajinga wajinga. Tafahali mods msiuunganishe Uzi huu
4. Ninaomba kuwasilisha
 
Acha ujinga mkuu, hivi wewe unaona ni sawa mjamzito kulipia huduma ya uzazi? Tena ilipaswa mama akijifungua apewe na package ya pesa kwa ajili ya lishe ya mzazi na mtoto.
Ujinga ni wenu na wanasiasa wenu. Nimekwambia kule MSD na washitiri hawatoi vya bure. Huduma bure itawezekana endapo ufadhili wa serikali na wadau wa maendeleo utatosheleza mahitaji
 
Acha ujinga mkuu, hivi wewe unaona ni sawa mjamzito kulipia huduma ya uzazi? Tena ilipaswa mama akijifungua apewe na package ya pesa kwa ajili ya lishe ya mzazi na mtoto.
Cheki akili hizi. Mke wako, mtoto wako, unataka serikali imhudumie mkeo?
Mimba sio dharura. Unapopanga kuzaa, jipange pia na fedha za kumhudumia mjamzito wako. Acheni kuleta siasa kwenye kazi za watu. Acheni Propaganda kwenye afya. Hata Marekani huduma za Mama Na mtoto sio bure, sembuse huku kwetu?
Shituka.
 
We mpumbavu unaishia Afrika ndiyo Maana unaropoka ujinga, umelelewa kimasikini ukakua na mentality za roho mbaya ndiyo maana unaona jambo la ajabu mzazi kulipwa
 
Kwa sababu watanzania wengi ni wajinga, wamezoea kudanganywa, wanadanganyika, wanapenda kudanganywa na hawapendi kuambiwa ukweli.
Kumekuwa na changamoto ya sera ya afya inayotaka huduma za uzazi na za watoto chini ya miaka mitano kushindwa kutekelezwa ipasavyo. Mimi nataka kuchangia kama ifuatavyo;
1. Huduma za afya hazitolewi Kwa matamko ya wanasiasa , huduma zinahitaji fedha. Vituo vinanunua dawa na vifaa tiba kutoka MSD na washitiri. Kule MSD vya bure ni condoms na ARVs nazo hatujui hatma yake baada ya Trump kufanya yake
2. Hospitali za umma zinaendeshwa na vyanzo mbalimbali vya mapato baadhi ni kama ifuatavyo
a. NHIF - Hili ni shirika la umma nalo lina changamoto zake
b. User fee- haya ni malipo ya papo kwa papo
c. Mfuko wa chanjo (GAVI) - Hapa huwezi sikia Kuna mtoto amelipia hela kuchanjwa. Chanjo zingine kama ya kichaa cha mbwa utalipia kwa sababu haiko kwenye ufadhili
d. Basket Fund - Hizi ni fedha ambazo hutolewa na serikali ikishirikiana na benki ya Dunia na wadau wengine wa maendeleo ambazo kwa baadhi ya hospitali hazikidhi mahitaji
3. Napenda kumpongeza RC Chalamila kwa kusema ukweli na kama wanasiasa wanataka huduma za uzazi na watoto chini ya miaka mitano zitolewe bure basi waitake serikali iongeze ufadhili kwenye huduma hizo vinginevyo waache porojo Kwa sababu tu watanzania wengi ni wajinga wajinga. Tafahali mods msiuunganishe Uzi huu
4. Ninaomba kuwasilisha
Hujatuambia Sera ya Serikali juu ya “huduma za uzazi na za watoto chini ya miaka mitano” inasemaje!
 
Screenshot_20250204-195601.jpg
Screenshot_20250204-195622.jpg
 
Hujatuambia Sera ya Serikali juu ya “huduma za uzazi na za watoto chini ya miaka mitano” inasemaje!
Sera naitambua vizuri. Shida mtunga sera katunga kisha kaishia mitini. Tunataka mtunga sera apeleke fedha zinazokidhi mahitaji kwenye vituo vya kutolea huduma ili sera aliyotunga itekelezeke. Tunamuomba mtunga sera aache porojo afanye kazi
 
Sera ni independent of mtunga sera. Mtunga sera awepo au asiwepo, sera lazima ifuatwe kama bado haijafanyiwa marekebisho!
 
Kwa sababu watanzania wengi ni wajinga, wamezoea kudanganywa, wanadanganyika, wanapenda kudanganywa na hawapendi kuambiwa ukweli.
Kumekuwa na changamoto ya sera ya afya inayotaka huduma za uzazi na za watoto chini ya miaka mitano kushindwa kutekelezwa ipasavyo. Mimi nataka kuchangia kama ifuatavyo;
1. Huduma za afya hazitolewi Kwa matamko ya wanasiasa , huduma zinahitaji fedha. Vituo vinanunua dawa na vifaa tiba kutoka MSD na washitiri. Kule MSD vya bure ni condoms na ARVs nazo hatujui hatma yake baada ya Trump kufanya yake
2. Hospitali za umma zinaendeshwa na vyanzo mbalimbali vya mapato baadhi ni kama ifuatavyo
a. NHIF - Hili ni shirika la umma nalo lina changamoto zake
b. User fee- haya ni malipo ya papo kwa papo
c. Mfuko wa chanjo (GAVI) - Hapa huwezi sikia Kuna mtoto amelipia hela kuchanjwa. Chanjo zingine kama ya kichaa cha mbwa utalipia kwa sababu haiko kwenye ufadhili
d. Basket Fund - Hizi ni fedha ambazo hutolewa na serikali ikishirikiana na benki ya Dunia na wadau wengine wa maendeleo ambazo kwa baadhi ya hospitali hazikidhi mahitaji
3. Napenda kumpongeza RC Chalamila kwa kusema ukweli na kama wanasiasa wanataka huduma za uzazi na watoto chini ya miaka mitano zitolewe bure basi waitake serikali iongeze ufadhili kwenye huduma hizo vinginevyo waache porojo Kwa sababu tu watanzania wengi ni wajinga wajinga. Tafahali mods msiuunganishe Uzi huu
4. Ninaomba kuwasilisha
Ambao hawako kwenye management sekta ya afya hasa hizi za serikali hawawez elewa kabisa hili, hospital hauwez kujiendesha bila kupata mapato. Hizi exemptions labda kama serikali ingekuw inaleta fungu kama wanavyofanya projection na OCs ,otherwise itabaki tu kuwa siasa
 
