DOKEZO Wanasiasa na mipango ovu ya kuiua eGA

DOKEZO Wanasiasa na mipango ovu ya kuiua eGA

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
E-GA ni taasisi inayoratibu serikali mtandao, ni taasisi ambayo inajenga mifumo karibu mingi sana inayotumika na serikali.

Serikali imeokoa pesa nyingi sana kutoka nje ya nchi na imetoa ajira kwa wazawa. Zaidi sana taarifa na usiri ama unyeti wa taarifa za serikali umeongezeka baada ya mifumo ya ndani kuanza kutumia

Nini kinaendelea kwa sasa?
wanasiasa kadhaa ambao sitawataja leo wanaratibu mpango wa kuiua E-GA ili mifumo ya serikali ianze kutengenezwa nje /ku out source kwa jina la kiluguru.

Je hawa wanasiasa wananufaikaje?
wanasiasa hawa wamesha weka hisa zao kwenye kampuni kadhaa ndani na nje ya nchi ambazo wakisha iua EGA , watazipa kandarasi hizo kampuni ambazo nyuma ya pazia ni zao , wanakuja kwa mgongo wa sekta binafsi lakini ukweli sio sekta binafsi , ni matumbo binafsi.

Mpaka sasa wamefanikiwa kuwang'oa E-GA TRA , tayari TRA anakamilisha ununuzi wa mfumo kwa zaidi ya Bilion 12 za kitanzania(TZS).

Mfumo mwingine TANESCO upo njiani.

Hali ni mbaya sana, wanamtafuta Mkurugenzi wa E-GA ikibidi auawe maana anakwamisha madili

************************* UPDATES********************
Taarifa Mpya tulizozipata zinaeleza juu ya uhusika ya Viongozi waandamizi toka taasisi mbalimbali za serikali na wanasiasa kadhaa kusuka mpango huu wa kuifuta E-GA . Script iko kama hapa chini.

1.E-GA iwe moved from ofisi ya rais utumishi kwenda Wizara ya TEHAMA chini ya Waziri Nape Nnauye.
2. Ikishafika wizara ya TEHAMA , haraka haraka mswaada wa kuninafsisha mashirika na taasisi kadhaa za umma utapitishwa , na moja ya taasisi za kubinafsishwa itakua ni E-GA.

3. Wakisha kubaliana bungeni, E-GA itachukuliwa rasmi na kikundi flani ambacho kitakua kimetegesha Kampuni flani kuimeza E-GA.

4. Watumishi waliopo E-GA baadhi watasambazwa kwenye taasisi mbali mbali wengine watabaki kwenye hio kampuni binafsi , kama ilivyo kwa AIRTEL ambapo serikali ina share kadhaa.


Rai yangu: Waziri Nape Nnauye huu ni mtego unategewa , ng'amuka mapema , unaangushiwa jumba bovu .
NOTE: Majina ya wahusika yapo tayari , hayatakua shared hapa kulinda policy za platform hii.
Mkuu ulisema uzi huu umefutwa....

Ikawaje?
 
Nina kijana wangu ambaye ametoka kwenye kiuno changu aliyebobea kwenye kuunda mifumo ya kielekroniki, ameniambia kuna watu wanategemea kupata 10% ndio hao wanaocheza na mifumo ili ionekane haifai kisha deals wapewe watu wao.
I know vijana wachache pale very talented, actually i can say those few guys ni genius sana , sio wote lakin kuna vijana ega wana brain nzuri sana . Serikali ikipatazama vizuri badala ya kupavuruga , hio itakua silcon valley yetu .

Maisha ya kuangalia maslahi binafsi yakupinga kabisa .
Tuwe wazalendo ,tukuze vipaji vyetu , watoto wetu wasiishie kuja kuwa watazamaji wa mifumo ikitengenezwa na kuuzwa nchini.
 
I know vijana wachache pale very talented, actually i can say those few guys ni genius sana , sio wote lakin kuna vijana ega wana brain nzuri sana . Serikali ikipatazama vizuri badala ya kupavuruga , hio itakua silcon valley yetu .

