Suzy Elias
JF-Expert Member
- Nov 9, 2021
- 1,067
- 6,200
Kwa nilichokishuhudia uwanja wa Taifa ni aibu kwa mamlaka za mpira wa miguu hapa Tanzania.
Kundi kubwa la mashabiki waliosemekana ni wa Yanga walishangalia bila aibu goli/ushindi wa timu ya Taifa ya Uganda huku wakisema "acha mwana majivuno Karia apigwe ili aendelee kuwafungua wana michezo wa kweli."
Wengine wakadai " haya Karia kawafungie na Uganda kushiriki mashindano kwa kuwafunga Taifa Stars."
Hakika nukuu hizo hapo juu ni wazi zinasadifu chuki kubwa iliyopo kwa baadhi ya mashabiki wa mpira wa miguu hapa nchini.
Mpasuko huo unaojionyesha bayana hakika si wa kupuuzwa hata kidogo!
Ni wajibu wa mamlaka za nchi kumkemea Karia aache maneno yake ya nyondo na uonevu kama upo kwa mashabiki wa timu zingine hapa nchini.
Mpasuko kwenye jambo lihusulo maslahi mapana ya nchi hakika si wa kupuuzwa hata kidogo.
Mungu ibariki Tanzania.