Wanasiasa wa Upinzani kuweni makini mnapofanya mahojiano na Media za Nje

Wanasiasa wa Upinzani kuweni makini mnapofanya mahojiano na Media za Nje

Kama ameongea hivyo kwenye issue ya COVID19 huyo ni tatizo. Haiwezekani madaraka yakufanye ufanye chochote ili ufanikiwe bila kujali uzalendo.

Hivi uzalendo ni kupiga risasi wanaokukosoa?

Magufuli na wenzake huko CCM na serikali yao yote siyo wazalendo unless uwe hujui maana ya "uzalendo" na "mtu mzalendo"....

Huyu ni tyrant, muuaji na mwizi bila shaka yoyote...

Very unlucky and unknowingly, you're defending these...!!
 
Kama ameongea hivyo kwenye issue ya COVID19 huyo ni tatizo. Haiwezekani madaraka yakufanye ufanye chochote ili ufanikiwe bila kujali uzalendo.

Kama ni kweli kwa hili Lisu alipaswa kujibu kwa kulinda image ya nchi, lakini unatarajia nini kama hivi vyombo vyetu kila akiongea wanakata asisikike? Sijasikia hayo majadiliano ili nijiridhishe na alichojibu, ili niweze kuwa katika mazingira mazuri ya hitimisho. Ni vyema vyombo vya hapa nchini vikaacha kuwa biased na kumuhoji yeye hayo maswali wanayotaka aweke uzalendo, sio mambo ya kumbania kisha kuacha ahojiwe na watu wengine.
 
uala la Tanzania kufungua mipaka na kukaribisha Watalii kipindi cha COVID-19 kimewaumiza sana majirani zetu, na wataalam wa masuala ya uchumi lazima watakwambia tumegain positively kiuchumu kwa move hii.

Niseme ukweli ni ujinga kuiponda serikali kwa hatua ilizochukua kuhusu COVID-19, Halafu unasema COVID-19 ipo sana Tanzania kwa takwimu zipi? Kilichopo ni watu kuchukua tahadhari na kuendelea na maisha.

Hivi hii COVID-19 ingekuwepo hapa Tanzania na maambukizo yawe ndio kama tunavyoelezwa Tanzania si kungekua na maiti huko Barabarani zimezagaa? Nani aliangalia fainali ya FA cup kati ya Simba na Namungo? mliona ule msongamano

Lets be careful guys, Ninajua wengi hawatapenda hii kwakua wana mahaba na upinzani lakini penye ukweli lazima usemwe.
Wakisema Lissu bado hajapona ama amepewa mulungula na watu fulani...baadhi ya watu wanahamaki. Hata hivyo, dawa yake na wale wanaomuunga mkono kwa kutaka kuizamisha Tanzania inachemshwa na wananchi. Atainywa na atapona.
 
Halafu mbaya zaidi mwezi ujao zinaanza kampeni vipi atahutubia wananchi kwa YouTube au atawakusanya tu na kuwatoa mhanga kwenye corona.?
Hajajiandaa wala kuandaliwa kuwa mgombea Urais. Anaongea kiharakati mno kuliko jukumu analotakiwa ku face. Kwasasa nchi ipo kwenye diplomacy tension na Kenya sababu ya COVID19 na kila mmoja anataka nchi yake kunufaika.

Hapo alipaswa kujua aseme nini au ikibidi aseme hilo ni swala la ndani na tunaoshauri serikali kwa utaratibu tuliojiwekea na kuhusu hali ya sasa no comments sababu hakuna takwimu rasmi na pia wananchi wanaendelea na maisha bila hofu.

Anaposema watu wanakufa amesikia kwa nani? Huyu wasipomuweka chini wakamtoa hasira na uanaharakati tutashuhudia kampeni kituko safari hii.
 
Leo Nilibahatika Kusikiliza Live interview ya Mheshimiwa Tundu Lissu na Televisheni moja nchini Kenya. Mtangazaji Aliegemea kwenye Hoja tatu kama zilivyo orodheshwa hapo chini.

