Wanasiasa acheni kuwachonganisha watoa huduma za afya na wananchi

Hizo hospital za umma ni mali za wahudumu wa Afya?
Habari,

Hospitali za umma ni Mali ya wananchi wa Tanzania, zinasimamiwa na serikali kwa niaba ya wananchi.

Ila tukupe uelewa, ukifika hospitali ukakuta duka la dawa limejaa dawa,zile dawa hazijaletwa na serikali Ili zitolewe bure ( ni dawa chache sana ndizo zinaletwa kutolewa bure,kama dawa za UKIMWI, Kifuakikuu na baadhi ya Chanjo), zingine zote hospitali inazinunua bohari ya dawa, na inatakiwa kuziuza kwa wagonjwa wanapozihitaji. Halafu ukaguzi wa serikali unapita kuona kama zimetolewaje, mapato yanayopatikana ndiyo yanalipia huduma za maji,umeme, posho za wafanyakazi wanaojitolea ama mikataba, na kulipia wagonjwa wasiojiweza kwenye malipo kama wazee, watoto na wajawazito.

Hospitali zinatakiwa kujiendesha zenyewe kwa mapato yanayopatikana kwenye hivyo vifaa, ndipo wataweza kulipia wafanyakazi (malipo tofauti na mishahara ambayo inalipwa na serikali), wakanunua mashine na vifaa tiba, wakanunua mashuka,vitanda,magodoro, wakafanya marekebisho ya vifaa chakavu,wakanunua Oxygen,wakafanya usafi ,ulinzi etc
 
Acha ujinga mkuu, hivi wewe unaona ni sawa mjamzito kulipia huduma ya uzazi? Tena ilipaswa mama akijifungua apewe na package ya pesa kwa ajili ya lishe ya mzazi na mtoto.
Yeye hajasema ni sawa au si sawa Yeye amezungumzia uhalisia wa mambo yalivyo huku kwa ground, hiyo habari ya ni sawa au si sawa hicho ni kitu kingine tena, kinahitaji labda uzi mwingine 🤗
 
Mkuu wakati mwingine shida sio ukosefu/ukata wa fedha bali ni uchaguzi sahihi wa vipao mbele husika.

Kingine Mkuu, asilimia 100% ya watunga sera na watunga sheria wana Bima ya afya hawaelewi maumivu ya wananchi wa kawaida!!

Yaani mwenye shine hajui mwenye njaa!!
 
🤔 🤔 🤔
 
Hivi chanjo ya tetanas huwaga ni nani anayeifadhili, maana takribani hospitali zote huitoa bure?
 
Kuchanganya watu, ama kutoa matamko nusu nusu huwa ni kwa faida ya nani?

Kama wanasiasa wanauma na kupulizia kama panya buku, kwanini staff wa tiba wasitoke hadharani kueleza ukweli wenye mashiko kama huu uliouelezea hapa, kunakuwa na uoga gani kuiweka sawa issue ya haki?

Kwa hiyo ninyi staff wa afya mnaona ni sahihi kuchonganishwa na wananchi nanyi mkakaa kimya ama kulikalia kimya jambo hilo?

Hivi raia kutofahamu ukweli ambao hajawahi kuelimishwa kwao, anastahili kuitwa mjinga?

Kwa jambo kama hili, hamuoni kuwa ninyi staff wa afya, kuanzia Waziri wenu mnastahili kubebeshwa lawama hizi moja kwa moja kwa kuwajibishwa?
 
Haohao wanaotoa maagizo ndio haohao wamegeuza kodi za wananchi ni mali yao.

Huyu aliyesema sitaki kusikia nini??
Watu wanamsifia sana lakini ni walewale kaulize wakulima watawasimulia mapito wanayopitia.

Hakuna maendeleo kila siku ni stori tu. Hospitali ya Mkoa ni masikitiko, barabara za mitaa ndio maumivu.

Yes wanasiasa acheni longa longa nyiiingi
 
Habari,

Naona ni faida ya wanasiasa, inawasaidia waonekane wao wako sawa, shida ni watendakazi wa chini yao (wahudumu wa afya)

Ila zipo juhudi zinazofanywa na serikali pamoja na wahudumu wa afya kupunguza gharama za matibabu kwa haya makundi maalumu,ila mtazamo sahihi ni kuwa gharama za matibabu zinachangiwa (mwananchi anahusika kugharamia, na serikali inapunguza gharama kwa kumchangia kwa sehemu)

Pia,badala ya kusema huduma ni bure, tuseme huduma ama gharama imelipiwa, yaani kile unachoambiwa ni bure, ujue Kuna mtu AMEKILIPIA kwa niaba yako, iwe ni serikali ama mapato mengine ya hospitali yakahusika kukulipia

Ili upate huduma na matibabu mazuri, kwa hali tuliyonayo sasa, ni vizuri ukajiandaa kifedha, ama ukawa na bima ya afya, la sivyo Kuna hatari ya kuhudumiwa chini ya kiwango( sio kwamba wahudumu wa afya wanakufanyia makusudi, Bali vipimo dawa na matibabu mengi kwa sasa sio bure kama inavyosemekana)
 
Nmekuelewa.
Ukiwa hotellni, kuna "Room service" inaweza kuwa bure au ya kulipia. Kama ni ya bure, ina maana unaletewa chakula au kinywaji bure lakini unalipia hicho kitu ulicholetewq. Kama ni paid room service ina maana utalipia ulichoagiza pamoja na huduma ya kuletewa.

