Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Mwaka 1992 Tanzania ilitangaza kuwa ni nchi ya vyama vingi. 2020 bado kuna viongozi wanao simama majukwaani na kusema mkichagua upinzani hatuleti maendeleo.
Sifa kubwa ya kiongozi ni kuweza kuwaongoza wale anao wajibika nao kisheria katika mamlaka yake. Kiongozi anaefuata kanuni za haki bila kupendelea wa kabila lake, wa dini yake au wa chama chake. Ataweka imani yake kwa anaowaongoza na wata msaidia kukitokea matatizo kwakua anasimamia haki.
Kama wazazi tunashauriwa kuwapeleka watoto shuleni hata kama una uwezo wa kukodi mwalimu wa kuwafundisha watoto wako nyumbani. Shuleni mtoto anaanza kujifunza kuishi na watu wengine mbali na wale anaotoka nao nyumba moja. Mtoto ataanza kutunza vifaa vyake visiibiwe, kuwahi dawati kama hayatoshi kwakua hapa mama wala baba hayupo kukuita ukae kwenye kiti chako.
Chama kitakachounda serikali baada ya uchaguzi kiwe na lengo la kutuletea maendeleo katika haki bila kutubagua.