Wanaume kuweni makini sana kuoa wanawake waliotoka Vyuoni

Wanaume kuweni makini sana kuoa wanawake waliotoka Vyuoni

Uzi una comments nyiiiiiingiiii lakini nimesikitika sana wale feminist wa JF wameupita kushoto ila wanauzoom tu. Nimeona comments za wawili tu.

Anyways kaka apumzike kwa amani huko alipo. Mwanamke akishakua na KAZI au ELIMU ya CHUO inahitaji umakini sana kuanzisha nae mahusiano. Katika mwanamke wa kuoa siwezi gusa pisi za aina hiyo.
 
Nitoe tahadhari, hata hao wasio na elimu kubwa the same wana matatizo kama huyu binti msomi, wakipata mwenye pesa kukuzidi hakuna rangi utaacha kuona. Oeni wacha Mungu, hawa wanajua thamani ya ndoa hata kama ni wasomi wakubwa na wana pesa hawaharibu ndoa zao. Ndoa kwao ni sehemu ya ibada na ni maadili mema katika jamii. Kuoa kibishibishi kwa tamaa ya kuoa pisi kali au mbaya bila ku predict tabia zake mficho hatari kwa ndoa huja kuleta majuto baadae na ndoa kusambaratika
 
Enhee ikawaje? kaka yako naye anakunywaje sumu juu ya mwanamke aliyekutwa naye ukubwani?
Hayo mambo yasikie tu but hayana formula. how man percieve pain ni tofauti na mtu, wapo wenye experience so hawayumbi sana, wapo wageni lazima liwayumbishe, wapo wavumiliv wana suffer once after that wanakaa sawa
Ni kuomba Mungu akuvushe salama
 
Mimi nakuelewa sana Mkuu

Kuna jamaa yangu ni Daktari kabisa alioa Mhasibu msomi wa chuo kikuu wakazaa mtoto mmoja na tumemchangia kabisa kwny shughuli yake...juzi akaoa binti mdogo aliyeishia Fm IV

Ukimuuliza kulikoni? Anasema ameamua kumuoa Mwanamke anayemsikiliza na sasahivi ana amani tele

Kuna Wanawake wasomi hawafai kabisa kiukweli though sio wote
Mwanaume anahitaji kusikilizwa , problem is kwa wanawake wasomo wengi they cant provide that
 
Mume aheshimiwe na mkewe wakati huo mke asikilizwe na mumewe, tofauti na hivyo hakuna ndoa salama
 
Afu kuna mvulana anakuja anasema tafuteni Pesa B'se Mwanamke bila Pesa humuwezi



Pesa haiwezi kumkeep mwanamke kwa MWANAUME kamwe, ataact unyenyekevu at the beginning of relationship kwasababu ya Pesa na vitu na mali lakini akishapata UWEZO/Pesa hawezi kubaki b'se kilichokua kinamuweka keshakipata abaki afanyaje?


Kijana wa kiume kua na kitu kingine cha thamani ambacho halionekani kwa macho ya nyama na damu ambacho kitamfanya mwanamke awe proud of you and love you na Sio vitu vya kuonekana kwa macho ya nyama na damu hata kama una Pesa


Tengeneza mazingira mwanamke akupende upendo wa Kweli na sio kwasababu ya vitu au mali au Pesa
 
Kitu ambacho wanaume wengi hamkijui ni Tabia za mwanamke ambae Anajitafuta au ana hali ngumu kimaisha huwa ni kama simba jike mwenye njaa kali so chochote kitakachotokea mbele yake kama kimenona anapita nacho, Maisha ya Binti alietoka Chuoni hana kazi wala Pesa huwa ni kama Wife Material full adabu na utii

Ndio hawa wanawake wa vyuoni au waliomaliza na ajira hawana, simaanishi kuwa hawana haki ya kupata wenza ila uwe makini sana kuwasoma kabla ya kuwaowa, Hao wakishaolewa huwa wanaendelea kuhaso kutafuta ajira sasa usiombee atume maombi alafu ukute upo nae Dar alafu uskie kapangiwa kituo cha kazi Dodoma huko or Mwanza au apate kazi ya maana ukiwa nae hapo ndio utaanza kujua tabia zake halisi

Mwaka 2017 nilimpotezaga kaka yangu, alikipenda kibinti kikiwa mwaka wa pili chuoni akawa anakihudumia,hadi kinamaliza Chuo akakiowa bwana ila kwenye uchumba tu ugomvi ulikuwa hauishi maana kulikuwa na Tetesi yule binti alikuwa na mpenzi wake wa zamani kwa siri ila kilichompeleka pale kwa Bro ni pesa

