Wanaume huwa mnafikiria hatari zinazoweza kuletwa na mchepuko?

Wanaume huwa mnafikiria hatari zinazoweza kuletwa na mchepuko?

Abnormal women..
Few wanaofanya kwa hamu tu na sio hisia

In most cases.,women are emotional
For most women u js dont go to bed with a man you dont love...haipoo
Je hawa wapenda hela na waangalia fursa mbona wanaenda tu
 
mada moto sana!
lakini kweli michepuko ni smoking gun..
nikikumbuka mchepuko alivyosababisha mjomba akanywa ngao ya kidonge!
alimfanyia kila kitu ila kosa moja alifanya ni kwamba lazma arudi kulala nyumbani na kuacha mchepuko peke yake...
akitoka kwa mchepuko kurudi kwa mke wake huku mchepuko anaingiza jamaa wake.
siku vimeumana jamaa alishindwa kuvumilia akanywa ngao ya kidonge na kuacha mke na watoto wadogo!
lile jomba langu sijui lilikuwa linapewa nyoro!
daahh inaskitisha sana
Dah hii inaumiza sana ila hatuwezi jua labda ndoa yake ilibaki jina ile ya wanandoa kugawana vyumba ila wanatoka mlango mmoja!!
 
Kila jambo kwenye maisha ya kawaida huwa lina faida na hasara.

Kwa kawaida tuliowengi tunapofanya jambo huwa tunaangalia faida zaidi kuliko hasara.
Hata linapokuja swala la kuoa huwa tunaangalia faida zaidi kuliko hasara, japokuwa hasara za kuoa ni kubwa kuliko faida zake.
 
Kuna huyo bro wangu since nipo form two hadi nikamalizaga na chuo huo mchepuko anao tu na wanapendana na unatupenda ndugu zake pia tunao ujua.

Alafu kama mfalme tu mwenye hekima dunia nzima alikua na michepuko 300 then who are we......? Katika kizazi hiki cha mwendo kasi.

Hata mimi binafsi kuna ninayo tena na full control kwao kama hataki atokee. Yaani anatritiwa kama Mke vile
 
Mchepuko si mrithi wa mali zako, hata uk RIP ni nadra kwa mchepuko kupata chochote labda uwe umezaa nae nae napo pia hutegemea umuhimu wa huyo mtoto kwa familia ya mume.

Mnapo kula chakula kwa mchepuko kuna uwezekano maadaui wako kuulipa mchepuko hela ukuondoe duniani. Mfano wewe unampa mchepuko laki mbili kila mkikutana, wanakuja mahasimu wako ki biashara, wanampa milioni tano akuwekee sumu kwenye chakula. Aweke sumu kwenye chakula na sahani na kijiko ulicholia vitupwe mbali kupoteza ushahidi.

Siku hizi hata mke akipewa dau la kutosha anakuondoa tu, hasa wale wanawake ambao kutwa wao kusema wanaume wote ni SAWA, ni mbwa tu. Everyone has a price.
 
Fikiria ukifa mke wako anakua widow lakini mchepuko ni official spincer
Wanawake hawa wa siku hizi hata Hilo neno widow hawalifahamu, ukifa Leo baada ya miezi 2 tu ana boyfriend na wewe unakuwa past tense. Hata watoto hawawasumbui wanapeleka boarding tu.

Wenyewe Wana makundi yao, hawababaishwi na mwanaume yoyote hata waume zao Wana kila kila kitu mwanamke anachohitaji, wanakutana jioni nao wanakaa baa na kunywa ladies only, tena wote married. Siku hizi wameacha kunywa bar wanaalikana nyumbani mwanaume unawapisha garden wanaendelea na Stori zao.

Version ya wanawake wa zamani na hawa wa sasa ni tofauti kabisa, hawa wa kuanzia late 70s, 80s na kuendelea, Yaani vijana wa kiume wanakiona Cha moto haswa.
 
Mchepuko si mrithi wa mali zako, hata uk RIP ni nadra kwa mchepuko kupata chochote labda uwe umezaa nae nae napo pia hutegemea umuhimu wa huyo mtoto kwa familia ya mume.

Mnapo kula chakula kwa mchepuko kuna uwezekano maadaui wako kuulipa mchepuko hela ukuondoe duniani. Mfano wewe unampa mchepuko laki mbili kila mkikutana, wanakuja mahasimu wako ki biashara, wanampa milioni tano akuwekee sumu kwenye chakula. Aweke sumu kwenye chakula na sahani na kijiko ulicholia vitupwe mbali kupoteza ushahidi.

Hilo la sumu hata mke anweza kulifanya.... Ni mazingira tu mliyonayo...
 
Mume/mke wako wa ndoa ndio mahusiano sahihi na salama, sio rahisi mume wako au mke wako akudhuru hata kama mmetofautiana au kugombana

Kuanzisha mahusiano nje ni gharama, usumbufu, hatari na pia ni kujitafutia mikosi tu isiyo na sababu

Management ya mahusiano ya nje ni ngumu, huwezi kuwaridhisha wapenzi wawili, wakati mwingine utaona mmoja anakukera tu na hata kumjibu msg unaona kero

Bakini njia kuu😎
Kwenye hiyo line ya mwisho, wewe umejitoa?
 
Tubaki njia kuu boss, hapo nilikua nawalenga wanaume ndio maana nikajitoa
We sema hivyo, maana hata nyie mnachepuka haswa... SI UNAKUMBUKA HESABU YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI? KWAMBA KWA SAMPLES ZILIZOPELEKWA KWAKE, 49% YA WANAUME WANALEA WATOTO SI WAO
 
We sema hivyo, maana hata nyie mnachepuka haswa... SI UNAKUMBUKA HESABU YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI? KWAMBA KWA SAMPLES ZILIZOPELEKWA KWAKE, 49% YA WANAUME WANALEA WATOTO SI WAO
Hili nalo ni janga lingine
 
Back
Top Bottom