Wanauchumi nipeni bajeti nikiwa na buku 3 natoboa vipi siku

Asubuhi piga neutral.

Mchana nunua maandazi ya buku kunywa na maji (maji yawe kama chai). Itabaki buku 2.

Usiku nenda kwa mama lishe yeyote wa kilocal mwambie unataka ukoko wa buku 2. Utapata ukoko mwingi sana na mboga nyingi kwa ajili ya kuulainisha. Utakula mpaka utauangalia.
Ni noumaa!
 
Ukoko kumbuka tumbo la kuhara likikushika na haina pesa ya kujitibisha
 
Vijana wenzang pesa zinapokutembelea tuwe tunanunua katoyo kamoja kaemergency siku umekosa kabisa mchongo unaingia road kama mida hii unaanza kula vichwa mpaka saa 6 za usiku

Fanya hvyo kila siku mpaka michongo itakapokaa sawa
 
Supu ya kero?
Kwani nyama kg 1 bei gani?
Ukifika pale Vigunguti kuanzia saa 3:00AM -05:00AM

Utapata nyama ya bei rahis Sana kupitia Kwa wachinjaji

So mama ntilie ndo ununua hiyo nyama na kuuza supu wastani wa 500-1000 na kuendelea
 
Kwa kipato chako nakushauri utafute lijimama dar lenye kipato kikubwa likulee
 
Vijana wenzang pesa zinapokutembelea tuwe tunanunua katoyo kamoja kaemergency siku umekosa kabisa mchongo unaingia road kama mida hii unaanza kula vichwa mpaka saa 6 za usiku

Fanya hvyo kila siku mpaka michongo itakapokaa sawa
Ushauri tumeuzingatia
 
Ukifika pale Vigunguti kuanzia saa 3:00AM -05:00AM

Utapata nyama ya bei rahis Sana kupitia Kwa wachinjaji

So mama ntilie ndo ununua hiyo nyama na kuuza supu wastani wa 500-1000 na kuendelea
Napiga hesabu
Mtu asafiribafate nyama
Mkaa, maji, chumvi, vyombo, muda
Hiyo supu ya jero inakuwaje
 
Nenda kwenye soko lolote kubwa katika mkoa wako huwezi kukosa mishe ya kukuingizia japo buku 5 kwa siku.

Buku tatu
Chai na chapati mbili 700
mchana unapiga Dash unakuja kula mpakani saa 11/12 (baina ya mchana na Usiku ) Wali wa buku jero.

Siku imeisha hiyo 800 utaamkia nayo kesho nauli ya kutafuta chochote kitu.

Ukiwa huna kitu epuka kulala sana na kujifungia ndani.Toka nje katafute huku ukimuomba Mungu akufanyie wepesi katika njia zako. Pia usiibe, usidhulumu wala usimkufuru Mungu kwa hali yako hiyo ya Umaskini.
 
Labda umeze hewa ya oxygen breakfast, mchana utafune matumaini, halafu usiku ulale na ndoto za pilipili hoho!

Kutamba! labda upike ugali kwa moto wa mshumaa halafu ule na harufu ya dagaa.

😂
 
Street hack:

Kama huna kitu mfukoni basi usiishi sehemu ambayo ni mbali na Soko lolote kubwa katika mkoa wako.

Sokoni ndio sehemu unayoweza kupata chai na lunch ya mkopo iwe unalipa baadae baada ya kuwa umeshashiba. Na ndio sehemu unaweza kupata vyakula kwa bei rahisi na pia kutokana na mzunguko wa pesa kuwa mkubwa maeneo hayo ni rahisi kupata vibarua vidogo vidogo kama kubeba mizigo midogo midogo hata kufanya biashara ndogondogo za kusambaza mifuko, kuuza kahawa n.k na maisha yakaenda vizuri tu.
 
Breakfast ni kwa matajiri
Sada una buku tatu unawaza Breakfast?

Nenda wayahudi watatu utakunywa na maji
 
Street hack:

Kama huna kitu mfukoni basi usiishi sehemu ambayo ni mbali na Soko lolote kubwa katika mkoa wako.

Sokoni ndio sehemu unayoweza kupcodeata chai na lunch ya mkopo ime unalipa baadae baada ya kuwa umeshashiba. Na ndio sehemu unaweza kupata vyakula kwa bei rahisi na pia kutokana na mzunguko wa pesa kuwa mkubwa maeneo hayo ni rahisi kupata vibarua vidogo vidogo kama kubeba mizigo midogo midogo hata kufanya biashara ndogondogo za kusambaza mifuko, kuuza kahawa n.k na maisha yakaenda vizuri tu.
Code
 
Nenda kwenye soko lolote kubwa katika mkoa wako huwezi kukosa mishe ya kukuingizia japo buku 5 kwa siku.

Buku tatu
Chai na chapati mbili 700
mchana unapiga Dash unakuja kula mpakani saa 11/12 (baina ya mchana na Usiku ) Wali wa buku jero.

Siku imeisha hiyo 800 utaamkia nayo kesho nauli ya kutafuta chochote kitu.

Ukiwa huna kitu epuka kulala sana na kujifungia ndani.Toka nje katafute huku ukimuomba Mungu akufanyie wepesi katika njia zako. Pia usiibe, usidhulumu wala usimkufuru Mungu kwa hali yako hiyo ya Umaskini.
Ushauri wako inatakiwa ulipiwe😅🤣😀
 
Back
Top Bottom