1. Kupigwa Risasi kwa Tundu Lissu
2. Hali ya Covi-19 kwa Tanzania kwa sasa
3. Hali ya haki za Binadamu kwa Tanzania kwasasa

Binafsi Nitaegemea kwnye hoja ya Pili ambayo ni COVID-19.

Ikumbukwe kwamba Kenya ni Moja ya nchi mpinzani wetu mkubwa katika sector ya utalii na ndio maana mpaka leo kuna watu wanajua mlima kilimanjaro ambao ni moja ya kivutio kikubwa cha utalii duniani upo Kenya.

Suala la Tanzania kufungua mipaka na kukaribisha Watalii kipindi cha COVID-19 kimewaumiza sana majirani zetu, na wataalam wa masuala ya uchumi lazima watakwambia tumegain positively kiuchumu kwa move hii.

Niseme ukweli ni ujinga kuiponda serikali kwa hatua ilizochukua kuhusu COVID-19, Halafu unasema COVID-19 ipo sana Tanzania kwa takwimu zipi? Kilichopo ni watu kuchukua tahadhari na kuendelea na maisha.

Hivi hii COVID-19 ingekuwepo hapa Tanzania na maambukizo yawe ndio kama tunavyoelezwa Tanzania si kungekua na maiti huko Barabarani zimezagaa? Nani aliangalia fainali ya FA cup kati ya Simba na Namungo? mliona ule msongamano

Lets be careful guys, Ninajua wengi hawatapenda hii kwakua wana mahaba na upinzani lakini penye ukweli lazima usemwe.

Sijafurahia walivyofanya baada ya mahojiano kuweka TBT YA IDDI AMIN DADA AKIWAFOKEA MAWAZIRI WAKE.

"Nitasema kweli daima fitina kwangu mwiko." Moja ya imani za chama pendwa ambayo ilibakia kwenye makaratasi.

Msema kweli ni mpenzi wa Mungu. Vitabu vya dini vinasema "usiseme uongo."

Mchana utaendelea kuwa mchana hata kama binafsi ungependa vipi iwe usiku.

Kujidanganya hakutatusaidia:

Watanzania, Kuukimbia ukweli hakutatusaidia

Heko Lissu kwa kuusema ukweli. Hauko peke yako. Wanaokumbatia janja, ghiliba, hadaa, na yote ya namna hiyo watakutana nasi October 2020 at our best.

Wanasahau kuwa wahanga wa ugonjwa huu wana ndugu na jamaa zao. Eti kuwa kwa njaa zao wao binafsi, basi kila mmoja na wahanga wote waingie kwenye ushabiki tu wa fulani dhidi ya fulani.

Mtoa mada tambua ushabiki wa kwenye Mbao FC, Ndanda, Mbeya City, Namungo FC nk, hauna nafasi kunapokuja masuala halisi na hasa yenye kuhusisha maisha ya watu.
 
Huyo jamaa yenu ni roporopo by birth wala hajaanza leo.

Ni sawa na kumwambia bata asinye kinyesi rojorojo.😁!
 
Leo Nilibahatika Kusikiliza Live interview ya Mheshimiwa Tundu Lissu na Televisheni moja nchini Kenya. Mtangazaji Aliegemea kwenye Hoja tatu kama zilivyo orodheshwa hapo chini.

1. Kupigwa Risasi kwa Tundu Lissu
2. Hali ya Covi-19 kwa Tanzania kwa sasa
3. Hali ya haki za Binadamu kwa Tanzania kwasasa

Binafsi Nitaegemea kwnye hoja ya Pili ambayo ni COVID-19.

Ikumbukwe kwamba Kenya ni Moja ya nchi mpinzani wetu mkubwa katika sector ya utalii na ndio maana mpaka leo kuna watu wanajua mlima kilimanjaro ambao ni moja ya kivutio kikubwa cha utalii duniani upo Kenya.

Suala la Tanzania kufungua mipaka na kukaribisha Watalii kipindi cha COVID-19 kimewaumiza sana majirani zetu, na wataalam wa masuala ya uchumi lazima watakwambia tumegain positively kiuchumu kwa move hii.

