Wanaume kuweni makini sana kuoa wanawake waliotoka Vyuoni

Wanaume kuweni makini sana kuoa wanawake waliotoka Vyuoni

Nitoe tahadhari, hata hao wasio na elimu kubwa the same wana matatizo kama huyu binti msomi, wakipata mwenye pesa kukuzidi hakuna rangi utaacha kuona. Oeni wacha Mungu, hawa wanajua thamani ya ndoa hata kama ni wasomi wakubwa na wana pesa hawaharibu ndoa zao. Ndoa kwao ni sehemu ya ibada na ni maadili mema katika jamii. Kuoa kibishibishi kwa tamaa ya kuoa pisi kali au mbaya bila ku predict tabia zake mficho hatari kwa ndoa huja kuleta majuto baadae na ndoa kusambaratika
Agiza chochote...bili juu yangu....namba yangu ni 0743$$$$$$
 
Hii ipo kwa pande zote hata kwa wanawake wapo kibao wamekula za uso kwa kukubali kuolewa na wanaume wanaojitafuta baada ya kuwewezeshwa na hao wanawake wakawatenda
Wachache sana mmoja kwa mia,kiasili mwanamke ni mbinafsi sana mbele ya hela yake.Wanawake wanaoweza kumvumilia mwanamme hasiye na kitu ni wachache mnooo.

Kundi jingine la wanawake wake hawafai hata kidogo Slay Queens, waanika matako na sura Social networks, yaani hawa piga acha.Kuna wapuuzi wengine wanakurupuka na kuishia kula za uso.
 
Kitu ambacho wanaume wengi hamkijui ni Tabia za mwanamke ambae Anajitafuta au ana hali ngumu kimaisha huwa ni kama simba jike mwenye njaa kali so chochote kitakachotokea mbele yake kama kimenona anapita nacho, Maisha ya Binti alietoka Chuoni hana kazi wala Pesa huwa ni kama Wife Material full adabu na utii

Ndio hawa wanawake wa vyuoni au waliomaliza na ajira hawana, simaanishi kuwa hawana haki ya kupata wenza ila uwe makini sana kuwasoma kabla ya kuwaowa, Hao wakishaolewa huwa wanaendelea kuhaso kutafuta ajira sasa usiombee atume maombi alafu ukute upo nae Dar alafu uskie kapangiwa kituo cha kazi Dodoma huko or Mwanza au apate kazi ya maana ukiwa nae hapo ndio utaanza kujua tabia zake halisi

Mwaka 2017 nilimpotezaga kaka yangu, alikipenda kibinti kikiwa mwaka wa pili chuoni akawa anakihudumia,hadi kinamaliza Chuo akakiowa bwana ila kwenye uchumba tu ugomvi ulikuwa hauishi maana kulikuwa na Tetesi yule binti alikuwa na mpenzi wake wa zamani kwa siri ila kilichompeleka pale kwa Bro ni pesa

Kaka akaowa kibishi, Ndoa iko Mwaka wa kwanza tu, Binti akala shavu Kigoma huko shirika linalodeal na wakimbizi pesa nje nje, Ndoa ndio ilipoanza kuwa ndoano hapo maana ilikuwa ni Marufuku kaka kumfuata yule Binti kigoma hadi arudi yeye Dar hao ni wanandoa yani

Za chini chini wambea wakamtonya Kaka kuwa yuke Binti huwa anamsafirisha yule Mwanaume wake wazamani hadi kigoma anafikia kwake mara kwa mara na anamrudisha Dar tena kwa Ndege, Na ndio maana Binti hakutaka kaka Awe anaenda kigoma

Kaka mwaka 2016 mwishoni akanywa sumu ila aliponyea kufa yote ni kama alipata sonona ,akawa hana mtu wa kumwambia, Baada ya lile tukio ndio akaipa Familia ukweli sasa, familia ikaweka kikao yule Binti akaitwa ila akasema yupo Bize Kigoma huko yote jeuri ya pesa na pumzi

Ikabidi sisi kama familia sasa tuongeze ukaribu uliopitiliza, ili ile hali iondoke tukawa tunakaa kwake kwa zamu yote kumpa kampani maana tulishaona Dalili mbaya na ndio tulikuwa tunamtegemea yani wadogo zake ametusomesha na kutupigania sana, Wifi tukawa tukimpigia simu hata kupokea hapokei

Mwaka 2017 mwezi wa Sita akaanza kuugua vitu visivyoeleweka mara Presha mara anadondoka kazini, Alipopelekwa Hospitali kwa uchunguzi ikaonekana Mishipa yake ya moyo imeanza kutanuka tukaambiwa anatakiwa arelax na aache kuwa mtu wa Mawazo , ila kila tukijaribu ikawa mtihani, 2017 mwishoni akafariki alidondoka tu bafuni kumkimbiza Hospitali tayari akawa ameshaondoka hili pigo siwezi kulisahau

Baada ya hili tukio kutokea Baba nae hadi leo hajawahi kuwa sawa kabisa, ila aliwaita watoto wake wote wa kiume kitu nachokumbuka alisema oweni wanawake wenye elimu za kawaida msije kusumbuana huko mbele, na akasema tumewasomesha kwa garama kubwa na sasa mna kazi zenu yeyote atakaeleta tena Mwanamke hapa kama ana Elimu ya juu basi huyo Mwanamke naye ni Sharti awe na pesa na kazi kabla hamjafahamiana yaani kiwaunganishe upendo sio Pesa mlizokuwa nazo

