Wanaume acheni huu uchafu

Wanaume acheni huu uchafu

Dunia ya leo bado hatuwezi kuhakikisha choo kinakuwa na maji!! Yaan choo kinakaa bila maji kumsubiri atakayeingia akuje na maji yake!!!
 
Habari ya weekend
Leo naomba niwaulize enyi kaka zetu na baba zetu, aliyewaambia kuwa ninyi mkienda msalani kwa haja ndogo hamtakiwi kubeba maji ni nani?

Utaona mkaka mtanashati kabisa, kwa macho ya kawaida anaonekana anajiheshimu ila sasa muangalie mambo anayofanya ptuu yanatia aibu. Tunaoishi kwenye nyumba zenye vyoo vya kushea tuna tabu sana...

Hebu bebe ni maji sio uungwana kuingia kule mahali then unaacha harufu ya mikojo, asilimia kubwa ya wanaume mnafanya hivi sio vizuri kwa kweli.
Niwatakieni wiki njema
Ungeeleza choo cha namna gani. Kama cha shimo mbona haileti maana kukojoa tu uingie na maji?
 
Hii tabia ninayo mimi yani kwenda haja ndogo na maji ni mwiko mpaka mwaka fulani wapangaji wenzangu waikuwa wakiniona nimetoka kwenye harakati zangu wanaitana ili mwenye kwenda chooni aende kabla sijaenda mimi

Nilikifanya choo cha wapangaji wenzangu kama changu maana siku ambayo nilikuwa nikishinda geto wanajua hali ya hewa itakuwa tofauti tena kipindi hicho natumia vile vilevi vyetu vikali

Sema nilianza kuingia na maji baada ya mtoto wa mpangaji kuugua U.T.I walinikalisha kikao nweeeeeeh eti kwa hii hali nitaua watoto

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hayo maji nikienda nayo nitayafanyia nini?
Huruhusiwi kunywa maji toilet
.
20200416_212847.gif
 
Nastaajabu hilo ila hustaajabu zaidi mtoto wa kike aingiapo bila maji na atokapo ni mkavu kama hakuna kilichotokea, dunia ina mambo
 
Habari ya weekend
Leo naomba niwaulize enyi kaka zetu na baba zetu, aliyewaambia kuwa ninyi mkienda msalani kwa haja ndogo hamtakiwi kubeba maji ni nani?

Utaona mkaka mtanashati kabisa, kwa macho ya kawaida anaonekana anajiheshimu ila sasa muangalie mambo anayofanya ptuu yanatia aibu. Tunaoishi kwenye nyumba zenye vyoo vya kushea tuna tabu sana...

Hebu bebe ni maji sio uungwana kuingia kule mahali then unaacha harufu ya mikojo, asilimia kubwa ya wanaume mnafanya hivi sio vizuri kwa kweli.
Niwatakieni wiki njema
Una point lakini umefanya jumuishi mno.
Nadhani ungesema kwa wale wanaoishi kwenye nyumba ambazo hazina maji vyooni wabebe maji. Na siyo wanaume tu, tunashudia wanawake wengine wakitinga bila maji. Ukiona wanabeba ujue wako ktk "nyakati". Ila wahusika ujumbe umewafikia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhani wengi hatuna utaratibu huo labda kwakua maumbile yetu yanaruhusu kufanya hivyo,,Lakini ladies inawalazimu kuingia na maji ili kuosha nyeti baada ya haja..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom