Mustard Seed
Member
- Jan 30, 2025
- 13
- 9
Habari,Hizo hospital za umma ni mali za wahudumu wa Afya?
Hospitali za umma ni Mali ya wananchi wa Tanzania, zinasimamiwa na serikali kwa niaba ya wananchi.
Ila tukupe uelewa, ukifika hospitali ukakuta duka la dawa limejaa dawa,zile dawa hazijaletwa na serikali Ili zitolewe bure ( ni dawa chache sana ndizo zinaletwa kutolewa bure,kama dawa za UKIMWI, Kifuakikuu na baadhi ya Chanjo), zingine zote hospitali inazinunua bohari ya dawa, na inatakiwa kuziuza kwa wagonjwa wanapozihitaji. Halafu ukaguzi wa serikali unapita kuona kama zimetolewaje, mapato yanayopatikana ndiyo yanalipia huduma za maji,umeme, posho za wafanyakazi wanaojitolea ama mikataba, na kulipia wagonjwa wasiojiweza kwenye malipo kama wazee, watoto na wajawazito.
Hospitali zinatakiwa kujiendesha zenyewe kwa mapato yanayopatikana kwenye hivyo vifaa, ndipo wataweza kulipia wafanyakazi (malipo tofauti na mishahara ambayo inalipwa na serikali), wakanunua mashine na vifaa tiba, wakanunua mashuka,vitanda,magodoro, wakafanya marekebisho ya vifaa chakavu,wakanunua Oxygen,wakafanya usafi ,ulinzi etc