Sema na nafsi yako kuwa leo mko kwenye msimu wa kwaresma/Ramadhani hivyo mtafunga siku nzima. Hiyo buku tatu iweke kwenye wallet yako itakupa ujasiri wa kuwa nina hela na itaondoa hofu.
Ikifika saa moja usiku muda wa kufungua/kuvunja funga yako nenda kwenye kijiwe cha kahawa toa mia 5, hapo upate vikombe vya kahawa na kashata hadi ushibe.
Rudi nyumbani oga maji baridi, kunywa maji ya kuchemsha nyumbani au hata ya bomba lala usingizi wa amani huku kwenye wallet umebakiwa na 2,500 ya kuanza nayo kesho.
Leo isikutishe, unaimudu. Kesho huijui, ipangilie vyema.
Kila la Kheri.