Maisha ya kuangalia maslahi binafsi yakupinga kabisa .
Tuwe wazalendo ,tukuze vipaji vyetu , watoto wetu wasiishie kuja kuwa watazamaji wa mifumo ikitengenezwa na kuuzwa nchini.
Kuna mtu yupo PPRA pale ni zao la EGA lakini anabomoa E-GA utadhani imemchukulia mke wake , jamaa ananunua hadi vijana wa E-GA kadhaa ili waihujumu E-GA , unaambiwa jamaa ameunda gang ya maana hatari , wameona kuiua kawaida hawawezi sasa wananunua vijana kwa pesa ili vijana wasifanye majukumu yao ya msingi wawe wanawazungusha kwenye vikao mbali mbali washindwe kufanya kazi .
Sema Mushir** ni hatari sana .
 
Kuna mtu yupo PPRA pale ni zao la EGA lakini anabomoa E-GA utadhani imemchukulia mke wake , jamaa ananunua hadi vijana wa E-GA kadhaa ili waihujumu E-GA , unaambiwa jamaa ameunda gang ya maana hatari , wameona kuiua kawaida hawawezi sasa wananunua vijana kwa pesa ili vijana wasifanye majukumu yao ya msingi wawe wanawazungusha kwenye vikao mbali mbali washindwe kufanya kazi .
Sema Mushir** ni hatari sana .
Shit....

Rais achukue hatua haraka sana E-GA watu watapeana sumu.

Awamu ya Rais Magufuli kuna ushenzi kama huu uliibuka , Rais Magufuli aliamuru department nzima kuhamishwa, huyo mushiro alihamishwa na department yake yote , kuanzia mkurugenzi wa idara hadi ofisa wa ngazi ya mwisho , maana sumu ilikua imesambaa idara nzima; jamaa akawa benchi kwa muda.

Amepenya sasa yupo PPRA kama mkurugenzi wa … pale , amejoin gang na wenzake sasa they are back for revenge Mungu wangu.

Hivi tuna usalama wa Taifa active kweli nchi hii? yaan maafisa usalama mmesinzia kabisa mnasubiri vijana wapigwe sumu muandike Rest in peace au sio?

Idara ya usalama wa Taifa hamna msaada and you have no idea na kinachoendelea .

Mmesinzia usingizi mnahitaji kuamshwa na mijeredi ya moto , subirin waue vijana wa E-GA mtaelewa nyie endeleeni kula shisha
 
na kuna mbunge juzi anasimama kumtetea kijanammoja eti ana akili sana , moyo uliwaka kwa hasira , kijana anayetetewa ana miliki kampuni ambayo kawekwa na wanasiasa, anapiga pesa anawapa mabwana zake wana siasa ni aibu kubwa sana na wanasiasa wanajua mpaka wamefungua tawi Dubai , ni genge la kihalifu lipo serikalini linaendelea na kazi wengine ni viongozi wakubwa sana
Wanamwita Serial Entreprenuer, Tech Mogul 😂😂
 
Hapo ndio unapofeli, hakuna mfumo complex, na Tanzania hii tuna watu lukuki wa kuweza kufanya hii mifumo

Unachotakiwa kuelewa ni kuwa, mfumo haui imara ndani ya siku moja, hata wao wanaoleta mifumo nchini hawakutengeneza ndani ya siku moja, it took them years mpaka wakafika point na kukubali mifumo yao iko stable kutumiwa na nchi zingine

Kwa hiyo na sisi tukiwapa muda wataalam wetu, with time mfumo utakua stable na tutaweza hata kuuza nchi zingine

Tatizo letu kila mwanasiasa akishika nafasi anataka kuja na kitu chake wakiangalia matumbo bila kujali ubora wa kitu anachokikuta.
Kwa hapa tulipofika nadhani ni serikali kufanya maamuzi ya kugharamia kuwapeleka vijana wa kitanzania ambao ni IT kwenye vyuo vyenye ubora huko nje tunakoamini kwamba wako mbele kidogo ktk sayansi yenye kuhusiana na IT ili wakapate ujuzi ambao utaendena na technologie ya sasa kwenye mifumo

gharama ya kusomesha haitakuwa ghali ukilinganisha na gharama ya kununua mifumo na tena kupitia hao watakaokuwa wamepata elimu basi watakaofanya nao kazini maofisini nao watajifunza hivyo mwisho wa siku tutakuwa tunazalisha wataalamu endelevu kila miaka inaposonga.
 