Niseme ukweli ni ujinga kuiponda serikali kwa hatua ilizochukua kuhusu COVID-19, Halafu unasema COVID-19 ipo sana Tanzania kwa takwimu zipi? Kilichopo ni watu kuchukua tahadhari na kuendelea na maisha.

Hivi hii COVID-19 ingekuwepo hapa Tanzania na maambukizo yawe ndio kama tunavyoelezwa Tanzania si kungekua na maiti huko Barabarani zimezagaa? Nani aliangalia fainali ya FA cup kati ya Simba na Namungo? mliona ule msongamano

Lets be careful guys, Ninajua wengi hawatapenda hii kwakua wana mahaba na upinzani lakini penye ukweli lazima usemwe.

Sijafurahia walivyofanya baada ya mahojiano kuweka TBT YA IDDI AMIN DADA AKIWAFOKEA MAWAZIRI WAKE.

..Jpm anawaambia wananchi wasichukue tahadhari.

..TL anawaambia wananchi wachukue tahadhari.

..huu utaratibu wa kuenenda kiholela-holela wakati dunia ikihangaika kukabiliana na covid19 inatishia watu wa nje kujumuika na sisi.

..pia tukionekana hatuko makini ktk kuchukua tahadhari tunaweza kusababisha mataifa mengine yatuzuie kusafiri kwenda nchini kwao.

..Tunamshukuru kwamba covid19 haijatupiga ukilinganisha na mataifa mengine, lakini ni UJINGA kuenenda kana kwamba tunaitafuta covid19.
 
Hapo huyo Tundu kakosa uzalendo unaipondaje nchi yako kwa watu Baki huko nje, corona yenyewe ni ugonjwa wa propaganda, pia kuwa mpinzani sio lazima uponde kila Jambo corona ingekuwepo kweli basi wagonjwa wangeonekana kila hospital.

Na pia sio lazima kuiga wengine kwenye ku deal na mambo, hapo tundu kakengeuka Sana tu maana upinzani wa mihemko na usio na tija wa kuharibu imagine ya nchi ni upinzani hewa, haufai kwa mstakabali wa nchi
Kwa hiyo Marekani wanapotangaza maambukizi ya Covid-19 na kuonesha wanaongoza duniani ni kukosa uzalendo.

Watanzania mbona mnapenda nchi iongozwe kienyeji enyeji hivyo. Tunaenda shule ili tupractice professionalism sio uswahili.
 
Kuna kitu chaitwa maslahi ya taifa yaani National Interest.

Hao mabeberu wake huko waliko hata wakigombana vipi, wakija kwenye media wanakuwa wanaunga mkono na wanaweka pembeni tofauti zao za kisiasa.

Juzi tu huko UK serikali waliamua kufunga moja ya mikoa ya kaskazini maeneo ya Manchester kwa kuogopa kuenea kwa ugonjwa na ilikuwa ni siku kuu ya iddi.

Lakini vyama vya upinzani vikiongozwa na Labour walikuja kwenye media na wakasema wanaunga mkono hatua ya serikali.

Hivyo hivyo walifanya walipoweka karantini ya wiki 2 wapinzani wameunga mkono.

NI kwa maslahi ya taifa au National Interets.

Ukiwa raia wa nchi unatakiwa kulinda maslahi ya taifa si kuyatafutia majambazi huko nje ya kuja kuharibu.

..hivi CCM mmewahi kuwaunga mkono wapinzani ktk jambo gani?

..mbona kila siku mnawachafua na kujaribu kuwaaminisha wananchi kwamba wapinzani ni watu wabaya?
 
Yani wanaofanya CCM iendelee kuwa madarakani ni hao hao wapinzani kwa kushindwa kujitambua na kutambua nafasi zao.

Ni bora shetani unaemjua siku zote, kuliko...
Shetani ni shetani tu, ukikaa vibaya anakumiminia risasi 38, ogopa shetani.
 
lisu anaendelea na drama zake za risasi wakati akisubiri ilani ya uchaguzi itoke kwa mabeberu huko.
 
