DOKEZO Wanasiasa na mipango ovu ya kuiua eGA

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mtaalam.hiv hio mifumo muse ni kitu gan. ? Ina tofaut ipi na cheque
 
unaona mwanasiasa anatamka maneno ambayo maskini hata hayajui , amemezeshwa na waliomtuma , anahangaika kutamka neno hata Digitalization , unaona kabisa hapa kuna mchoro

Hadi sasa vijana wadogo wa kitanzania wameweza kuunda mifumo ambayo imeendelea ku-off set ile ya wakoloni ambayo ililetwa kwa maslahi ya wachache;

Mfano sasa mfumo wa kumanage rasilimali watu ni ya kutengenezwa na wazawa nadhani tangu 2021, mfumo wa manunuzi nao umeshaanza kuondolewa kwa baadhi ya taasisi na kuwekwa uliotengenezwa na wazawa.

Jitihada hizi za kuendelea kuja na mifumo mingine ndizo hizo zinataka kuangushwa na wachache kwa manufaa yao. Mfano wakati fulani ilitokea fault iliyosababisha mfumo wa ununuzi wa LUKU kutofanya kazi for almost 3 days Waziri Mkuu aliingilia kati na kuamuru kuundwa timu ya watalaam kutoka taasisi mbalinbali ikihusisha eGA, TANESCO, wizara ya fedha, nishati.

Lakini sasa ni zaidi ya miaka 2 hakuna lolote na kimsingi ilikuwa ni issue ya kuwepo na backup system ili ikitokea ile ya wa South Africa ambayo ndiyo vendor wa huo mfumo ambao is like kama tulikodi maana hata server zilikuwa kwao, maajabu kbs na waziri mkuu nae akawa anashangaa kama sisi raia..... bad enuf siku chache watu wakatunukiwa hiyo wizara ya nishati!!
 
Mimi naunga mkono hoja yako lakini kwa complex organisms kama tanesco na tra, hakuna namna zaidi ya kununua.

Wataalamu wetu waisome hiyo mifumo ili waweze kuanza kujenga ya taasisi ndogo ndogo kama halmashauri, taasisi za umma ndogo ndogo ili miaka ijayo waweze kuitengeneza.
 
Mtaalam.hiv hio mifumo muse ni kitu gan. ? Ina tofaut ipi na cheque
Mimi pia sio najua ila nimepita thru maandiko mbalimbali hasa kusoma jornals; MUSE-Mfumo wa ulipaji Serikalini, ni accounting package iliyobuniwa na watalaam wa ndani kwa ajili ya circle nzima ya malipo serikalini katika module za payable, recevable na purchasing. Imepunguza paper work including checks kwa kuwa ina option ya direct transfer to payee account na ndio maana mlipwaji unatakiwa kuwasilisha taarifa zako za kibenki kwa mlipaji.....
 
Mimi naunga mkono hoja yako lakini kwa complex organisms kama tanesco na tra, hakuna namna zaidi ya kununua.
Ununuzi unaohusisha mikataba kwetu ni tatizo mkuu wangu, maana mifumo mingi ambayo ime run huko nyuma ikiwa na element za kuinunua si kwamba mnapewa full ownership ya hiyo mifumo, badala yake mnakuwa kama mmeikodi na server za mifumo wakati mwingine zinakuwa kwao au la contract inawataka muajiri mtu wao au wawe wanatoa technical support kwa malipo ya ziada siku zote za operation ya mfumo. Updates zote unatakiwa ulipie licences ambazo nyingi ni renewables na ni kwa malipo. Ni kama mtu anapanda shamba anajivunia kila akihitaji!!
 