Kaka akaowa kibishi, Ndoa iko Mwaka wa kwanza tu, Binti akala shavu Kigoma huko shirika linalodeal na wakimbizi pesa nje nje, Ndoa ndio ilipoanza kuwa ndoano hapo maana ilikuwa ni Marufuku kaka kumfuata yule Binti kigoma hadi arudi yeye Dar hao ni wanandoa yani

Za chini chini wambea wakamtonya Kaka kuwa yuke Binti huwa anamsafirisha yule Mwanaume wake wazamani hadi kigoma anafikia kwake mara kwa mara na anamrudisha Dar tena kwa Ndege, Na ndio maana Binti hakutaka kaka Awe anaenda kigoma

Kaka mwaka 2016 mwishoni akanywa sumu ila aliponyea kufa yote ni kama alipata sonona ,akawa hana mtu wa kumwambia, Baada ya lile tukio ndio akaipa Familia ukweli sasa, familia ikaweka kikao yule Binti akaitwa ila akasema yupo Bize Kigoma huko yote jeuri ya pesa na pumzi

Ikabidi sisi kama familia sasa tuongeze ukaribu uliopitiliza, ili ile hali iondoke tukawa tunakaa kwake kwa zamu yote kumpa kampani maana tulishaona Dalili mbaya na ndio tulikuwa tunamtegemea yani wadogo zake ametusomesha na kutupigania sana, Wifi tukawa tukimpigia simu hata kupokea hapokei

Mwaka 2017 mwezi wa Sita akaanza kuugua vitu visivyoeleweka mara Presha mara anadondoka kazini, Alipopelekwa Hospitali kwa uchunguzi ikaonekana Mishipa yake ya moyo imeanza kutanuka tukaambiwa anatakiwa arelax na aache kuwa mtu wa Mawazo , ila kila tukijaribu ikawa mtihani, 2017 mwishoni akafariki alidondoka tu bafuni kumkimbiza Hospitali tayari akawa ameshaondoka hili pigo siwezi kulisahau

Baada ya hili tukio kutokea Baba nae hadi leo hajawahi kuwa sawa kabisa, ila aliwaita watoto wake wote wa kiume kitu nachokumbuka alisema oweni wanawake wenye elimu za kawaida msije kusumbuana huko mbele, na akasema tumewasomesha kwa garama kubwa na sasa mna kazi zenu yeyote atakaeleta tena Mwanamke hapa kama ana Elimu ya juu basi huyo Mwanamke naye ni Sharti awe na pesa na kazi kabla hamjafahamiana yaani kiwaunganishe upendo sio Pesa mlizokuwa nazo

Akasema kuwa ukiniletea hapa Mwanamke Mwenye elimu ya juu na hana kazi wala pesa basi mkatafute baba mwjngine ampokee huyo mwanamke kama mnae la sivyo aishie huko huko, yaani Baba ni kama alivurugwa na ile hali

Ila wansemaga Dam ya mtu ni kama nzito or inaweza kukulilia ila sijui kama ni kweli but yule Binti mwaka 2022 Tabora huko, alipataga ajali mbaya sana Gari aliyokuwa anaendesha ikagongana na lori miguu yote ikabanwa mean ikasagika akakatwa miguu yote kwa sasa ni mlemavu kabisa hana miguu.
Hili suala ni kweli ndugu
 
Khakhakha wanaume wa JF wamekuskia ....
Chakushangaza sasa wanaolewa kila siku na wffgvcvcxxxc😂 nkae kimya tu maana nitavxcdgfdffggxddf
 
Ni vizuri na busara sana kuwa na akiba ya maneno. Usiwaone hao wanaochukua hayo maamuzi kuwa ni wajinga! Bado tu hujabananishwa!

Unaingia mzima mzima unajitoa unahudumia, unasomesha mpaka wewe unajisahau halafu mkeo anakuja kuanza kukudharau na kuchezewa na majamaa waziwazi. Kama huna kifua au support system nzuri linaweza kutokea la kutokea.

Hayanaga mwongozo!

Hayanaga baunsa!
Hayanaga Formulo
 
Uzi una comments nyiiiiiingiiii lakini nimesikitika sana wale feminist wa JF wameupita kushoto ila wanauzoom tu. Nimeona comments za wawili tu.

Anyways kaka apumzike kwa amani huko alipo. Mwanamke akishakua na KAZI au ELIMU ya CHUO inahitaji umakini sana kuanzisha nae mahusiano. Katika mwanamke wa kuoa siwezi gusa pisi za aina hiyo.
Jadda hajakomenti kabisa
 
Samahani lakini ukweli ni kwamba makosa ni ya kaka yako. Alikuwa anamng"ang'ania alitaka kuvumbua nini?
Ukishaona red flags mbili tatu piga chini..
Huko kwenye vikao vyenu wanaume huwa mnadiscuss nini?
 
Back
Top Bottom