Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Wakuu,
Jana nilikuwa naangalia takwimu za Watanzania ambao wana matatizo ya moyo kitaalamu Cardiovascular Disease (CVD)
Kulingana na report kutoka kwenye tovuti ya Geospatial Health, 13% ya watanzania wana matatizo ya moyo yaani kitaalamu CVD.
Hii ikanipa kihali hasa katika kipindi hiki ambacho Tanzania ipo kwenye vuguvugu la Uchaguzi.
Kampeni za wanasiasa kutoka Tanzania zimejaa makelele mengi sana.
Unakuta umelala usiku na familia yako, gari la matangazo linapita bila kujali kuwa ni muda wa wa kupumzika ni matangazo tu ya kuwa mchague fulani au chague chama fulani.
Soma pia:
Au kwenye sehemu za public kama sokoni, barabarani kuna muda hata kwenye makazi ya watu, unakuta wanasiasa wanafanya kampeni kwa kutumia Maspika yanayotakiwa kufungwa kwenye sherehe, kwenye majumba ya watu.
Kelele zinakuwa nyingi na husababisha karaha na sometimes kama ni tabia endelevu hupelekea watu kupata magonjwa ya moyo, presha na athari zinazoendana na hizo.
Soma pia:
Na hii si katika kipindi cha uchaguzi tu . Hata baada ya uchaguzi, zile shamrashamra za wagombea walioshinda ikiwemo kupiga baruti, kupiga yowe na kupiga honi za magari na boda huleta usumbufu na athari nyingine za kiafya kwa watu.
Nashauri Wizara ya Muungano na Mazingira ambayo ipo chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Baraza La Taifa La Hifadhi Na Usimamizi Wa Mazingira (NEMC) pamoja na TAMISEMI wakakaa chini na kutunga sheria za kuweza kuzuia makelele na uchafuzi wa hali ya utulivu katika kipindi cha uchaguzi kwa vyama vyote