Wanaume huwa mnahitaji nini?

Wanaume huwa mnahitaji nini?

Meridah Tough

Senior Member
Joined
Nov 27, 2017
Posts
136
Reaction score
365
Habarini zenu ndugu zangu?

Kwa kweli inafikia kipindi nakuwa sielewi hizi ishu za mahusiano.

Mwenzenu nimekuwa kwenye mahusiano na mkaka wa miaka 33. Amenizidi miaka 4. Na tumekuwa naye kwa muda mrefu sana. Katika mahusiano yetu hayo, kiukweli sijisifii lakini nimejitahidi kuwa mwema sana kwake. Nimekuwa mnyenyekevu na msikivu sana kwa mwenzangu.

Tofauti na wengi wanavyosema kuwa ukiwa hivyo unaleta upendo lakini kwangu mimi naona inakuwa tofauti. Badala ya upendo, naonekana kama mtu mjinga ambaye nimekufa na nimeoza kwake kiasi kwamba siwezi kujitetea kwa lolote.

Tabia hii kwa mwenzangu, ikazua yeye kuwa na wanawake wengine kisirisiri na inapotokea nimegundua anataka kunifanya mimi nionekane nimemkosea adabu! Kweli nina madhaifu kama binadamu, lakini kwa upendo wa dhati kwa huyu mtu kwa kweli nilikuwa nao.

Yeye mwenyewe anajua na hiyo ilimtia sana kiburi. Sasa amezua tabia mpya. Inapotokea naona mwenzangu anafanya mambo ya kipuuzi na kuwa na wanawake wengine, namwambia achague. Na cha ajabu anachagua mwenzangu mie naendelea na maisha mengine. Lakini haiwezi kupita mwezi bila huyu jamaa kurudi na kuomba msamaha sana.

Nimechoka hali hii na ninahitaji sana kuendelea na maisha mengine wadau. Naombeni mnisaidie mawazo yenu labda wapi nakwama na nini nahitaji katika suala hili la mahusiano maana naona ule uvumilivu na upendo unakufa na chuki inaibuka moyoni mwangu juu ya huyu kaka. Nilidhani ni hali ya kawaida ila sasa nina siku ya tatu akinitafuta, sina uwezo wa kuongea naye vizuri. Kwa mara ya pili toka tuanze mahusiano nimemtukana na nimemruhusu aende anapotaka kwenda.

Ila bado analalamika kwa marafiki zake kuwa nimekuwa mjeuri.
 
Each time you forgive a man and take him back for the same mistake, he loses some level of respect for you.

Sasa jitafakari. Hapo hujaolewa wala hujazaa unadhalilika. Ukija kuolewa ama kupachikwa tu ki zygote kuna rangi utaacha kuona kweli?
 
Huyo akupendi kashakufanya wewe wa kukupumzikia, mnyime hiyo kitu uone kama atahangaika nawewe tena kwako anajua ni uhakika kwa kile anachokitaka. Achana nae huyo anafanya makusudi na usitegemee kama atabadilika kama hadi sasa hajabadilika.

NB: usimtukane wala kumjibu vibaya tekeleza jambo lako kistaarabu kabisa tulia fanya maisha yako.
 
Sio kwamba anahisi ila ni ukweli kuwa umekufa na kuoza kwake kiasi cha kuwa mnyonge wake au reserve.

Uzuri umeshajua kuwa unachokifanya sicho ila nguvu ya mapenzi inakuzidia kiasi cha kushindwa kuresist matamanio ya moyo wako

Sasa unadhani comments na huruma za humu zitakusaidia vipi kama huwezi kuweka mipaka yako na kuisimamia ?
 
Achana na mtu mshenzi kama huyo alijua bila yeye wewe hutoboi komaa hivyo hivyo hata simu usipokee kabisa sometime sisi wanaume tunakuwa washenzi sana. Alijua huwezi ondoka sasa nenda kweli mazima
 
Sio kwamba anahisi ila ni ukweli kuwa umekufa na kuoza kwake kiasi cha kuwa mnyonge wake au reserve.

uzuri umeshajua kuwa unachokifanya sicho ila nguvu ya mapenzi inakuzidia kiasi cha kushindwa kuresist matamanio ya moyo wako

sasa unadhani comments na huruma za humu zitakusaidia vipi kama huwezi kuweka mipaka yako na kuisimamia ?
Brilliant advice.
 
acahana na mtu mshenzi kama huyo alijua bila yeye wewe hutoboi komaa hivyo hivyo hata simu usipokee kabisa sometime sisi wanaume tunakuwa washenzi sana. Alijua huwezi ondoka sasa nenda kweli mazima
Na wanaume wakishajua umekufa umeoza kwao aisee utaburuzwa uchakae.
 
Anaambia watu umekuwa jeuri na hao watu wanakwambia?How?Mko wangapi kwenye hayo mahusiano?Au mna fans wa mahusiano yenu?..

As long as kuna 'hao watu 'una wa entertain ..you will never be free...

Mahusiano strong muongee wenyewe kila kitu..bila kuhusisha watu...

Kama hao watu huwa anawapa offer za bia
Siku zote watakushauri 'uvumilie'
 
Back
Top Bottom