Wanaume huwa mnahitaji nini?

Wanaume huwa mnahitaji nini?

Mwambie akajitambulishe ukweni, muda wote huo anaonja kwani Chumvi haijakoa tu🏃‍♂️🏃‍♂️
 
kwa lugha ngumu ni kwamba hamja match kwa hiyo hakuna upendo ila unahitajiana na yeye hakuhitaji sana ila kipo anachohitaji kwako! kwa kifupi piga chini vinginevyo kwa kuwa wanawake mnaouwezo wa kubeba yote mawili endelea kuwa naye huku ukijua hakupendi na jipange jinsi ya kukabiliana na vidonda vya tumbo, pressure na ndugu zake yanayoweza kutokana na mateso ya nafsi yako (maumivu ya ndani) kwa ajili ya mapenzi.
 
Habarini zenu ndugu zangu?

Kwa kweli inafikia kipindi nakuwa sielewi hizi ishu za mahusiano.

Mwenzenu nimekuwa kwenye mahusiano na mkaka wa miaka 33. Amenizidi miaka 4. Na tumekuwa naye kwa muda mrefu sana. Katika mahusiano yetu hayo, kiukweli sijisifii lakini nimejitahidi kuwa mwema sana kwake. Nimekuwa mnyenyekevu na msikivu sana kwa mwenzangu. Tofauti na wengi wanavyosema kuwa ukiwa hivyo unaleta upendo lakini kwangu mimi naona inakuwa tofauti. Badala ya upendo, naonekana kama mtu mjinga ambaye nimekufa na nimeoza kwake kiasi kwamba siwezi kujitetea kwa lolote.

Tabia hii kwa mwenzangu, ikazua yeye kuwa na wanawake wengine kisirisiri na inapotokea nimegundua anataka kunifanya mimi nionekane nimemkosea adabu! Kweli nina madhaifu kama binadamu, lakini kwa upendo wa dhati kwa huyu mtu kwa kweli nilikuwa nao.

Yeye mwenyewe anajua na hiyo ilimtia sana kiburi. Sasa amezua tabia mpya. Inapotokea naona mwenzangu anafanya mambo ya kipuuzi na kuwa na wanawake wengine, namwambia achague. Na cha ajabu anachagua mwenzangu mie naendelea na maisha mengine. Lakini haiwezi kupita mwezi bila huyu jamaa kurudi na kuomba msamaha sana.

Nimechoka hali hii na ninahitaji sana kuendelea na maisha mengine wadau. Naombeni mnisaidie mawazo yenu labda wapi nakwama na nini nahitaji katika suala hili la mahusiano maana naona ule uvumilivu na upendo unakufa na chuki inaibuka moyoni mwangu juu ya huyu kaka. Nilidhani ni hali ya kawaida ila sasa nina siku ya tatu akinitafuta, sina uwezo wa kuongea naye vizuri. Kwa mara ya pili toka tuanze mahusiano nimemtukana na nimemruhusu aende anapotaka kwenda.

Ila bado analalamika kwa marafiki zake kuwa nimekuwa mjeuri.

Ulijihakikishia kuwa huyo mtu ana tabia njema? Maana wengi wanalalamika lakini kumbe kajiingiza kwa vijana wale wanaokwenda kuscrub nyuso na kutia dawa ndevu!! Wale vijana wanasukwa na kwenda saloon za kike kukatwa kucha!!

Jitoe nae, kata mawadiliano nae, kumbuka mabaya yake pekee utasonga mbele!!

Hakikisha unaonyesha misimamo yako, ukisimamia kwamba tabia zako zimefanya nione wewe si mume mwema tena kwangu!! Hakikisha unasimama hivyo!! Unapobabaika na kubadili misimamo ndipo unampa credit ya kuwa hata akiharibu, atakubembeleza utarudi tuu!! Thus why anarudia rudia uovu wake kwako.

Laah! Endelea kuvumilia akuletee magonjwa!!
 
Hiyo sio kwa wanaume tu hata wanawake ila bref hakupendi huyo.
Fanya maamuzi,Kwenye mapinduzi yoyote lazima kuwe na wakati mgumu wa mapito"

Unaogopa kuachana nae kwa kuhofia huo wakati.
Hakuna wa kukuonea huruma hapa,bali jionee mwenyewe na nafsi yako ndio huruma pekee inayoweza kufanya kazi na kukuponya.

Usije ukasema haujaambiwa, ukitiwa chumvi huko shaulako.
 
Habarini zenu ndugu zangu?

Kwa kweli inafikia kipindi nakuwa sielewi hizi ishu za mahusiano.

Mwenzenu nimekuwa kwenye mahusiano na mkaka wa miaka 33. Amenizidi miaka 4. Na tumekuwa naye kwa muda mrefu sana. Katika mahusiano yetu hayo, kiukweli sijisifii lakini nimejitahidi kuwa mwema sana kwake. Nimekuwa mnyenyekevu na msikivu sana kwa mwenzangu.

Tofauti na wengi wanavyosema kuwa ukiwa hivyo unaleta upendo lakini kwangu mimi naona inakuwa tofauti. Badala ya upendo, naonekana kama mtu mjinga ambaye nimekufa na nimeoza kwake kiasi kwamba siwezi kujitetea kwa lolote.

Tabia hii kwa mwenzangu, ikazua yeye kuwa na wanawake wengine kisirisiri na inapotokea nimegundua anataka kunifanya mimi nionekane nimemkosea adabu! Kweli nina madhaifu kama binadamu, lakini kwa upendo wa dhati kwa huyu mtu kwa kweli nilikuwa nao.

Yeye mwenyewe anajua na hiyo ilimtia sana kiburi. Sasa amezua tabia mpya. Inapotokea naona mwenzangu anafanya mambo ya kipuuzi na kuwa na wanawake wengine, namwambia achague. Na cha ajabu anachagua mwenzangu mie naendelea na maisha mengine. Lakini haiwezi kupita mwezi bila huyu jamaa kurudi na kuomba msamaha sana.

Nimechoka hali hii na ninahitaji sana kuendelea na maisha mengine wadau. Naombeni mnisaidie mawazo yenu labda wapi nakwama na nini nahitaji katika suala hili la mahusiano maana naona ule uvumilivu na upendo unakufa na chuki inaibuka moyoni mwangu juu ya huyu kaka. Nilidhani ni hali ya kawaida ila sasa nina siku ya tatu akinitafuta, sina uwezo wa kuongea naye vizuri. Kwa mara ya pili toka tuanze mahusiano nimemtukana na nimemruhusu aende anapotaka kwenda.

Ila bado analalamika kwa marafiki zake kuwa nimekuwa mjeuri.
acha kupoteza muda wako kwa huyo jamaa, anarud sio kwamba anakupenda bali anajua ndo anapopendwa
 
Vibaya mno hapo jamaa anajikosha tu apige rungu dharau zirudi mbona atakoma afu jamaa pengine amtie na mimba kabisa atie kufuli ..Over
Si bora mimba utazaa?

Akimuomba kwingine kwa kigezo kwamba atatulia?

Atakataa kwa alivyokufa na kuoza?
 
Pole sana
Ila naomba uliza.... Jimbo lipo wazi ? Tuanze tuma maombi?
 
Wameachana kina Billgates nyie wengine ni kina nani hasa hapa chini ya jua
 
Back
Top Bottom