Ungekuja na idadi za ndugu zako wa karibu waliopoteza maisha kwa ugonjwa huo wa Covid -19 hapo kidogo ningeanza kukuelewa, lakini stori za vijiweni hapa havina nafasi. Vifo vya binadamu vilikuwepo na vitaendelea kuwepo hata kabla ya Korona, idadi ya vifo bado inaendelea kuwepo kama ile hata kabla ya corona ambao vifo vyao vinafahamika kwa madaktari. Tueleze ni mkoa gani ambao wananchi wana ugonjwa huo hatari kuzidi ukimwi na malaria?
A country with no data, a chiefdom type of leadership.
 
Hajajiandaa wala kuandaliwa kuwa mgombea Urais. Anaongea kiharakati mno kuliko jukumu analotakiwa ku face. Kwasasa nchi ipo kwenye diplomacy tension na Kenya sababu ya COVID19 na kila mmoja anataka nchi yake kunufaika.

Hapo alipaswa kujua aseme nini au ikibidi aseme hilo ni swala la ndani na tunaoshauri serikali kwa utaratibu tuliojiwekea na kuhusu hali ya sasa no comments sababu hakuna takwimu rasmi na pia wananchi wanaendelea na maisha bila hofu.

Anaposema watu wanakufa amesikia kwa nani? Huyu wasipomuweka chini wakamtoa hasira na uanaharakati tutashuhudia kampeni kituko safari hii.
Kabisa anahitaji washauri ili aongee kama Rais mtarajiwa sio mwanaharakati wa mitaani.

Watanzania hakuna anaependa kuona Wala kusikia adha za corona..

Lisu asicheze na hisia za wahisani zaidi kuliko za Watanzania wa kawaida ambao hawawezi kumudu lockdown ya hata siku tatu.

Toka amefika Tanzania amekuwa kwenye mikusanyiko muda wote bila tahadhali yoyote Ile, Ina maana hahofii Covid-19.

Atuambie ndani ya familia yake aliyoiacha Tanzania wamekufa wangapi kwa corona ama ndani ya Chadema pamoja na misongamano yote Ile wamekufa viongozi na wajumbe wangapi pamoja na familia zao.

Aendelee kupigania Uhuru wa kujieleza na sheria za mitandao za ajabu ajabu.
 
Kweli wewe ni busu la kenge. Ambaye hafi hadi damu zimtoke maskioni. Mleteni dreva wake akaripoti kituo cha polisi atausema ukweli wa kwanini yeye alitoka mzima kabsaaa. Na ilihali ukijua risasi haina macho?? pia kwanini ajeruhiwe mguu wa kulia pasipo mguu wa kushoto kutopata hitirafu. Kuna maswali mengi ya kujiuliza lakini majibu yatapatikana pindi mtakapo mleta na kumkabidhi dereva wake kituo cha polisi. Ni hayo tuu
CCTV camera ziling'olewa na majambazi wenzako
 
Wewe nae acha kutetea UJINGA, Suala la COVID19 ni Kama MIMBA tu ufiche usifiche litaonekana tu, Sasa kwà TZ hii matukio Kama hayo tuneyaona wapi!?? Au umesikia wapi kaka!!

TL tatizo ana mdomo mkubwa Sana anaongeaongea tu Kama Propeller Kuna vitu hapaswi kuzungumza kabisa Ila yeye anaongeaongea tu bila Tashwishiwi,.

Hawa hawa Wapinzani walituaminisha kuwa COVID19 Ipo sana bunge lifungwe wabunge waende Quarantine, GVT ikagoma wakaenda wenyewe afu Baada ya siku 14 wakarejea tena Bungeni na wakakaa na CCM hao hao na bila Hata kuchukua tahadhari Wala kugoma kukaa nao Bungeni!!

Afu Wewe Tena unatetea UJINGA Sijui nawewe nae MJINGA Mkuu, Upinzani wa BONGO haupaswi kabisa kupewa madaraka labda DUNIA iumbwe kwà Mara ya pili!!
Tumeficha data, ukiugua utajijua mwenyewe na familia yako
 
Back
Top Bottom