Nchi hii inahitaji watu watakaothubutu kuwa expose namna hii wakoloni weusi wanao angalia matumbo yao pekee, vizazi vijavyo vitarithi nini kwa madudu kama haya? Maxence Melo tusaidie kupaza sauti , umepigana vita nyingi sana , na umeshinda , wasaidie wadogo zako , kizazi hiki kitakukumbuka sana , platform yako inasaidia sana lakini pia investigative journalism inahitajika kuibua mapapa wala watu serikalini
 
huyu waziri wa minoti atatumaliza aisee
 
Najaribu kukuelewa , lakini mfano mfumo wa kumanage human ressource TRA ana functions tofauti na Bandari?
Kuna generic systems ambazo zina same features kama mfumo wa HR, sasa inatatanisha kidogo ,ukiona TRA makusudi kabisa anaamua kununua solution ambayo ni simple na inatumika maeneo mengine bila shida kabisa.
 

Kama ni kweli, maana inaweza kuwa ni tetesi au uzushi, nchi yetu, shida ni nini? Mbona kila kitu chema kinapigwa vita? Mambo mabaya mabaya ndio yanapewa platform kama vile hatujali kesho yetu itakuwaje?

Inasikitisha sana. Muomba Mungu hachoki. Ipo siku Mwenyezi Mungu atanyoosha mkono wake atutendee haki. Haiwezekani kabisa wachache waharibu na kama vile haki haipo, waendelee kupeta. CAG na ripoti yake ni mfano halisi
 
Kiongozi , nilichokisema Maxence Melo ni mwandishi mzuri wa habari , anaweza kufanya uchunguzi wake , ni jambo ambalo liko wazi kabisa , wanasiasa kadhaa wanaplot hio move na sio kwa siri , nisingesema mambo ya ramli hapa
 
Huu uzi ni mzuri sana kufahamisha watanzania kinachoendelea,cha ajabu TISS wanakenua tu meno,
Lingine hapa jukwaani wamejaa chawa wa hao wanataka kuua huo mfumo,ndio maana uzi wako hauna wachangiaji,
Mkuu unakijua kichwa cha mwendawazimu?...mfano mzuri ni nchi yako sasa...tafakari....!!!!
 
kuna wajinga kadhaa ,familia zao zikishakua covered wengine hata mkikosa kazi haiwahusu .
Wanatengeneza makampuni binafsi , wanayapa tender pesa wanavuta wao kwa migongo ya kampuni binafsi ambazo ni zao
Hii ni laana na ipo siku itaondoka na mtu. Kuna mambo yanastaajabisha sana. Lengo lake ni nini?
 
Hii ni laana na ipo siku itaondoka na mtu. Kuna mambo yanastaajabisha sana. Lengo lake ni nini?
Ni uhuni uliopitiliza , watu kama hawa wakifumbiwa macho wanaozesha regime nzima , ukiangalia machafuko mengi ya nchi zinazotuzunguka hua ni migogoro midogo midogo ambayo hua inapuuzwa mwanzo .
 
out of respect , ni washenzi sana wanaofanya hio mipango kama ni kweli.
ili iweje sasa , they should atleast leave it for poor kids wafanye tech issues.
E-GA ndio sehemu pekee ambapo ukiajiriwa unaenda kufanya kazi kweli , hakuna watoto wa wakubwa pale , hio mifumo ikitengenezwa nje ya nchi sas si tuna expose siri za nchi nje au ndo tumeamua kuuza nchi
 
sijasema Raisi kuna mambo hajui , ninachosema ni kuwa rais anaweza kupotoshwa , akapewa ukweli usio ukweli , na hapo ndipo ninasema rais anakua hajui .
Mfano watu wamdanganye rais afute E-GA wampe sababu za uongo huwezi sema rais ana husika
Mkuu huwezi mdanganya rais kiivo. Kwanza TISS watakua wamelala wapi mpaka waruhusu ujuha kama huo? Ukiona issue kama hizo zinafanyika jua rais lazima ajue.
 
Ni mjinga tu ndio ataamini hivyo! Kuanzia private sector zetu mpaka vyuo vikuu kuwe hamna mtu mwenye uwezo huo? Si kweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…