DOKEZO Wanasiasa na mipango ovu ya kuiua eGA

DOKEZO Wanasiasa na mipango ovu ya kuiua eGA

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Kuna halmashauri sasa hivi zime-outsource kukusanya mapato, imenichekesha Sana. Halmashauri zimeipa kampuni binafsi kukusanya mapato. Fatilia sasa mwenye hiyo kampuni

Bado nawaza raisi, waziri na viongozi wengine wameweza kukubali vipi kitu kama hiki?
Kuna uhuni flani unaendelea , kuna watu wakiwekwa wazi nchi itakua shocked , wana sifa nzuri sana kwenye public lakin ni hovyo sana
 
EGA imeanzishwa 2019, Ila kabla ya hapo kulikua na hiyo wakala wa serikali mtandao. Ni kitu kimoja japo majukumu yalikuja kuboreshwa na kutungiwa Sheria zingine

Serikali mtandao imeanzia mbali kabla hata ya JK, ni toka enzi ya mkapa. Ila kila awamu kulikua na maboresho

Muhimu tuairudi nyuma, badala ya kuidhohofisha EGA, kwa sasa ndio ilipaswa ipewe nguvu zaidi maana teknolojia imekua kwa kasi.
halafu kuna watu wanataka waizime
 
hakuna maajabu kwenye mifumo ya tehama , tunaaminishwa ni migumu ili wapewe watu wa pembeni watu wapige 10% , kimsingi nawachukia sana watu wanaoharibu kesho ya taifa letu
Kinachopaswa kupiganiwa ni watu wafanye kazi bila mashaka ya kesho nchi kuwekwa mifukoni mwa watu kadhaa , Dunia imebadirika digital era hii tuna embrace ubinafsishaji wa mifumo ya serikali
 
Yaan watu wanataka Rais akiandika memo ipite kwenye mfumo wa mtu binafsi tena wa mchongo? we have the most corrupt politicians and senior leaders in some organizations of all time
 
EGA imeanzishwa 2019, Ila kabla ya hapo kulikua na hiyo wakala wa serikali mtandao. Ni kitu kimoja japo majukumu yalikuja kuboreshwa na kutungiwa Sheria zingine

Serikali mtandao imeanzia mbali kabla hata ya JK, ni toka enzi ya mkapa. Ila kila awamu kulikua na maboresho

Muhimu tuairudi nyuma, badala ya kuidhohofisha EGA, kwa sasa ndio ilipaswa ipewe nguvu zaidi maana teknolojia imekua kwa kasi.
The most corrupt elite people on government tech institution wanaendelea kuongoza taasisi Muhimu ambazo zinahusika kwenye decision making, Maxence Melo you can fact check this by verifying Tech leaders wa wizara ya fedha na mipango , checki their credibility kuna mtu wa honyo sana pale utakuja kunishukuru .
Ntakua nakufungulia code kila siku
 
Aisee Rais awe makini sana na baadhi ya watu,TISS imsaidie EGA ni moja ya taasisi bora sana.Alianzisha JK ikaja kuimarishwa JPM wasikubali ipotwwee serikali itapoteza mapato mengi.
 
E-GA ni taasisi inayoratibu serikali mtandao, ni taasisi ambayo inajenga mifumo karibu mingi sana inayotumika na serikali.

Serikali imeokoa pesa nyingi sana kutoka nje ya nchi na imetoa ajira kwa wazawa. Zaidi sana taarifa na usiri ama unyeti wa taarifa za serikali umeongezeka baada ya mifumo ya ndani kuanza kutumia

Nini kinaendelea kwa sasa?
wanasiasa kadhaa ambao sitawataja leo wanaratibu mpango wa kuiua E-GA ili mifumo ya serikali ianze kutengenezwa nje /ku out source kwa jina la kiluguru.

Je hawa wanasiasa wananufaikaje?
wanasiasa hawa wamesha weka hisa zao kwenye kampuni kadhaa ndani na nje ya nchi ambazo wakisha iua EGA , watazipa kandarasi hizo kampuni ambazo nyuma ya pazia ni zao , wanakuja kwa mgongo wa sekta binafsi lakini ukweli sio sekta binafsi , ni matumbo binafsi.

Mpaka sasa wamefanikiwa kuwang'oa E-GA TRA , tayari TRA anakamilisha ununuzi wa mfumo kwa zaidi ya Bilion 12 za kitanzania(TZS).

Mfumo mwingine TANESCO upo njiani.

Hali ni mbaya sana, wanamtafuta Mkurugenzi wa E-GA ikibidi auawe maana anakwamisha madili

************************* UPDATES********************
Taarifa Mpya tulizozipata zinaeleza juu ya uhusika ya Viongozi waandamizi toka taasisi mbalimbali za serikali na wanasiasa kadhaa kusuka mpango huu wa kuifuta E-GA . Script iko kama hapa chini.

1.E-GA iwe moved from ofisi ya rais utumishi kwenda Wizara ya TEHAMA chini ya Waziri Nape Nnauye.
2. Ikishafika wizara ya TEHAMA , haraka haraka mswaada wa kuninafsisha mashirika na taasisi kadhaa za umma utapitishwa , na moja ya taasisi za kubinafsishwa itakua ni E-GA.

3. Wakisha kubaliana bungeni, E-GA itachukuliwa rasmi na kikundi flani ambacho kitakua kimetegesha Kampuni flani kuimeza E-GA.

4. Watumishi waliopo E-GA baadhi watasambazwa kwenye taasisi mbali mbali wengine watabaki kwenye hio kampuni binafsi , kama ilivyo kwa AIRTEL ambapo serikali ina share kadhaa.


Rai yangu: Waziri Nape Nnauye huu ni mtego unategewa , ng'amuka mapema , unaangushiwa jumba bovu .
NOTE: Majina ya wahusika yapo tayari , hayatakua shared hapa kulinda policy za platform hii.
Tiss wanatakiwa kushughulika na makundi ya kiharamia aina hii.
 
Sauti kwanza wajue tumejua/imesikika... then huku tukitafakari hatua za vitendo.
The trap has been set , i don't think kama wata escap , kuna mmoja wao anahangaika na kusumbua hadi PM anajitetea eti watu wana mframe , tunaomba atulie hivyo hivyo syndicate yao imefukuliwa warelax yaan
 
Tiss wanatakiwa kushughulika na makundi ya kiharamia aina hii.
Half classfied intel ni kwamba tayar wako kwenye radar za TISS , no more explaination , nazionea huruma familia zao maana wameziingiza matatani kwa ulafi wao , now let them enjoy the side B of their game
 
Aisee Rais awe makini sana na baadhi ya watu,TISS imsaidie EGA ni moja ya taasisi bora sana.Alianzisha JK ikaja kuimarishwa JPM wasikubali ipotwwee serikali itapoteza mapato mengi.
Nilikua moja ya watu niliokua nashangaa sana kwa nin TISS wamekausha kwenye hili swala ,lakin just for your info ,TISS wameshaifanya priority 1 hii issue , kuna watu soon mtasikia moshi umewafika
 
Hata kama ni kweli, Ila sidhani Kama E-GA is that competent. So isiangaliwe Kama wanasiasa wanataka iua Ila efficiency ndo inatafutwa. Sasa why hatuwezeshi vya ndani Hilo sijui
IT bado ni fani changa. Kuna fani kongwe kama Civil engineering. Hivi umewahi kujiuliza ni kwa ninj hadi leo miradi mikubwa ya barabara na ujenzi wa maghorofa inafanywa na kampuni kutoka nje? Miaka yote hii tumeshindwa kujifunza na kuweza kuendesha hii miradi kupitia makampuni ya Wa Tanzania?

Jibu ni kwamba hatuko strategic. Hatuna mipango madhubuti ya ku transfer technology. Kwa hiyo tutaendelea hivyo hivyo.

Kuhusu swala la eGA wengine waliochangia humu hawajui undani wa Tech na Performance ya eGA.

EGA iliundwa ili iratibu na kusimamia ujenzi na mifumo na miundombinu ya TEHAMA serikalini. Ni kama PPRA wanavyo simamia masuala ya procurement.

Kipindi eGA inaanzishwa taasisi nyingi zilikuwa hoi kimifumo...hivyo walihanasisha na kuanza kutengeneza tovuti na vimifumo vidogo vidogo. Wamefanya kazi nzuri. Lakini tatizo ni kwamba kwa wao kutengeneza mifumo wanakuwa ni marefaree na wachezaji. Kunakuwa na conflict of interest ambayo siku za usoni inaweza kuwa na madhara.

Hivyo inatakiwa eGA waachane na biashara ya ujenzi wa mifumo wajikite kwenye usimamizi wa mifumo.

Huwezi kuwa una jenga mifumo na ku audit mifumo mwenyewe.
 
Kwa chap chap ninavyofikiri,bila kuathiri Sheria za nchi maana sijui taratibu za nchi kuhusiana na usalama wa taarifa zake, nadhani waanze kwa kununua systems/programs duniani then wa customize to fit the need. Then pale watakapokua fit waanze kuzidevelop from scratch. Hii ya ku develop from scratch naona yaweza kuwa shida zaidi.
Mtazamo wangu
Uko sahihi. kuwe na mkakati wa ku transfer technology. Kama TRA wanavyofanya..kufanya kazi na wakorea ni jambo zuri.

Mifumo na hata tovuti zinazojengwa na eGA ni za kiwango cha chini sana.
 
Hii inatokana na udhaifu wa mifumo yetu ya Ulinzi na Usalama. Pia udhaifu wa BUNGE bunge ambalo linapoteza muda na fedha na kuwa rubber stamp kupitisha kila bajeti bila upembuzi.

Udhaifu wa Katiba imetoa madaraka na kinga hata kwa wahalifu na wanaotumia madaraka yao kwa kujinufaisha.

Kama wangekuwa wanashitakiwa, wananyongwa na kufilisiwa mali zilizo nje na ndani upuuzi huu usingekuwepo.

Ova
 
Mimi nikisema wanasiasa ni viumbe hatari, kuna majitu inasema mdini, Tunatakiwa tuogope wanasiasa kuliko hata tunavyoogopeshwa na wakuu wa imani kuhusu dhambi.

Wananchi wanapiga kelele sasa kuhusu eGA lakini hatusikii hata wanasiasa yoyote kuliongelea hili na kwenye jukwaa hili la JF wapo. Kisha litapitishwa bungeni kwakupigia kura nyingi za ndiyo.

Nisiwe mnafiki bila kitu kinachoitwa haki za binadamu ningekuwa natandika viboko kiume yeyote aliye mbele yangu anaye jiita wanasiasa maana hao viumbe ndiyo waliyotufikisha hapa.
 
Back
Top Bottom