Hizo hospital za umma ni mali za wahudumu wa Afya?
 
Sera ni independent of mtunga sera. Mtunga sera awepo au asiwepo, sera lazima ifuatwe kama bado haijafanyiwa marekebisho!
Basi tumia sera hiyo kujifungua nyumbani kwako.

Unaelekezwa sera ni maneno tu, vitendo na utekelezaji ndio huo mpaka serikali itie fungu. Hospitali haiwezi nunua mahitaji ya mjamzito kujifungua kwa kutumia sera kama sarafu. Ni lazima ziwepo shilingi.
 
Kumbuka Basket Fund wachangiaji zaidi ni donor Countries, Serikali sidhani kama huwa inaweka pesa mule kwenye hilo fuko, na wao hutoa ku subsidize gharama zote za Afya hasa kwa watanzania wengi tusiokuwa na uwezo, huwa hawabagui kwa mama na mtoto, wazee au vijana.

Budget ya Serikali kwa asilimia zaidi ya 50 imekuwa ikichangiwa na Donor countries.

Kuna Pesa zingine Serikali hupokea kwa miradi maalumu, kama kChanjo fulani, Kifua kikuu na ukoma, Ukimwi na siku hizi kumekuwa na Nchi na mashirika mbali mbali yamechangia Magonjwa yasiyoambukizwa kama Moyo, High Blood Pressure na n.k.

Wanasiasa wanaongea wanayoambiwa Bungeni na Serikali. Waliposema Elimu Bure wao wakachagiza hivyo hivyo, lakini Utasikia wazazi wanahimizwa kuchangia chakula, mara Madawati yametolewa na CRDB, au Mtu au kikundi fulani, lakini Serikali inasema Elimu ni Bure.

Afya hivyo hivyo, Wizara ikisema Huduma za Afya ni bure, wanasiasa huwa wanapanda kuchagiza walichoambiwa na serikali, na kwasababu CCM na Serikali ni wale wale sioni kwanini mmoja wao adanganye, na mwingine aseme ukweli.
Serikali itoke itoe tamkjo kwamba huduma 1,2,3 ni Bure na Huduma A,B,na C mwananchi achangie.

Lakini huwa tunapata taarifa nusu nusu, Bima ya Afya tuliambiwa ni kwa kila mwananchi, lakini siyo kila mwananchi ana bima. NHIF wanakwambia kifurushi fulani, vipimo utalipia, matibau utapata bure, waweke wazi kwamba Huduma ya afya ni Bure au tunapaswa kuchangia.

Hili siyo la siasa, ni la Serikali, sema tuna bahati mbaya CCM ndiyo Serikali, hivyo tunashindwa kufahamu lipi la kisiasa na lipi ni la serikali.
 
Basi tumia sera hiyo kujifungua nyumbani kwako.

Unaelekezwa sera ni maneno tu, vitendo na utekelezaji ndio huo mpaka serikali itie fungu. Hospitali haiwezi nunua mahitaji ya mjamzito kujifungua kwa kutumia sera kama sarafu. Ni lazima ziwepo shilingi.
Kwa kuwa aliyeweka hiyo sera ni Serikali na aliyeomba fedha Bungeni kwa ajili ya hiyo sera ni Serikali, taxpayers tunaipaje Serikali free pass kwamba sera ni maneno tu? Tumefika hapa kwa sababu ya docility kama hii. Tunahitaji kubadilika; tuwe na utamaduni wa kuwawajibisha wale tuliowaweka madarakani. Kama sera haitekelezeki, kwanini Serikali haiibadilishi na kuwaambia taxpayers ukweli wa mambo ulivyo?
 
Habari,

Wananchi hawafahamu kinachoendelea kwenye sekta ya afya, hasa sehemu za kutokea huduma za afya kama hospitali.

Kuna malipo ya aina mbili, kwanza ni malipo ya 'huduma' na pili ni malipo ya 'vifaa/vitendea kazi/bidhaa'. Sera inasema 'huduma' ni bure, na hapo wananchi wanafikiri serikali imemaanisha Hadi vifaa ni bure, sisi tunafanya kazi kwenye maeneo ya kutokea huduma,tunaambiwa na serikali hiyohiyo bidhaa'/vifaa WALIPIE, ila wakiwa kwenye majukwaa wanajificha nyuma ya neno 'huduma' ni bure.

Kwa hiyo, mjamzito akifika hospitali, huduma ya kuchunguzwa na daktari ama nesi, hiyo ni bure (wengine wanalipia kulingana na ngazi ya hospitali). Lakini,ikishakuwa vipimo ama dawa, lazima atalipia kwa sababu hiyo sio huduma, ni bidhaa.

Tujifunze tofauti ya 'huduma' na 'bidhaa'
 
Back
Top Bottom