Story yako Imenikumbusha 2005,
Kuna Jamaa yangu traffic (tulisoma wote primary, Yuko morogoro) alinambia mkewe nesi kahamishiwa kikazi dar. Akifika nimpe sapoti.
Basi kipind icho namimi bado nahangaika na maisha, nmepanga. Nikampokea kwangu na baada ya siku 5 nikamtaftia nyumba akahamia chumba Cha kupanga mtaa mwingine karibu zaid na KAZIni kwake .
Basi Kuna siku akaniomba Kias flani cha pesa (nyingi kiasi), nikamwambia sina.
Akalia anashida nazo sana. Atarudisha mwisho wa mwezi. Basi Nikaenda kumkopea kwa mtu. Kurudisha Sasa ikawa kipengele. Pesa ya watu ikakaa sana kila mwezi anapiga kalenda.
Nilivomdai Sana,nikawa serious akachukia na Simu zangu akawa hapokei kabisa. Nami nikampotezea.Deni lile nikalilipa mwnyw maana mkopeshaji hamtambui uyo mdada.
Baadae jamaa yangu akawa ananiuliza maendeleo ya mkewe, nikamwambia Sijui chochote hatuna mawasiliano mazuri maana kaninunia. Sababu nikamwambia kila kitu. Jamaa akasema ataenda kuongea nae.
Jamaa alipoenda kumuuliza,
Mwanamke akajitetea kwamba hamna kitu Kama hicho, nilikua namtaka kimapenzi kinguvu kanikataa. Jamaa akaniita meza Moja na mwanamke. Huwez amini mwanamke yule bila kupepesa akasimamia Maneno Yale Yale kwamba namtaka. Honestly niliumia Sana. Kisha ikabd nijiweke pembeni zaidi na wao wote wawili. Ila jamaa hakunichukia, tukawa na mawasiliano ya juu juu tu.
2009, nikaja kukutana na jamaa kwenye msiba flani morogoro akanambia wameshaachana na uyo mkewe tangu mwaka Jana (2008). Alimfumania na mwanaume mwingine alikopanga nyumba ambae Ni mfanyakaz mwenzie daktari. Na waligombana Sana na uyo jamaa. Ila Mwanamke kamkana jamaa. Ikaisha hivyo.
Sasa 2010,nilikua na nyumba 1 kimara yenye chumban&sebule self ziko 2, uzio mmoja.
Basi Nikiwa dukan kwangu akaja jamaa mmoja akajitambulisha Ni daktari anasema kaambiwa kwangu napangisha, anahitaji chumba na sebule self. Nikasema umepata. Kodi Ni Kias flan. Akasema sawa ila mpk apakague.
Nikamwambia Kama uko tayar nikupe kijana akakuonyeshe maana pamefungwa.
Akasema yeye ana HARAKA, ila MKE wake atapitia Hapa jion akapakague akiridhika nako sawa, yeye atalipia. Nikasema POA.
Jion sim ngeni ikaingia,
Mwanamke anajitambulisha yeye Ndo MKE wa jamaa anataka akakague iyo nyumba. Nikamwmbia njoo dukan nikupe kijana akupeleke . Akasema kwasababu dukn Ni mbali nimpe kijana funguo wakutane kwny nyumba akakague. Nikasema sawa.
Baadae usiku mdada kanipigia anasema Yuko na kijana na karidhika Napo, ila kitasa Cha mlango wa chumbani Ni kibovu. Nikamwambia Kama anaweza arekebishe mwnyw atapunguza kwenye pesa yake ya Kodi Ila asifunge kitasa cha kuzidi elfu 20.Akasema sawa. Kijana akamwachia ufunguo.
Kesho yake saa 8 ananipigia kwamba tayar keshafunga kitasa Cha elfu 10, elfu 5 ufindi, jumla elfu 20. anikute wapi anipe Kodi yangu ilobaki. Nikamwambia ailete dukani kwangu
Gafla jion Niko ofsin,
Akatokea yule yule mwanamke tuliegombana nae kipind kile, kuniona akawa anajichekesha TU. Sikuonesha kinyongo nae pale pale. Akanipa Kodi yangu pungufu ya elfu 20 ela ya kitasa. Ila akasema atahamia wikendi j.mosi au j.pili. nikasema "sawa"
Baadae ameshaondoka,
Nikatafakari sana kua kumpangisha kwangu uyu mpuuzi utakua Ni ufala na dharau. ukzngatia story ya jamaa yake kua alimfumania na mfanyakaz mwenzie. Nikamkumbuka yule dokta alokuja kutafta chumba kwangu akajitambulisha Ndo mme wake.
Baada nikahisi jamaa akija kujua uyu mpuuz kapanga kwangu, na anaishi na mwanaume alomfumania nae. hatonielewa hata kidg.Ikabd niipangue gia angani.
Ijumaa ikabd nipigie kua sikujua kumbe MKE Wangu niliposafiri akishapangisha tayar kwa mtu mwingine na anahamia MDA wowote ule. Na Ela alishakula wife. Tunafanyaje sasa. Kitasa Chako unang'oa au nikurudishie Ela yako. Akasema kibaki nimrudishie TU elf 20 yake pamoja na Kodi yake. Akasema anaifata dukan. Nkasema sawa
Kaja dukan analalamika sijamfanyia fair, kapapenda na alishafanya Hadi usafi tayar. Nikamwambia Mimi mwnyw sikujua, wakulaumiwa Ni wife. Akachukua 20 + Kodi yake akaondoka zake
Sasa mistake Ni kwmaba wife sikumshirikisha huo uongo. Mwaka 1 mbele sikuMoja wife ananambia kukutana na uyo mdada k'koo wamepiga story na anamlalamikia yeye khs nyumba. Afu wife kanikana hajui chochote maana simshirikishagi kwny kupangisha nyumba.
Hapo nikajua Moja kwa Moja,
Uyo mdada keshajua tayar kua nilimfanyia kusudi TU umafia kumbadilishia gia angani pale kwangu.[emoji4]