Akasema kuwa ukiniletea hapa Mwanamke Mwenye elimu ya juu na hana kazi wala pesa basi mkatafute baba mwjngine ampokee huyo mwanamke kama mnae la sivyo aishie huko huko, yaani Baba ni kama alivurugwa na ile hali

Ila wansemaga Dam ya mtu ni kama nzito or inaweza kukulilia ila sijui kama ni kweli but yule Binti mwaka 2022 Tabora huko, alipataga ajali mbaya sana Gari aliyokuwa anaendesha ikagongana na lori miguu yote ikabanwa mean ikasagika akakatwa miguu yote kwa sasa ni mlemavu kabisa hana miguu.
Malipo ni hapa hapa mbona, kule tunaenda kulala tu.
 
Kijana unaetaka kuoa tafuta binti darasa la saba sogea sogea mpaka form four or six weka ndani kula maisha.

Usicheze na hao wacheza porn vyuoni kwa kigezo cha kusaidiana maisha siku akipata kazi,na kiuhalisia hiyo ni sababu ndogo sana ya kukufanya uje kujuta cuz hakuna kusaidiana maisha kati ya mwanamke na mwanaume dunia hii hilo mnadanganywa na ma-feminaa
Ukioa mwenye elimu zaidi ya hapa ni ujinga
 
Wachache sana mmoja kwa mia,kiasili mwanamke ni mbinafsi sana mbele ya hela yake.Wanawake wanaoweza kumvumilia mwanamme hasiye na kitu ni wachache mnooo.

Kundi jingine la wanawake wake hawafai hata kidogo Slay Queens, waanika matako na sura Social networks, yaani hawa piga acha.Kuna wapuuzi wengine wanakurupuka na kuishia kula za uso.
Unataka kusema slay queens hawana moyo wa kumpenda mwanaume 😁 joseph1989
 
Mimi nashangaa sana

Mtu unaoaje strenger?

Inamaana kwenye kukua kwako hakuna wasichana mliokuwa nao mtaani wazuri tu

Au ulipoenda secondary hukuwa na target za wife material kichwani

Hata chuo miaka minne unaweza ukalenga mke anayejitambua tu

Mimi nashangaa sana

Mtu unaoaje strenger?

Inamaana kwenye kukua kwako hakuna wasichana mliokuwa nao mtaani wazuri tu

Au ulipoenda secondary hukuwa na target za wife material kichwani

Hata chuo miaka minne unaweza ukalenga mke anayejitambua tu
Oweni hata house girl wa baba mwenye nyumba mwenye akili ya maisha .
 
mke wangu alinambia nimsomeshee eti nimpeleke chuo akasome nlicheka mpka nkapaliwa...
Hapana mkuu,sio sawa.Kama mmezaa watoto nae,we mpeleke akasome.Mimi nilipofikia,siogopi mwanamke kunikengeukia,iwe ni kwa kuo gezeka elimu yake au pato lake. Ninachojua hawezi kuwatupa watoto wake,atawalea tu.
Mimi sihitaji fake loyalty.Ukitaka mwanamke awe loyal kwako kwa kumnyima elimu na chance ya kuongeza kipato,huenda akawa na mapenzi ya kinafki kwako.You never know, huenda pia mkeo yupo kati ya wale 1/100 ambao hata wawe na elimu na pato gani,bado wanaziheshimu ndoa zao.
Bila ya shaka miguu yake ipo busy Kigoma, Duh wahuni nyie hamkumpa jini lakini🤣🤣🤣
Wala sio jini,Karma is real
 
Taratibu mnaanza kuukubali uhalisia, kwamba mwanamke anamtii mwanaume endapo tu hana elimu wala ajira, tukiwaambia hali halisi iliyopo mnajidai mna mihemko na kuanza kututukana
Nyie wanawake ni wabinafsi sana, mwanamke akimdhuru mumewe, chama cha wanawake wa haki sijui za nini hakikemei, akifanyiwa ubaya mwanamke ndo kelele kibao mitandaoni.
 
Nyie wanawake ni wabinafsi sana, mwanamke akimdhuru mumewe, chama cha wanawake wa haki sijui za nini hakikemei, akifanyiwa ubaya mwanamke ndo kelele kibao mitandaoni.
Siyo ubinafsi bali ni kwa sababu jamii ilishaaminishwa kwamba mwanaume ni kiumbe strong hawezi kuzidiwa akili wala nguvu na mwanamke ambaye yeye ni kiumbe dhaifu, jamii ilishaaminishwa kwamba katika mgogoro wowote ule baina ya mwanaume na mwanamke siku zote mwanamke ndiye anayepoteza mwanaume yeye hana cha kupoteza hivyo mwanamke hatakiwi kushindana na mwanaume maana yeye ndiye atakuwa victim, sasa kutokana na hiyo imani iliyojengeka inakuwa ngumu kuamini kwamba eti wanaume nao wanadhuriwa na wanawake ndio maana wanaume wanapolalamika jamii inawapuuza kwa kudhani kwamba hayo malalamiko ni batili na hayana uhalisia
 
Back
Top Bottom