DOKEZO Wanasiasa na mipango ovu ya kuiua eGA

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Huu mchakato umepamba moto, Juzi juzi hapa nimesoma makala moja kutoka katika gazeti la The Citizen mwandishi inaonekana kabisa ana nia ovu kwani aliyoyaandika hayana ukweli hata kidogo nikabaki najiuliza lengo lake ni nini haswa.?? Mama Samia ukizama ukizama kwenye huu mtego laana hii haitokuacha. Mimi nasema mmoja kati ya wanasiasa hao ana ushirika wa karibu sana na ma Boss wa iliyokua Kampuni ya Six telecom[waziri mwenye kipara], enzi za Six telecoms alishirikiana na maboss hao kukwepa kodi ya kulipia masafa ya Simu za kimataifa na aliwaziba mdomo TCRA mpaka pale Jiwe Chuma Hayati JPM alipoingia madarakani na kuwanyorosha hao wahuni wa Six telecom. Toshekeni na pesa mlizoibia taifa hili mwisho wenu utakuwa mbaya sana.
Nape nnauye tafuteni mwandishi wa makala hii yenye lengo la kufifisha juhudi za Serikali katika maendeleo ya TEHAMA aseme au aweke ushahidi wa aliyoyaandika.
 
umeongea point kadhaa za muhimu ,lakini ushauri wa kwamba E-GA waachane na utengenezaji wa mifumo sijakuelewa kabisa , ili aachiwe nan? kwa maslah ya nan? Utengenezaji wa mifumo sio usimamizi wa mifumo , mifumo ni ya serikal , E-GA hatengenezi mifumo ya kutumika Vodacom wala NMB , anatengeneza mifumo ya kutumika serikalini
ukisema E-GA aachane na hio kaz unataka vijana wabaki kuwa ma project manager na ma system admins
unaua vipaji na unaingiza taifa kwenye utegemezi wa mifumo inayobeba siri kubwa za nchi
mfano mailing system ikamatwe na mmarekani ,RAIS akituma mail yeyote wanaona
HRMS ikamatwe na mrusi, siri za nchi zote ziko hadharani, japokua mtakua mmepata 10% lakin y?
 
Uko sahihi. kuwe na mkakati wa ku transfer technology. Kama TRA wanavyofanya..kufanya kazi na wakorea ni jambo zuri.

Mifumo na hata tovuti zinazojengwa na eGA ni za kiwango cha chini sana.
wewe ndugu yangu , sidhan kama unajua hii kitu vizuri , TRA wakorea wamewaleta lini? si mwaka huu ? wametransfer knowledge lini? Tena hao TRA wameleta wakorea kutengeneza Single window mfumo ambao tayar upo na uko operational ? Mmemdanganya Rais kwamba hakuna mfumo ambao ni single window ambao TRA na TPA wanaweza tumia wakati mfumo upo. TRA and TPA guys are just fraudulents mnawadanganya viongozi waandamizi ili mpige 10%
Vina muda basi , subirini
 
Kuna mkakati uko funded kuchafua na kufanya character assasination ya mifumo ya serikali linajulikana hilo THE CITIZEN wanajulikana nan anawatumia
 
Kuna mkakati uko funded kuchafua na kufanya character assasination ya mifumo ya serikali linajulikana hilo THE CITIZEN wanajulikana nan anawatumia
Hatari sana. Kwa mfano jamaa anasema This is where you have, for example, different water authorities deploying different systems to do the same thing. wakati inafahamika mamlaka imetengeneza mfumo mmoja tu unaotumiwa na mamlaka za maji tofauti na hapo awali ambapo kila mamlaka ilikua inajinunulia mfumo wake. Serikali tuilaumu kwa mambo mengine ila hapa kwenye tehama inafanya vizuri.
 
hawa watu wamenuia kufanya uovu , hawatatulia mpaka either washughulikiwe wote au waishughulikie E-GA , sema cha moto wameanza kukipata
 
BInafsi yangu kwenye hili la eGA niko tayari kuwa Mujahideen, nitaufikisha ujumbe kwa Rais kwa namna yoyote ile.
Kuna watu waliamini baada ya JPM kuondoka wangeweza kufanya mambo yao ya hovyo kirahisi sana , lakini i can assure them , they have a very high mountain to climb , game lao limefuchuka sasa wanahaha kutie in viongozi wakubwa
 
Watanzania tulivyo wa ovyo nyuzi kama hizi wachangiaji wanasuasua ila uzi Kawa wa ashura ungekuta mpaka leo page ya 1000 na. Kiukweli hawa wahuni wa nchi hii tunawamezea mate wakiingia kwenye kumi na nane ndiyo watajua kama nchi ya viumbe wanaitwa watanzania. Ila wache tu watuone sisi mazombie
 
