Wanaume huwa mnahitaji nini?

Wanaume huwa mnahitaji nini?

Tumechoka kuangaliaa chaneliiii teni tugeuzieni tuangalie kipindi cha wanyama apo tibisiii
 
Habarini zenu ndugu zangu?

Kwa kweli inafikia kipindi nakuwa sielewi hizi ishu za mahusiano.

Mwenzenu nimekuwa kwenye mahusiano na mkaka wa miaka 33. Amenizidi miaka 4. Na tumekuwa naye kwa muda mrefu sana. Katika mahusiano yetu hayo, kiukweli sijisifii lakini nimejitahidi kuwa mwema sana kwake. Nimekuwa mnyenyekevu na msikivu sana kwa mwenzangu.

Tofauti na wengi wanavyosema kuwa ukiwa hivyo unaleta upendo lakini kwangu mimi naona inakuwa tofauti. Badala ya upendo, naonekana kama mtu mjinga ambaye nimekufa na nimeoza kwake kiasi kwamba siwezi kujitetea kwa lolote.

Tabia hii kwa mwenzangu, ikazua yeye kuwa na wanawake wengine kisirisiri na inapotokea nimegundua anataka kunifanya mimi nionekane nimemkosea adabu! Kweli nina madhaifu kama binadamu, lakini kwa upendo wa dhati kwa huyu mtu kwa kweli nilikuwa nao.

Yeye mwenyewe anajua na hiyo ilimtia sana kiburi. Sasa amezua tabia mpya. Inapotokea naona mwenzangu anafanya mambo ya kipuuzi na kuwa na wanawake wengine, namwambia achague. Na cha ajabu anachagua mwenzangu mie naendelea na maisha mengine. Lakini haiwezi kupita mwezi bila huyu jamaa kurudi na kuomba msamaha sana.

Nimechoka hali hii na ninahitaji sana kuendelea na maisha mengine wadau. Naombeni mnisaidie mawazo yenu labda wapi nakwama na nini nahitaji katika suala hili la mahusiano maana naona ule uvumilivu na upendo unakufa na chuki inaibuka moyoni mwangu juu ya huyu kaka. Nilidhani ni hali ya kawaida ila sasa nina siku ya tatu akinitafuta, sina uwezo wa kuongea naye vizuri. Kwa mara ya pili toka tuanze mahusiano nimemtukana na nimemruhusu aende anapotaka kwenda.

Ila bado analalamika kwa marafiki zake kuwa nimekuwa mjeuri.
Watu wengine wana bahati ya kupata mpenzi mwema na mstarabu, lakini huchezea baraka hiyo. Mkuu huyo hakuthamni wala haoni thamani ya kuwa na wewe...piga chini na songa mbele
 
Daaah miaka 33 bado ana mambo ya 20's.
Bidada huyo sio wako HAKUPENDI, kikubwa ni wewe kumove one.

Wanaume wengi ni kweli tunakua na mahusiano na wadada wengi wengi lakini kuna huyo mmoja unaempenda na hufanyi ujinga kwake ni full heshima, sasa huenda huyo mtu sio wewe kwa upande wa jamaa.
Tafuta mtu wako.
 
Huu uzi ungemaliza kwa kuweka namba yako ingependeza, kuna wengine humu tuko na vipawa vya kuwapa utulivu nyie mlioangukia ktk mikono ya wahuni
 
Mwanaume anaekupenda hata ikitokea anacheat atajificha sana, na in case ukijua atajirekebisha haraka! Mkuu unapoteza muda wako, am a man najua!
 
Anaambia watu umekuwa jeuri na hao watu wanakwambia?How?Mko wangapi kwenye hayo mahusiano?Au mna fans wa mahusiano yenu?..

As long as kuna 'hao watu 'una wa entertain ..you will never be free...

Mahusiano strong muongee wenyewe kila kitu..bila kuhusisha watu...

Kama hao watu huwa anawapa offer za bia
Siku zote watakushauri 'uvumilie'
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent from my Infinix X652C using JamiiForums mobile app
 
Each time you forgive a man and take him back for the same mistake, he loses some level of respect for you.

Sasa jitafakari. Hapo hujaolewa wala hujazaa unadhalilika. Ukija kuolewa ama kupachikwa tu ki zygote kuna rangi utaacha kuona kweli?
Mara nyingi maandishi yako yana content iliyo makinika sana

Naomba urafiki mkuu
 
Asante.

Kwani urafiki wenyewe unasemaje Mkuu?

🤣🤣🤣🏃🏽‍♀️🏃🏽‍♀️🏃🏽‍♀️🏃🏽‍♀️🤭🤭🤭
Ifikie mahali wana jamii muweze kujamiiana vizuri panapo faragha huko pi emu!
 
Ila twende ndani turudi nje mapenzi yanauma..😬
Mi mwenyewe niliachwaga na pisi moja hiyo hasira zikaishia kwenye kung'ata mbao!
Hasa ukiwa upande wa “Fala” utateseka mno
 
Each time you forgive a man and take him back for the same mistake, he loses some level of respect for you.

Sasa jitafakari. Hapo hujaolewa wala hujazaa unadhalilika. Ukija kuolewa ama kupachikwa tu ki zygote kuna rangi utaacha kuona kweli?
And this goes the other way round!
 
Back
Top Bottom