Wanasiasa pingeni na pigeni marufuku ufundishwaji wa wanafunzi masuala ya uzazi

Wanasiasa pingeni na pigeni marufuku ufundishwaji wa wanafunzi masuala ya uzazi

Ukisoma vizuri alichoandika mtoa mada kuna kitu cha kujifunza ndani yake.

Hata hivyo masikitiko makubwa ni namna wachangiaji wanavyomvamia kwa matusi na kebehi kana kwamba amefanya kosa la jinai kutoa mawazo yake

Rais Kikwete juzi juzi alitukumbusha kuwa hoja haipigwi nyundo! Hoja hujibiwa kwa hoja bora zaidi

Mtoa mada kwa mtazamo wake anaona hizi elimu za uzazi kwa watoto zinaleta madhara zaidi kuliko faida

Badala ya watu kujibu hili kwa kuonyesha faida, badala yake wamemvamia kwa matusi!

Labda tujiulize vitu vichache kwa ujumla wake kuhusu hii elimu ya uzazi ambayo hadi watoto wa shule ya msingi siku hizi wanafundishwa:

Kabla ya kusambaa kwa elimu hii ya uzazi kwa watoto na sasa ilivyosambaa, ni wakati gani zaidi maadili yamepolomoka?

Kabla ya kusambaa kwa elimu ya uzazi kwa watoto na sasa iliposambaa, ni kipindi gani mabinti wanaonekana kujihusisha na ngono mapema zaidi?

Kabla ya hizi NGOs anazolalamikia mtoa mada ku-promote elimu ya uzazi kwa watoto na sasa, ni kipindi gani kumekuwa na ongezeko la mimba za utotoni zaidi?

Kisha tujiulize kabla ya elimu hii ya uzazi kuanza kuenezwa kwa watoto kupitia NGOs, vyombo vya habari na matamasha mbalimbali na sasa inapohimizwa zaidi, ni kipindi gani watoto wa kike wanaona kufanya ngono ni jambo la kawaida kiasi kwamba hata akigombezwa anaona kama ananyimwa haki yake ya msingi?

Tukijiuliza mambo kama hayo huenda tunaweza kuwa kwenye uwanja mzuri wa kujadili mada na kubaini kama hii elimu ya uzazi kwa watoto imeleta faida kubwa au imeleta hasara

Note: Binafsi naamini kuna umri ambao mtoto hasitahili kufundishwa vitu visivyo vya umri wake.

Unamfundisha mtoto wa darasa la tano, kidato cha kwanza, cha pili au hata cha tatu faida za kutumia condoms na njia nyingine za uzazi wa mpango ili akavitumie wapi? Anahitaji kupanga uzazi gani kwa wakati huo?

Unamfundisha mtoto wa shule ya msingi/O-level umuhimu wa kutumia njia za uzazi wa mpango wakati wa kujamiiana kujikinga na mimba maana yake ni nini? Kwamba asione tabu kujinyima tendo hilo kwasababu uwezo wa ku enjoy na kubaki salama anao au tusemeje?

Elimu ya uzazi ni muhimu kweli kuwasaidia watoto wa kike kuja kuwa mama bora lakini kwa namna inavyoendeshwa na kupigiwa promo imefikia hatua haisaidii tena kwa baadhi ya watoto hasa wa rika la chini bali inaharibu na kuwapa ujasiri wa kutaka kushiriki ngono mapema zaidi kwasababu hawaoni madhara ya kufanya hivyo

Siku hizi watoto wa kike kidato cha pili, cha tatu hawaoni tabu kutumia vidonge vya uzazi wa mpango na wengine wanagombana na manesi huko kwa kuomba huduma ya kuweka vijiti! Haya ndo malengo mahususi ya elimu hii?

Siku hizi mtoto wa kike kidato cha pili, cha tatu haoni aibu kulala na mwaume mwenye umri sawa na Baba yake kwasababu anajua watatumia condoms? Hiki ndo kilicholengwa? Kuwaondolea aibu mabinti au?

Tukubali tukatae, tutukane tusitukane, tumuite mleta mada (pengine na Mimi niliyechangia hapa) kwamba tumebeba matikiti maji badala ya vichwa, lakini ukweli utabaki kuwa ukweli haya mambo yanaharibu watoto zaidi kuliko kuwajenga!

