Wanasiasa wa Upinzani kuweni makini mnapofanya mahojiano na Media za Nje

Wanasiasa wa Upinzani kuweni makini mnapofanya mahojiano na Media za Nje

Mlachake

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2009
Posts
4,437
Reaction score
4,618
Leo nilibahatika kusikiliza Live interview ya Mheshimiwa Tundu Lissu na Televisheni moja nchini Kenya. Mtangazaji Aliegemea kwenye Hoja tatu kama zilivyo orodheshwa hapo chini.

1. Kupigwa Risasi kwa Tundu Lissu
2. Hali ya Covi-19 kwa Tanzania kwa sasa
3. Hali ya haki za Binadamu kwa Tanzania kwasasa

Binafsi Nitaegemea kwnye hoja ya Pili ambayo ni COVID-19.

Ikumbukwe kwamba Kenya ni Moja ya nchi mpinzani wetu mkubwa katika sector ya utalii na ndio maana mpaka leo kuna watu wanajua mlima kilimanjaro ambao ni moja ya kivutio kikubwa cha utalii duniani upo Kenya.

Suala la Tanzania kufungua mipaka na kukaribisha Watalii kipindi cha COVID-19 kimewaumiza sana majirani zetu, na wataalam wa masuala ya uchumi lazima watakwambia tumegain positively kiuchumu kwa move hii.

Niseme ukweli ni ujinga kuiponda serikali kwa hatua ilizochukua kuhusu COVID-19, Halafu unasema COVID-19 ipo sana Tanzania kwa takwimu zipi? Kilichopo ni watu kuchukua tahadhari na kuendelea na maisha.

Hivi hii COVID-19 ingekuwepo hapa Tanzania na maambukizo yawe ndio kama tunavyoelezwa Tanzania si kungekua na maiti huko Barabarani zimezagaa? Nani aliangalia fainali ya FA cup kati ya Simba na Namungo? mliona ule msongamano

Lets be careful guys, Ninajua wengi hawatapenda hii kwakua wana mahaba na upinzani lakini penye ukweli lazima usemwe.

Sijafurahia walivyofanya baada ya mahojiano kuweka TBT YA IDDI AMIN DADA AKIWAFOKEA MAWAZIRI WAKE.
 
Hapo huyo Tundu kakosa uzalendo unaipondaje nchi yako kwa watu Baki huko nje, corona yenyewe ni ugonjwa wa propaganda, pia kuwa mpinzani sio lazima uponde kila Jambo corona ingekuwepo kweli basi wagonjwa wangeonekana kila hospital.

Na pia sio lazima kuiga wengine kwenye ku deal na mambo, hapo tundu kakengeuka Sana tu maana upinzani wa mihemko na usio na tija wa kuharibu imagine ya nchi ni upinzani hewa, haufai kwa mstakabali wa nchi
 
Haupo kwa vigezo gani? Kwanini haupo

Upo kwa vigezo gani? Kwanini upo

Very confusing this case jameni
 
Aache upuuzi yeye toka anaingia nchini amechukua tahadhari gani dhidi ya corona...mbona mda wote amekuwa kwenye nyomi ya watu tena hata wazee akina Sefu wanatembea bila barakoa tena kwenye msongamano wa watu.

Atulie ajenge hoja zake vyema, wengi tupo nyuma yake..vya ukweli tutamsapoti vya uongo ataambiwa ukweli ajirekebishe.
 
I agree. Kwa hili hata mimi sipo nae kabisa.
 
Mkuu wewe unauakika gani kama Corona imeisha Tanzania ..??
Ungekuja na idadi za ndugu zako wa karibu waliopoteza maisha kwa ugonjwa huo wa Covid -19 hapo kidogo ningeanza kukuelewa, lakini stori za vijiweni hapa havina nafasi. Vifo vya binadamu vilikuwepo na vitaendelea kuwepo hata kabla ya Korona, idadi ya vifo bado inaendelea kuwepo kama ile hata kabla ya corona ambao vifo vyao vinafahamika kwa madaktari. Tueleze ni mkoa gani ambao wananchi wana ugonjwa huo hatari kuzidi ukimwi na malaria?
 
Aache upuuzi yeye toka anaingia nchini amechukua tahadhari gani dhidi ya corona...mbona mda wote amekuwa kwenye nyomi ya watu tena hata wazee akina Sefu wanatembea bila barakoa tena kwenye msongamano wa watu.

Atulie ajenge hoja zake vyema, wengi tupo nyuma yake..vya ukweli tutamsapoti vya uongo ataambiwa ukweli ajirekebishe.
Vijana wanasema leo Lissu katoa boko.
 
Back
Top Bottom