Wanasiasa mkemeeni Karia wa TFF, amesababisha mpasuko mkubwa mno kwenye timu yetu ya taifa

Wanasiasa mkemeeni Karia wa TFF, amesababisha mpasuko mkubwa mno kwenye timu yetu ya taifa

Kwa nilichokishuhudia uwanja wa Taifa ni aibu kwa mamlaka za mpira wa miguu hapa Tanzania.

Kundi kubwa la mashabiki waliosemekana ni wa Yanga walishangalia bila aibu goli/ushindi wa timu ya Taifa ya Uganda huku wakisema "acha mwana majivuno Karia apigwe ili aendelee kuwafungua wana michezo wa kweli."

Wengine wakadai " haya Karia kawafungie na Uganda kushiriki mashindano kwa kuwafunga Taifa Stars."

Hakika nukuu hizo hapo juu ni wazi zinasadifu chuki kubwa iliyopo kwa baadhi ya mashabiki wa mpira wa miguu hapa nchini.

Mpasuko huo unaojionyesha bayana hakika si wa kupuuzwa hata kidogo!

Ni wajibu wa mamlaka za nchi kumkemea Karia aache maneno yake ya nyondo na uonevu kama upo kwa mashabiki wa timu zingine hapa nchini.

Mpasuko kwenye jambo lihusulo maslahi mapana ya nchi hakika si wa kupuuzwa hata kidogo.

Mungu ibariki Tanzania.

Mimi hata sijakuelewa...

Mkubwa, kwani kila mtu anamjua huyo Karia wa TFF? Na TFF ni kitu gani kwani...?

Hebu eleza, Karia ni nani? Ni kwa namna gani na kwa sababu zipi kasababisha huo mpasuko huko TFF..?

Unataka au unashauri afanywe nini na nani...?
 
Kwa nilichokishuhudia uwanja wa Taifa ni aibu kwa mamlaka za mpira wa miguu hapa Tanzania.

Kundi kubwa la mashabiki waliosemekana ni wa Yanga walishangalia bila aibu goli/ushindi wa timu ya Taifa ya Uganda huku wakisema "acha mwana majivuno Karia apigwe ili aendelee kuwafungua wana michezo wa kweli."

Wengine wakadai " haya Karia kawafungie na Uganda kushiriki mashindano kwa kuwafunga Taifa Stars."

Hakika nukuu hizo hapo juu ni wazi zinasadifu chuki kubwa iliyopo kwa baadhi ya mashabiki wa mpira wa miguu hapa nchini.

Mpasuko huo unaojionyesha bayana hakika si wa kupuuzwa hata kidogo!

Ni wajibu wa mamlaka za nchi kumkemea Karia aache maneno yake ya nyondo na uonevu kama upo kwa mashabiki wa timu zingine hapa nchini.

Mpasuko kwenye jambo lihusulo maslahi mapana ya nchi hakika si wa kupuuzwa hata kidogo.

Mungu ibariki Tanzania.
Acha utapeli. Mambo ya kujinukuu hayana maana.
 
Ni kweli kabisa ndugu, yaani ushindi wa simba na yanga naufananisha kabisa na ushindi wa CCM, mwingi unapatikana kwa hila kuliko uwezo. Siku timu za Simba na Yanga zinaingia kwenye ushindani wa kweli ndio soka letu litaboreka.
Nchi hii hakuna Moira Kuna upuuzi tu wa midomoni basi
 
Wala Karia hahusiki,siku mkija kuacha upumbavu wenu wa Simba na Yanga ndio mtakuja kuendelea..

Ligi inaendeshwa Kwa matakwa ya Simba na Yanga ,timu zingine zinaonewa nk ndio maana Huwa siangaliagi mpira wa Bongo hata siku moja..

Safi Sana Uganda kawanyoeni na kule
Well said mkuu. Eti mleta mada analeta upuuzi wa Simba na Yanga jukwaani na kutuaminisha kuwa taifa Stars imeshindwa kwasabb ya Karia. Ujinga mtupu.

Hakuna mpira nchi hii. Kuna upumbavu tu wa midaomoni
 
lakini timu ngeni zikija hapa, hakuna hujuma ili timu zetu zifuzu, kwani TFF huwa inaogopa nini
Angalia mjinga mwingine huyu hapa. Aliyekuambia kazi ya vyama vya mpira ni kufanya hujuma kwa timu toka nje ya nchi ni Nani? Ujinga huu mtauacha lini enyi wapumbavu?
 
Tanzania Football Failure TFF
Hili shirikisho ni upumbav mtupu, imejaa vilaza tupu... Karai sijui karia ni useless ni hopeless... TFF imefeli mazima haina mikakati thabiti ya kuinua mpira wa Tz...
 
Tangu akili kukomaa, nimeona vipindi vitatu vya uongozi wa TFF: enzi za Ndolanga, Tenga, na sasa Karia.

Kwa maoni yangu, TFF ya Tenga ilikuwa sirias katika kukuza soka Tanzania.

Kwenu wakongwe!
 
MANARA AMEWASHIKIA AKILI MASHABIKI WENGI WA YANGA.

UGOMVI BINAFSI WA MANARA NA KARIA AU BABRA AU DEWJI UNAGEUZWA KUWA WA YANGA NZIMA.

HUO NI UPUMBAVU!
 
Tangu akili kukomaa, nimeona vipindi vitatu vya uongozi wa TFF: enzi za Ndolanga, Tenga, na sasa Karia.

Kwa maoni yangu, TFF ya Tenga ilikuwa sirias katika kukuza soka Tanzania.

Kwenu wakongwe!
USICHOKIJUA LIGI YA SASA TANZANIA NDIO LIGI BORA EAST AFRICA.

KARIA ANA MAPUNGUFU YAKE ILA TUWEKE PEMBENI USIMBA NA UYANGA!
 
Back
Top Bottom