Kama wanasiasa ndio wanatudanganya kupitia maana hizi, basi sisi wapiga kura ni mang'ombe tu
 
Kwahiyo ukifika hospitali mkeo anajifungua utawaambia maneno haya watoa huduma?
Utawaambia manesi habari za docility, taxpayers, sera, bungeni, serikali?

Unahisi hospitalini wanatishiwa na hizo siasa. Ukitaka siasa fanyia nje au usibebeshe mimba au usiumwe kwanza mpaka uzikamilishe, otherwise hunikuti hospitalini ukanambia siasa zako. Ni ama serikali yako itoe hela ujifungue au kutibiwa kwa gharama zake, au ulipie wewe. Siasa hazitolipia huduma wala vifaatiba.
 
Mama mjamzito analeta mlipa kodi mpya.. sio sawa kulipia gharama za kujifungua ili hali anawaletea mlipa kodi mpya wa siku za usoni.. lazima serikali imsaidie bure huyu mama kumleta huyo mlipa kodi mpya salama na kuhakikisha huyo mama anatoka kujifungua salama ili alete tena mlipa kodi mwingine mpya siku za husoni.

ILE KAULI ITAWAFANYA WATOA HUDUMA ZA AFYA KWA WAJAWAZITO WAWE NA VIBURI KUPITA KIASI NA KUJA KUPELEKEA KUIBUKA KWA VIFO VYA WAJAWAZITO KUTOKANA NA UZEMBE NA KIBURI CHA WATOA HUDUMA ZA AFYA. ILIPASWA MWESHIMIWA AKEMEE KIDIPLOMASIA KUSEMA VILE NI KAMA KARUHUSU WAJAWAZITO KUNYANYASIKA PINDI WATAKAPO KOSA HELA ZAKUJIFUNGULIA..
 
Asante

Ni kama ulivyoeleza

Kwa kuongezea, haya maneno ya huduma ni bure, yako zaidi kwenye TAMISEMI, sehemu za kutolea huduma ambazo ziko chini ya mamlaka za TAMISEMI. Ambazo ni zahanati, vituo vya afya na hospitali za wilaya (huko unaweza kupewa huduma hizo za bure,hata baadhi ya dawa na vipimo ukavipata kwa bure)

Changamoto yake ni kuwa huko Kuna huduma za awali kwa magonjwa ama changamoto za kiafya za kawaida tu,hata utaalamu wao ni wa chini, ukishapanda ngazi na kufika hospitali za juu,hizo habari za bure ni vema ukazisahau, matibabu ya huko ni gharama sana na hayatolewi bure, ukihitaji bure huko utapewa huduma nusu, utapewa matibabu ya kutuliza tatizo, sio kupona (kumbuka hio sio makusudi, bali ndiyo uwezo wao wa kukusaidia kulingana na uwezo wako wa kuchangia)

Tujiandae kifedha kabla ya kupata magonjwa, tuweke akiba ama tujiunge na bima za afya,itatusaidia kupata huduma nzuri za afya.
 
Habari,

Hoja yako inaelezea 'ideal health care' iweje, kwa mtazamo wako. Sisi tunaeleza uhalisia ukoje kwa sasa. Na hapo unajichanganya kufikiri mheshimiwa alikosea kuongea vile, ilhali hiyo ndiyo hali halisi ilivyo. Kwa kifupi, ulibahatika kusikia mambo yanayoendelea kwenye sekta ya afya, ambayo wananchi hawaambiwi kwenye majukwaa ya wanasiasa.

Sisi sote tunatamani huduma na gharama hizo ziwe 'bure' (sio bure haswa, bali zinalipiwa na serikali kwa niaba ya mwananchi mwenye kuhitaji). Ingetusaidia watoa huduma za afya kuwapa huduma nzuri kulingana na ugonjwa husika.

Ila kwa upande wako, kwa hali ilivyo sasa, kama uongozi utaendelea hivi hivi na miongozo hii tuliyonayo, ni heri ujiandae kifedha mapema kabla hujapatwa na tatizo la kiafya, ama uwe na bima ya afya inayoweza kukugharamia matibabu yote, la sivyo utahisi watoa huduma ndiyo wanakunyima huduma stahiki kumbe ni wewe mwenyewe hujajiandaa kulipia kadri inavyohitajika kwa uhalisia wa hospitali zetu. Utapewa huduma chini ya kiwango, utaathirika wewe na sio hao wanasiasa
 
Afterthought 1

Ikiwa mjamzito atapata shida kwa kukosa huduma kutokana na kukosa fedha, wanaohusika sio watoa huduma peke yake. Lawama itahusu serikali,watoa huduma, mgonjwa mwenyewe, mume/mwenzi wake, wazazi wake, ndugu zake na jamii inayomzunguka. Wote watalaumiwa kwa kushindwa kumsaidia mjamzito kujifungua salama.