Namna inavyoendeshwa inawafanya watoto wasione cha ajabu kufanya ngono. Inawajengea ujasiri kwamba wanaweza kufanya ngono na wakabaki salama wasiwe kitu chochote.

Nimeyasema haya kwasababu nina ushahidi huo. Hudhuria matamasha au sehemu yoyote hata kama ni shuleni siku ambayo hii elimu inatolewa hasa na hizi NGO kisha fuatilia maswali watoto wanayouliza na munkali wanaokuwa nao baada ya kipindi utapata majibu sahihi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpeleke wa kwako kwa Pilato

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi naona elimu ya jinsia inasaidia sana Mkuu
Usipomfundisha mtoto atajifunza kwa kuona, utandawazi umekuja na mengi
Mtoa mada umebeba kichwa au boga tunahurumia miguu yako kuibebesha boga badala ya kichwa
Ni ujinga sana km serikali itakusikiliza

Sent using Jamii Forums mobile app
Nahisi mtoa mada alimaanisha sex education ambayo kwa kiswahili inaweza kuwa ni elimu ya 'ngono' lakini neno hilo hutia ukakasi na wanaamua kusema elimu ya uzazi. Kama ni hivyo yuko sahihi. Kuwafundisha watoto wa shule za msingi kama wanavyofanya ulaya kwa mazingira yetu ni upuuzi wa kiwango cha juu. Ndo maana watoto wa nchi hizo kuuliza swali juu ya 'vagina' au 'penis' siyo tatizo. Hebu mtoto aulize nyumbani kwa kiswahili.

Naona wengine wanashabikia itolewe elimu ya jinsia. Haya yote yana manufaa huko kwa waliopinda. Yana maana sana kwa sababu hapo ndo watoto hushawishiwa waone umuhimu wa haki za mashoga kama sehemu ya jamii na kwamba hawavunji sheria. Hapo ndo neno gender lilishika kasi ili kuwaingiza lakini hapa kwetu bado ni 'sex' Mwanaume na mwanamke, basi! Anayetaka ushoga afie mbali. Walipoona hivyo, gender ikaingiza wanawake, watoto, wazee, wanaume, wasiojiweza wanaojiweza, nk. They are all immaterial!
 
Nahisi mtoa mada alimaanisha sex education ambayo kwa kiswahili inaweza kuwa ni elimu ya 'ngono' lakini neno hilo hutia ukakasi na wanaamua kusema elimu ya uzazi. Kama ni hivyo yuko sahihi. Kuwafundisha watoto wa shule za msingi kama wanavyofanya ulaya kwa mazingira yetu ni upuuzi wa kiwango cha juu.

Naona wengine wanashabikia itolewe elimu ya jinsia. Haya yote yana manufaa huko kwa waliopinda. Yana maana sana kwa sababu hapo ndo watoto hushawishiwa waone umuhimu wa haki za mashoga kama sehemu ya jamii na kwamba hawavunji sheria. Hapo ndo neno gender lilishika kasi ili kuwaingiza lakini hapa kwetu bado ni 'sex' Mwanaume na mwanamke, basi! Nayetaka ushoga afie mbali. Walipoona hivyo, gender ikaingiza wanawake, watoto, wazee, wanaume, wasiojiweza wanaojiweza, nk. They are all immaterial!

Wabongo bwana , kazi yenu nikuukimbia ukweli hila watoto wenu wakipata ukimwi na Early pregnant mnaishia kublame.

MPE mtoto Elimu yakijisinsia ....Unaweza kusoma kitabu cha kilio chetu/ Ukiukataa ukweli nisawa nakukimbia kivuri chako.
 
Twende polepole baadaye utagundua unashabikia usichofahamu. Hiyo elimu ni wapi iliposaidia Ukimwi na mimba? Nchi gani?
 
Mkuu IQ yako ndogo
Acha kuniita mkuu, sema mwalimu. Hapa nimeamua kukupa shule isiyokuwa kichwani mwako. Usikwepe uzembe wako wa kufikiri.
Nauliza tena, nchi gani ambayo sex education imesaidia kuzuia UKIMWI na mimba kwa watoto?
 
