Nachukia sana kumcheat na inanipaga wakati mgumu sana ila unajikuta inakubidi automatically wewe imagine mnaishi ndio ila maisha mmnayoishi hayaeleweki bas tu kuna muda mtu hana time na wewe umerudii usiku kazini mmesalimiana kwema kwema umekula, umeoga kilamtu kulala usikumwema hakuna chakuongea,
Alafu kuna mdada huko haishi kukusumbua kwanza kukujulia hali asubuh,mchana na jion kuhakikisha kwamba uko salama ndo anapata amani,ukiwa na mastress yeye ndo wa kwanza kukufariji na kukutoa kwenye stress, unajitahid kumpotezea ili usije ukamcheat mkeo lakin wap Mrembo wawatu yumo tu anakomaa hakati tamaa ivi nikasema wacha nimvute tu karibu niruke nae maisha yaende kimya kimya je bado utanilalamikia kuwa Kwanini nimecheat et nauliza
Kwani ndoa mlifunga wawili tuu, hapakua na watu muhimu kuanzia pastor mpaka wazazi, ndoa yenu haina viongozi/mentors mnao waheshimu? Kwan uyo mke hana wakubwa zake? Kwani uliwezaje kumtongoza mpaka akushinde saivi?
Wanawake wanahitaji akili nyingi sana kuishi nao, haina formula, kila mtu anambinu zake so usije kukariri et mwanamke inatakiwa awe hivi au vile, kama bado hujakomaa kiakili bas usije kuleta lawama dhaifu kama hizi mbele ya watu wazima.
Neno la hekima kwako ni kua ndoa sio sehemu ya kupata furaha burebure, ndoa ni kama shamba biashara au kitu chochote kizuri hua ni unavuna unacho invest,
Moyo wa mwanamke/Mwanaume nikama battery mkiwa ndani ukiona mwenzako ananzakuzingua ujue charge imeisha na inabidi kujua ni nini uweke sawa maana kipindi mnaanza kupendana obviously kuna vitu mlikua mnafanyiana mpaka penzi likawa moto so ndani ya ndoa kazi hua ni kuvimaintain na kuvizidisha na iyo ndo hua shida.
Kama ulianza kwa kumnyenyekea mkeo mpaka akakukubali bas jua kwenye kichwa chake anatafsiri mapenzi ni kunyenyekewa na ampendae, kama ulitumia pesa kumpata ivo ivo akili yake itawaza upendo ni pesa au caring, so ukingia kwenye ndoa ukajifanya ooh ndoa inabidi mwanamke ndoa anyenyekee mwanaume bas jua we ndo mwenye makosa na unamkosea sana.
Kabla hujamlaumu mkeo fanya kutrack back jinsi ulivompata ulikua unamfanyia mambo gani? af jiulize saivi upo vipi!? kama ndo ivo unavyofanya na amezingua bas usiogope, toa taraka kaoe uyo anayejiweka karibu na wewe sio KUCHEAT.
Mi nimepitia magumu ya kunyimwa tendo zaidi ya miaka mi5 ila saivi napewa kama kawa sababu nilijua wapi sijakucharge nilipoanza kupacharge ye mwenyewe automatically akaanza kuniita mpaka naona usumbufu.