Wakati Ni Sasa, Awamu Ya Muhari Waitaiuwa Tu Hakuna Namna Yoyote Uongozi Umedorora
 
Rule ya mwanasiasa nikutafuta deal zakumuingizia hela unafikiri hela zakampeni zao 2025 watatoa wapi. ..michongo ndio hii yakutafuta hela ilowachomoke.
Hata kampuni binafsi hii ipo sana kinachowazuia ni uimara wa anaewaongoza kua lazima tubane matumizi nakutumia pale palippnaulazima
 
Kwa hapa tulipofika nadhani ni serikali kufanya maamuzi ya kugharamia kuwapeleka vijana wa kitanzania ambao ni IT kwenye vyuo vyenye ubora huko nje tunakoamini kwamba wako mbele kidogo ktk sayansi yenye kuhusiana na IT ili wakapate ujuzi ambao utaendena na technologie ya sasa kwenye mifumo

gharama ya kusomesha haitakuwa ghali ukilinganisha na gharama ya kununua mifumo na tena kupitia hao watakaokuwa wamepata elimu basi watakaofanya nao kazini maofisini nao watajifunza hivyo mwisho wa siku tutakuwa tunazalisha wataalamu endelevu kila miaka inaposonga.
Wabongo wapo wazuri sn tena mno. ..shida wengi niwatoto wamaskini hawana network yakutosha. .wengine wameachakabisa IT nakwenda kufanya kilimo
 
Hapa naona mnachanganya mambo.

Mtoa mada ametoa dokezo kwamba Ega inaenda kupigwa chini yaani wanatolewa wanarudishwa "wapigaji" ,kuna tofauti ya kununua mifumo kutoka kwa wapigaji na wapigaji kuendesha mifumo baada ya kununua.

Ega kununua mifumo na kuiendesha wao siyo tatizo hata mabenk na taasisi mbalimbali zinanunua mifumo ,hata oracle/window ni mifumo ya nje hatuna OS zetu tulizodevelop sisi watanzania nadhani ushaanza kuelewa nini maana ya mfumo.

Kumbuka zamani malipo ya serikali yalikuwa "manually aka makaratasi" ,JIWE akaanzisha mfumo wa EGA(control number) lengo kwamba malipo yote ya serikali yanaratibiwa hapo hivyo baadhi ya aggregator(3rd parties) wakaondolewa some of them ni MaxMalipo, Selcom .....Hao ndio walikuwa wanapiga pesa before Ega ,kwasasa hayo makampuni yanapumulia mashine hivyo wanasiasa wanafanya lobbying warudishwe hao 3rd parties ili waendelee kupiga pesa.

Wabunge msiturudishe kwa wapigaji ,EGA iendelee kufanya kazi haiwezekani mapato ya serikali yakusanywe na 3rd party(Mtu kati aka dalali).
 
Kwa ujuzi wangu na navyowajua Ega hawana uwezo wa kutengeneza mifumo waliyonunua TRA wala TANESCO hata asilimia 10. Ile ni mifumo mikubwa inayotumika Duniani.

Ega ukiangalia tu website za serikali unaweza kujua ni watu wa uwezo gani halafu wapewe kutengeneza mifumo mikubwa kama ya TRA ama TANESCO kweli?

Sio kila kitu lazima kifanywe na wataalamu wetu wakuu. Vitu vingine viko juu ya wataalamu wetu.
Nini suluhu ya icho unachosema?km kuna mapungufu nadhani serikali itoe ufadhiri kwa vijana wakapikwe ili wawe na uwezo ili mifumo nyeti itengenezwe hapa mkuu
 
Yes RAIS ni taasisi kubwa ana jua ndio maana hata sisi tunasema hapa , lakini haimaanishi ana endorse hio move.
wanasiasa waovu wanapambana kutaka kumruka asijue ujanja wao , lakini bahati nzuri kamba yao imejulikana
Hizi ni story za kujifurahisha tu hana anachoweza kufanya.. watu wemepiga hela CAG amethibitisha umeona kilichofanyika? tuungane tudai Katiba Mpya itakayotuwekea mifumo mipya yakufunga..kufilisi nakufunga wangu ikiwe Rais ikiwa atazingua!
 
Binafsi mama sijaona shida yake ndio maana mpaka naandika hapa mama amewagomea , wanapambana sana wamruke mama anakaza
Ili tumuamini alete mchakato wa Katiba mpya vinginevyo haya yatakuwa ni maneno ya waunga juhudii tu
 
Back
Top Bottom