Mmmh wacha wale BATA
 
kuna magenge yameshakata vitaru kwenye sekta za ICT ,yanaona kama ni halali kubinafsisha ICT industry , ukiwakuta mzee wanapanga mikakati kama zimo kumbe majivu tupu
 
Hawa wezi natamani hata kuwatandika risasi, mfumo wa Single window upo ila wanaleta wakorea kisa 10% same applies kwa makamba kaleta erms ya wahindi wakati Erms tayari ipo, bashe kaleta mfumo wake wa kilimo wakati tayari mfumo upo, hii nchi hii kama kweli Mungu yupo mafisadi ya taifa hili yataangamizwa.
 
comrade, wanasiasa wakishatimiziwa au kuhakikishiwa matakwa yao ambayo ni mawili tu ,
1. Watarudi kwenye nafasi zao
2.Mifuko yao na matumbo yao yako salama watafanya lolote

Just few days ago, ofisi moja nyeti sana maada hii walikua wanaiongelea na vijana kadhaa wakawa asigned wakafanye upekuzi maalumu kwa wahusika wanaotajwa kusuka hii mipango , vijana wameanza kuleta feedbacks kumbe mmoja wa watu muhimu sana ambaye ni waziri kiungo naye ni mhusika . Jambo linakua more complicated na wanavuana nguo kisiasa as we speak .
Ni aibu aibu aibu sana.
Tuna mawaziri wanaoshirikiana na magenge ya wahalifu serikalini kutaka kuua taasisi ili waanzishe mchakato wa kubinafsisha taasisi ya umma.
Ni aibu kubwa sana , wewe kiongozi wa TEHAMA uliyepo Wizara ya fedha na mipango hufai kuwa ofisini, wewe uliyepo TAMISEMI hufai , palapala hufai na genge la wenzako , jueni tanzania imewafahamu na there is no escape
 
Ni rushwa na ufisaidi kila mahali watu wanampigisha shot raisi , wanataka wapige alaumiwe Rais . Mimi nawaasa wasaidizi wa rais waangalie weledi wa baadhi ya mawaziri na viongozi waandamizi wa TEHAMA nchini ,wanauza nchi kama wazee wetu kadhaa walivyouza nchi yetu upande wa sekta ya madini kwa kuingia mikataba ya miaka 99 .
wazalendo limebaki jina la kuchukulia kura lakini wameoza na matumbo yako yamevunda
 
Nashukuru watu mmeanza kufunguka .
Nchi upande wa TEHAMA imesha elekea kibra inasubiri kisu.
Wahusika wanahonga pesa magazeti waongelee vibaya mifumo ya serikali kweli? TISS do this once and for all mheshimishe taifa
 
Katika hili nitahakikisha ujumbe unamfikia Rais mama Samia, uamuzi utakua wake ila maamuzi yoyote mabaya yatakisulubu kizazi chake chote
 
Katika hili nitahakikisha ujumbe unamfikia Rais mama Samia, uamuzi utakua wake ila maamuzi yoyote mabaya yatakisulubu kizazi chake chote
Mhe Rais niwakufikishia ujumbe , ili asiwe na hatia kwenye damu zitakazomwagwa zisizo na hatia.
Future ya nchi kwenye TEHAMA ipo mikono salama EGA pale lakini kuna hao watu wanaisakama utadhani E-GA imewachukulia Wake zao
 
Mhe Rais niwakufikishia ujumbe , ili asiwe na hatia kwenye damu zitakazomwagwa zisizo na hatia.
Future ya nchi kwenye TEHAMA ipo mikono salama EGA pale lakini kuna hao watu wanaisakama utadhani E-GA imewachukulia Wake zao
EGA inasakamwa ka sababu imeondoa uhuni wa mabepari fulani hususani Maxmalipo. Inasikitisha sana. Nitafanya juhudi binafsi kuilinda taasisi hii, ninafahamu tulipotoka na wanufaika wa mfumo tuliotoka kabla ya eGA
 
EGA inasakamwa ka sababu imeondoa uhuni wa mabepari fulani hususani Maxmalipo. Inasikitisha sana. Nitafanya juhudi binafsi kuilinda taasisi hii, ninafahamu tulipotoka na wanufaika wa mfumo tuliotoka kabla ya eGA
Maisha ya kutumikia familia zao badala ya viapo vyao hayapaswi kuvumiliwa , watu wameshika madaraka kwa viatu vya uadilifu lakini kumbe waliapa kutumikia matumbo yao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…