Kijakazi
JF-Expert Member
- Jun 26, 2007
- 7,093
- 10,469
Majibu ya Sensa yameonyesha kwamba Wanawake ni wengi zaidi kuliko Wanaume, baadhi ya Wanaume wanaona ni jambo zuri kwao, lakini ni wajinga kwani wasichokijua ni kwamba Wanaume ni wachache kuliko Wanawake kwa sababu Wanaume wanakufa mapema kuliko Wanawake, Kibaologia uwiano kati ya Wanawake na Wanaume ni 1:1 Dunia nzima ila human factors kama vita, umaskini, njaa, magonjwa vinachangia nani aishi muda mrefu klk mwingine.
Hivyo Wanaume walipaswa wajiulize ni kwanini ni wachache? Ni kwanini wanakufa mapema? Kwa maana uwiano wa watoto wa kiume kike wanaozaliwa ni karibia sawa yaani 1:1 sasa nini kinatokea baada ya kuzaliwa hata Wanaume wapungue?
Next time angalia tu mtaani kwenu kuna wajane wangapi kulinganisha na wanaume waliopoteza wake zao kwa kifo?