Sasa unataka kusema elimu yakijinsia haifai au? Maana maeneo ya vijijini watoto wengi wamekosa elimu yakijinsia , na wengi wemeapata ukimwi na Mimba za utotoni ...sasa Hii Elimu ikifundishwa mashuleni itakuwa ndo njia sahii yakuzuia Mimba za utotoni + ukimwi
 
We mtu una elimu gani? Hayo unayoandika umeyaona wapi au umeyasikia wapi yakifanikiwa? Au ndo theory yako kichwani.
Unaulizwa hiki unajibu kile au unatukana.
Yaonekana huna la kutetea ila ulikuwa na muda wa kuandika JF. Next time usijadili jambo ambalo huna ufahamu nalo.
 
Sisi wabongo tunafeli hapo tuu, na ndio maana malezi yetu kwa kiasi kikubwa yana changamoto nyingi
Nyumbn mtoto ananyimwa elimu ya jinsia , taasisi zinajitolea kuwapatia elimu kwa faida yako wewe mzazi na mwanao wewe hutaki
Waswahili kwa nongwa
 
Mnasema waacheni wazae, sawa wafundisheni kila kitu msisahau hata ya kitandani, stupidity stories, eti mtoto azae arudi shule, ujinga mtupu, wenzengu wazungu ulisikia wapi mtoto kazaa akiwa school.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sisi wabongo tunafeli hapo tuu, na ndio maana malezi yetu kwa kiasi kikubwa yana changamoto nyingi
Nyumbn mtoto ananyimwa elimu ya jinsia , taasisi zinajitolea kuwapatia elimu kwa faida yako wewe mzazi na mwanao wewe hutaki
Waswahili kwa nongwa
Hata wewe ufahamu wako ni tatizo tu. Jipe muda wa kufikiri kabla ya kushukuru unachopewa.
 
Nahisi mtoa mada alimaanisha sex education ambayo kwa kiswahili inaweza kuwa ni elimu ya 'ngono' lakini neno hilo hutia ukakasi na wanaamua kusema elimu ya uzazi. Kama ni hivyo yuko sahihi. Kuwafundisha watoto wa shule za msingi kama wanavyofanya ulaya kwa mazingira yetu ni upuuzi wa kiwango cha juu. Ndo maana watoto wa nchi hizo kuuliza swali juu ya 'vagina' au 'penis' siyo tatizo. Hebu mtoto aulize nyumbani kwa kiswahili.

Naona wengine wanashabikia itolewe elimu ya jinsia. Haya yote yana manufaa huko kwa waliopinda. Yana maana sana kwa sababu hapo ndo watoto hushawishiwa waone umuhimu wa haki za mashoga kama sehemu ya jamii na kwamba hawavunji sheria. Hapo ndo neno gender lilishika kasi ili kuwaingiza lakini hapa kwetu bado ni 'sex' Mwanaume na mwanamke, basi! Anayetaka ushoga afie mbali. Walipoona hivyo, gender ikaingiza wanawake, watoto, wazee, wanaume, wasiojiweza wanaojiweza, nk. They are all immaterial!
Mijitu kazi kukosoa tu wala haitafakari kwanzasio kila kitokacho kwa mzungu kinatufaa ile mijitu haitupendi tudanganyike tu na unafiki wao.

Kuna myaka tuliambiwa tuwe na dini mseto inawezekana vipi hili?

Hawa watu kama hatutaishi kama watakavyo basi wapo tayali tufe sote wabaki wenyewe.

Ndo tunaendelea kuingia kwenye mipango yao ya mda mlefu.
 
Wabongo bwana , kazi yenu nikuukimbia ukweli hila watoto wenu wakipata ukimwi na Early pregnant mnaishia kublame.

MPE mtoto Elimu yakijisinsia ....Unaweza kusoma kitabu cha kilio chetu/ Ukiukataa ukweli nisawa nakukimbia kivuri chako.
Mtoto mdogo hatakiwi kushiriki ngono hilo ndo la kumfundisha sio kumuelekeza namna ya kufanya asizurike
 
Back
Top Bottom