Serikali jukumu la kwanza ni kuhakikisha vituo vya afya vipo, wahudumu wa afya wapo, vifaa tiba na madawa yapo (sio lazima yawe na yatolewe bure), miongozo ya matibabu ipo

Wahudumu wa afya jukumu lao ni kuwa na ujuzi na weredi katika fani zao,kuwapokea wagonjwa na kuwahudumia, kuwaelekeza gharama za matibabu kwa usahihi, kuwasaidia wasio na uwezo kwa kuwapa huduma na matibabu yenye msamaha wa gharama, ama kuwaunganisha na ustawi wa jamii katika vituo vyao, ama kuwapa huduma kwa kibali cha deni (wahudumiwe kwanza Kisha ndugu zao watakuja kulipia, wakishatafuta hizo fedha)

Jukumu la mgonjwa mwenyewe ni kutoa hizo gharama kutoka kwenye akiba yake, ama kupitia wanaomuuguza, mume,mwenzi,ndugu, jamaa rafiki.

Kila mtu anahusika kwa nafasi yake, usiweke jukumu la kumtibu mgonjwa kwa serikali ama wahudumu wa afya pekee,
 
Ukichunguza vizuri, hakuna mke wa mbunge wala waziri anajifungulia kwenye hizo hospitali mnazoambiwa ni bure.

Hii iwape taswira kuwa wanachokisema hawakimaanishi na mnachotumia wao hawaoni viwango stahiki kwenye huduma za hizo hospitali.
 
Sera ni independent of mtunga sera. Mtunga sera awepo au asiwepo, sera lazima ifuatwe kama bado haijafanyiwa marekebisho!
Sasa unaifataje sera kama vitendea kazi havipo
Mtunga sera hajaleta vitendea KAZI
Mtu amekuja hana gloves inabid akanunue
Au unataka huyo NES atoe pesa zake akununulie
 
Sasa unaifataje sera kama vitendea kazi havipo
Mtunga sera hajaleta vitendea KAZI
Mtu amekuja hana gloves inabid akanunue
Au unataka huyo NES atoe pesa zake akununulie
Gosh! Mmiliki wa hivyo vituo wa afya si ni Serikali? Yaani Serikali haipeleki PPE (gloves, etc) kwenye vituo vyake vya afya? Kama ni kweli, basi tuna tatizo kubwa kupita kiasi.

Medical professionals wawapo kazini ni sawa na askari walio kwenye battlefield. Kumpeleka medical professional kazini bila PPE ni sawa na kumpeleka askari kwenye battlefield bila combat gear (helmet, boots, camouflage, etc). Hili linawezekanaje?
 
Acha ujinga mkuu, hivi wewe unaona ni sawa mjamzito kulipia huduma ya uzazi? Tena ilipaswa mama akijifungua apewe na package ya pesa kwa ajili ya lishe ya mzazi na mtoto.
Hili liliwezekana kwenye DEVELOPED COUNTRIES.

SISI NI DEVELOPING COUNTRIES zingatia hili mkuu ☺️ 😊 mimba/ ujauzito sio dharula...

Pain story
Kuna siku miaka kadhaa imepita tuliamua kutoka kwenda kisinia hapo shishi food mwananyamala/ kijitonyama.
Mshikaji wetu mmoja mke wake alikua MJAMZITO na alikua yupo hapo hospital mwananyamala so alipata changamoto ya kujifungua mtoto kutokana na hiyo mtoto akawekwa kwenye uangalizi maalum na few hours later mtoto akafarik.

Mmoja wetu akaambiwa so akatutonya tukasema tusimwambie mpaka tushibe tumalize kula chakula..hata hatuku maliza chakula jamaa akaambiwa mtoto amefariki na mke kafanyiwa operation

Mke wangu akapata ujauzito best angu huyu alie fiwa na mtoto akaniambia nilifanya ubahili ndio maana yakanikuta ningetoa cash yasinge mkuta..hapo ndipo nikaanda maandalizi mazuri ya mke wangu kujifungua

Wanaume wenzangu kuepuka matatizo Kama haya ni kujiandaa mapema pia tuchangie huduma za afya hata posho pia kwa wakunga za kubrashia viatu inapo bidi
 
Acha porojo wewe, unajua wananchi ndo wanajenga vituo, kulipa mishaara ya watumishi kupitia kodi zao ? Hii agenda njoo nayo taratibu , watz sio mazwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…